-
Somo La Kwanza
-
Somo La Pili
-
Somo La Tatu
-
HATUA YA NNE
-
NAHAU ZA KISWAHILI
-
VITENDAWILI
-
METHALI
Methali
Methali
Ili kuuhifadhi utamaduni wetu na hekima za wahenga wetu mthali zimebuniwa kama methali zetu hazahifadhiwi, iko hatari kwa watoto wetu na wajukuu wetu kuzisahau kabisa. Kutokana na lahaja mbalimbali za Waswahili, methali huwa na maana sawa na nyingine lakini kna baadhi zinahitilafiana sana na badhi hazihitilafiani sana.
Zifuatazo ni methali zilizozoelekwa katika upwa wa Afrika Mashariki hasa sehemu za Mombasa, Tanga na Zanzibar.
- Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge
Maana ya neno ‘mbele’ ina maana ya ‘kabla ya wengine’. Maji maenge ni maji yaliyo safi yaliyotuama na takataka zake zikawa chini.
- Ajengaye siye alalaye Maana yake mtu anayeienga nyumba si lazima ailale. Anawezaa kuijenga akafana asslale au akiilala siku kidogo tu ikawa akarithiwa na wanawe, wakailala kwa siku nyingi zaidi.
- Bao nene si chuma chembamba. Maana yake ni kwa hata bao likiwa nene kiasi gani ni hafifu sana mbele ya chuma hata kikiwa chembamba kiasi gani.bao kinyume cha chuma ni kitu kiozacho, kiwezacho kuvunjika upesi.
- Chamb chma ni Baraka ya mvuvi. Maana yake ni kuwa Chambo ni aina ya chakula kinacholiwa na samaki ambacho wavuvi hukitumia katika kuwatega samaki ili wawashike.Kwa hiko kila mvuvi atumiapo chambo chema atapata samaki wengi (atabarikiwa).
- Endaye shamba mjini kwema. Maana yake ni kuwa Waswahili wana desturi kuwa na mashamba yao mbali na mjini wanapokaa. Hivyo, mtu atakapo kwenda shamba humbidi afunge safari. Kwa kuwa shamba aendako ni mbali na mjini, huwa haodoki mpaka kuwe kwema yaani kwe hakuna tatizo.
- Fungato haiumizi (hauvunji) mkono. Maana yake ni kwa fungato(mzigo unaofungwa vizuri) hauna vitu inavyochopoka ovyo. Mzigo w aina hiyo hubebeka vizuri na haumchokeshi mwenye kuubeba. Kinyume cha mzigo ambao haukufungwa vizuri unaoumiza mikono kwa kutaka kuvizuia vilinyomo visichopoke.
- Kidolechema huvishwa pete. Mtu akitaka kuvaa pete hataivaa kidole chochote bali ataangalia kidole kipendezacho akivishe. Hataivaa katika kidole cha mguu au kidole gumba
- Sikio la kufa halisikii dawa, maana yake yule mtu ambaye saa yake ya kufa imeshakufa, hataujaribu vipi kumpa dawa ni kazi bure.
- Tunda jema halikawii mtini yaani tunda zuri litaonekana haraka na litapurwa. Kitu kizuri hakichelewi kupata anayekitaka
- Kuchunga na peku ni kukosa ungo. Ungo ni aina ya chombo Waswahili huatumia kuchungia (Kupepetea) vitu kama mchele, mahindi mbaazi nk. mahindi, mbaazi na kadhalika. Peku ni ungo uliotumiwa siku nyingi na baadaye ukawa umevuja. Kwa hiyo mtu akitumia pekuni dlaili kwamba hana ungoAngekuwa na ungo hangetumia peku.
Prev
Vitendawili