KISWAHILI KWA SHULE ZA SEKONDARI (Kidato cha 1 – IV)

Misingi ya kufundisha somo la KiswahiIi

Misingi ya kufundishia somo la
Kiswahili
Ili kufundisha vizuri Kiswahili ni
muhimu kujua angalau mambo ya
lazima ya kuzingatia katika mchakato
huu. Si vyema kumlaumu mtu
aliyejikwaa akaanguka. Ni vizuri
ukatafiti kidogo ili kujua sababu za
kuanguka kwake.Unaweza kugundua
kuwa mtu yule haoni. Kuona ni msingi
muhimu kujikinga na kujikwaa.
Tunaelewa kuwa lugha hufundishwa
kwa kuzingatia stadi za kusikiliza,
kuzungumza, kusoma na
kuandika hivyo, tunapofundisha stadi
hizi kuna misingi ya kuzingatia.
2.1 Malengo

Baada ya kusoma na kuzingatia ada hii,
utaweza:
a) Kufafanua maana na umuhimu
misingi ya kufundishia somo la
Kiswahili
b) Kufafanua misingi ya
kufundishia somo la Kiswahili
c) Muda: Saa3

d) 2.1.1 Maana na umuhimu wa
misingi ya kufundishiasomo la
Kiswahili
e) Bila shaka katikaufundishaji wa
somo la Kiswahili kuna taratibu
maalum za kufuata kama ilivyo
katika lugha nyingine. Ni kama vile
unapotoa jaribio la lugha darasani
hutatoa karatasi za maswali na
kuondoka huku ukiwaacha
wanafunzi wanafanya jaribio hilo
Lazima utaweka utaratibu kama vile
kuwa na msimamizi muda wote ili
wanafunzi wasiweze kutazamana
na kufanya udanganyifu, kuheshimu
da wa kuanza na wakumaliza na
uwepo utulivu darasani
f) Ufundishaji wa Kiswahili nao hufuata
utaratibu maalumu.Misingi ya
kufunndisha Kiswahili ni hii
ifuatayo:
a) Kuwapo na pande mbili
zinazoshirikiana katika
mawasiliano(Kusikiliza na
kuzungumza)
b) Kusoma kwa kuelewa
c) Kumudu stadi za utungaji
d) Kujieleza kwa kina na kwa
ufasaha
e) Kumudu stadi za Ufahamu
f) Matumizi ya lugha ya kisanii
g) Mawasiliano ya masafa
h) Kanuni za lugha
2.1.2 Ufafanuzi wa Misingi ya
Kufundishia Kiswahili

a) Kuwapo kwa pandembili
zinazoshirikiana katika mawasiliano (kusikiliza na
kuzungumza)
Stadi za kusikiiza na kuzungmza huenda kwa pamoja
kwa kuwa mawasiliano hudai kuwapo kwa pande
mbili. Pande hizo ni kuzungumza na mtu
anasikiliza. Kwa hiyo kanuni ya kwanza katika stadi
hizo ni kuwepo kwa pande mbili za mawasiiano
Ili mtu aelewe kinachozungumzwa ni lazima
asikilize kwa makini. Kama anasikiliza juu juu
hatapata ujumbe kamili alioelezwa. Fikiria mtu
anayesikiliza tarifa ya habari redioni katika eneo la
sokoni
Sokoni kuna shughuli na kelele nyingi. Unafikiri
ataweza kuelewa taarifa hiyo vizuri? Kelele za sokoni
zitamzuia kusikiliza kwa makini. Kwa hiyo kanuni
nyingine ni kusikiliza kwa makini.
Tunasema mawasiliano ni pande mbili:unaotoa na
unaopokea. Tunasema pia kuna mpokeji asikiliza
kwa makini. Lakini ni lazima pia mzungumzaji
atamke kwa usahihi. Mzungumzaji akitamka kwa
makosa hataelewa au ataeleweka kwa namna
tofauti na kusudio lake. Mtu huyo ataeleweka,
lakini ujumbe hautaeleweka haraka. Wakati
mwingine mtu huyo ataeleweka lakini
ujumbe hautaeleweka haraka kwa kuwa msikilizaji
atatumia muda kufikiria matamshi yake na maana
iliyokusudiwa.
Kwa mfano,mzungumzaji anapotamka sehemu
zifuatazo:
a) Shasha mnakwenda wapi?
b)Mimi nimethema twende huko
c) Yule ntoto mkubwa amelala.
d) Ndio nakwenda huko kwa ndugu wangu.
Utamkaji huo haufikishi ujumbe kwa ufasaha na
kwa kasi inayotakiwa.

Kwa hiyo hapa tunaona
kanuni nyingine ya utamkaji kwa usahihi.
Baaadhi ya watu huzungumza kwa mtindo
tofauti.Je, mtu akinong’ona na wewe uko mbali
kidogo utasikia anachosema? Ni wazi kuwa
hutasikia na hutapata ujumbe aliokusudia
kukupatia.Sauti ndogo ya kunong’ona hufifisha
mawasilano Kwa hiyo kanuni nyingine ni
kuzungumza kwa sauti na kuzingatia lafudhi ya
Kiswahili.
Kwa hiyo kanuni mojawapo ya stadi ya kusikiliza
na kuzungumza ni usomaji wa vitabu eneo hilo la
kusikiliza na kzungumza.
Kama mtu hazumgumzi lugha fulani kwa muda
mrefu anapungukiwa na ujuzi wa lugha hiyo. Hali
hii inawatokea Watanzania wanaokwenda
kusoma nchi za Ulaya kusikotumika Kiswahili.
Baada ya kuhitimu masomo yake Mtanzania huyu
anapata shida sana kurekebisha uzungumzaji
wake wa Kiswahili. Je, asiyetumia Kiswahili kwa
miaka kadhaa anapungukiwa na vipengele gani
vya lugha?
Kwa hiyo hapa kuna kanuni nyingine ya kuzungumza
lugha haiyo mara kwa mara. Katika msingi huu wa
kuwepo kwa pande mbili zinazoshirikiana katka
kuwasiliana, kuna kanuni ndogo zinazozingatiwa na
vipengele gani vya lugha?

Kwa hiyo hapa kuna kanuni nyingine ya
kuzungumza lugha hiyo mara kwa mara. Katika
msingi huu wa kuwepo kwa pande mbili
zinazoshirikiana katika kuwasiliana kuna kanuni
ndogo zinazozingatiwa ambazo zimeelezwa pia.

b) Kusoma kwa kuelewa
Katika shule za sekondari inatwaliwa kuwa wanafunnzi
wanajua kusoma na kuandika. Walijifunza stadi hizo
katika shule za msingi. Hata hivyo, ni muhimu itamkwe
kwa uelewa ili mtu asome, lazima atambue umbo la herufi
baadaye aelewe maana ya neno na hatimaye aelewe
maana ya sentensi. Kwa hiyo kuna kusoma kwa utambuzi
na ksoma kwa uelewa. Katika sekondari msisitizo
huwekwa katika kusoma kwa kuelewa na kwa
burudani.
Inafaa kuwaelekeza wanafunzi wasome kitabu au andiko
Fulani kwa malengo maalum lakini ni vizuri zaidi
kuwaelekea wasome wakizingatia mambo muhimu. Hali
hii inawasaidia kumakinika na usomaji wao. Ni muhimu
kwapa maswali ya Ufahamu na yanayofikirisha baada ya
kusoma matini. Maswali yalenge ngazi ya juu ya kufikiri.
Maswali hayo ni kama, Kwa nini mtunzi wa riwaya
amemchora muhusika bapa katika nafasi hii? Unafikiri

Kinjeketile aliwasaidia wana chi katika vita ya Majimaji?
Toa sababu za majibu yako.
Ni muhimu pia kuwaelekeza wanafunzi wasome haraka.
Usomaji huu hauzingatii kuelewa kwa kina Unazingatia
kusoma na kupata maana ya jumla. Usomaji huu ule
unaotumiwa sana na watu wenye haraka wanaposoma
magazeti na majarid. Mtu anayesoma kwa utaratibu huu
anapata muono wa jumla katika mambo anayoyasoma.
Katika usomaji huu naweza kujibu maswali ya jumla tu
na sio ya kina.
Ili kuwawezesha wanafunzi wasme kwa kina na kwa
jumla lazima awaongoze wasome kwa muda
uliowapangia. Usomaji wa kina unahitaji muda mrfu
kuliko usomaji wa jumla. Pia maswali ya usomaji kwa
makiniyatakuwa yanaai fikra za kina. Yale ya jumla
yanadai majibu ya jumla tu. Katika usomaji ni kuhimu
kuzingatia kuwa matini unayoapa wanafunzi ilingane na
umri na mapendeleo yao. Pia matini zisiwe ndefu mnoa
kiiasi cha kuwachisha wasomaji nakwakaisha tamaa. Kwa
hiyo huu ni msingi wa kusoma kwa kuelewa.
c) Utungaji ( Stadi za kutunga insha na habari).
Kuandika kuna viwango vyake. Kiwango cha awali
kinafundisha kuumba herufimoja moja na hatimaye
kuumba maneno, sentensi na aya. Hatua ya kuumba herufi

inafanyika katika darasa la kwanza na la pili. Katika
sekondari msisitizo unakuwa kwenye kutunga habari
mbalimbali. Habari hizo zinaweza kuwa baruaa,insha,
haithi, matukio/visa mashairi, tamathali za semi, nk.
Mwalimu ni mambo gani utayasisitiza kwa wanafunzi
wako unapowaelekeza waandike barua, insha, nk.? je,
unataka mpangilio wa mawazo kimantiki? Je, unataka
watoe mawazo umuhimu kwa jamii? Je, unataka watoe
sababu za kutetea maazo wanayotoa? Je, unataka
wasimulie au waeleze kwa Kiswahili sanifu? Je, utapenda
watumie lugha ya kisanii mahali panapofaa? Kwa kila
swali ni vizuri utoe sababu a majibu yako.
Katika kuunga kituni lazima mtunzi aunde insha yake
katika mpangilio wa Utangulizi, Kiini na Hiimisho. Kwa
mfano: “Unataka kuelez uovu w wizi wa fedha serikalini
na jinsi atakavyovielelzea hasara zake kwa raia wa
kawaida. Mtunzi atajitahidi kutafuta ushahidi wa mambo
anaytka kuyasema hata kama ni ya jumla tu. Kwa mfano,
somavidokezo vituatavyo halafu waongoze wanafunzi
wavitumia katika kuandika insha:
“ Mhibiti wa fedha za Serikali alibaini matumizi asiyo
halali ya shilingi bilioni moja mwaka jana. Fedha hizo ni
za magazetini.hapo hapo tunaambiwa hospiali nyingi
hazina dawa, shule nyingi hazina vitabu na madawati ya

kutosha. Barabara nyingi vijijini ziko kaika hali mbaya.
Kwa jumla umasikini kwa raia Tanzania umeongezeka.”
Utungaji kwa wanafunzi kwa kutumia vidokezo hivyo
unakusudia kuimarisha upeo wao wa jinsi yakuwaelekeza
wanafunzi katika staddi za kuandika
Mazingatia hayo yote ndiyo unaounda Misingi ya
Kufundisha Utungaji
d) Kujieleza kwa Kina na kwa Ufasaha
Lengo kuu la kuzugumza ni kufikisha ujumbe. Watu
huzungumz ili washawishi wenzao wakubaliane na
mawazo ya mzunumzaji. Ili uweze kushawishi fikra za
wenzako ni lazimaueleze fikra zako kwa utaratibu
unaokidhi mahitaji yako. Si rahisi kumshawishi mtu kwa matusi au kumkashifu au kumpuuza. Ukifanya hivyo
kwwa hakika utamfanya akatae mawazo yako badala ya
kuyakubali. Kujieleza kwa kina na kwa ufasaha kunahitaji
msemaji awe na heshima na uvumilivu kwa hadhira
ayake. Msemaji awe na sauti ya kusikika na inayobadilika
kulingana na jambo analosema. Kama anasisitiza jamo
basi asuti ibadilike ikionyesha msisitizo huo.
Kwa hiyo katika kujieleza hadharani lazima mzungumzaji
awe na jambo maalumu la kuzngumza , pangiio mzuri wa
mawazo, lugha ya heshima na hoja zenye ukweli na

uthibitisho. Hii ni kanuni ya kujieleza kwa kina kwa
mdomo.
Inapokuwa lazima kujieleza kwa kuandika, hali
inakuwaje?
Kuandika kunawakilisha sauti z kujieleza kwa mdomo.
Kwa kuwa hapa hapana sauti. Ni lazima msemaji afuate
taratibu za uandishi. Taratibu za andishi ni pamoja na

Dodoma. Aaaa Mwambe sasa hapana, ujue wanakuona na
si ajabu wanaumia sana kwa namna unavyowakomalia.
Sasa ukisimama tu wanaangaliana sijui jamaa anataka
kuibuka na jambo gani na kwa nani au wakati mwingine
watakuzuia kusema.
Yaani jana mbunge Cecil Mwambe alipewa nafasi ya
kuuliza swali la nyongeza lakini badala ya kuuliza kuhusu
kilimo yeye akataka wawekeane ahadi na Waziri kama
akishindwa kusimamia kauli yake eti ajiuzulu.
Huyu mbunge nakuambia hajawahi kupoa kwa mawaziri
sema viongozi wanaokaa kwenye viti huwa wanaokoa
jahazi tu.

Lakini Mwambe Waziri Japhet Hasunga alisema kwamba
soko la mahindi lipo lakini unasema eti akishindwa
ajiuzulu?
Hivi yule uliyemtaja kwenye rushwa sakata hilo lilifikia
wapi, je ukishapewa vielelezo na lini itasomwa
bungeni.umizi sahihi ya alama za mkat, nukta, ulizo,
mshangao,nukyamili, nukta na mkato, aya, mpangilio wa
mawazo, uteuzi wa maneno na tamathali zasemina usafi
wa andiko zima.
Pamoja na kufauata taratibu hizo lazima mwandishi pia
awe na utaratibu wa kumpeleka msomaji taraibu kwenye
andiko. Kwa kifupi lazima mwandishi aanze na
utanguliziwenye kumwarifu msomaji mwelekeo wa
mwandishi. Baada ya hapo kinauata kiini cha adiko .
Hapa ndpo mwandishi hueleza madhumuni ya andiko na
kujenga hoja ya kutetea jambo analoshawishi. Haimaye
mwandishi anahitimisha anndiko lake kwa kukazia hoja
alizojenga na kusisiiza mamo makuu aliyosema. Kwa
hiyo kutumia vizuri taratibu na alama za uandishi ni
kanuni za kujieleza kwa kina kwa kuandika. Mazigatio
haya ndiyo yanayojenga msingi huu wa kufundisha,
kujieleza kwa kina na kwa ufasaha.
e) Ufahamu (Stadi za kupata Ufahamu kwa
kusikiliza na kusoma.

Kuna Ufahamu wa kusikiliza au kusoma kwa sauti
kusoma kwa sauti unalenga katika kumuimarisha
mwanafunzi kwenye matamshi na lafudhi ya Kiswahil
sanifu. Pia kana anasoma shairi basi anatakiwa alisome
shairi, Kwa hiyo hapa kunakanuni ya usomaji wenye
sauti ya kusikika n lafudhi sahihi. Hapa wanafunzi
wanaposoma lazima mwalimu uw makini kuwasikiliza
nna kuwasahihisha matamshi na lafudhi wanazotumia.
Katika Ufahamu wa kusoma kimya lazima msomaji
afuate taratibu a usomaji kima. Hapa hapatakuwa na
minong’ono wala mighuno . Usomaji huu unatakiwa
upangiwe muda. Wasomaji wasome kwa
mudauliopangwa na kujibu maswaliyaliyopangwa.
Lengo hapa ni kuwafanya wazoee kusoma haraka na
kuelewa jambo walilosoma . Hatimaye msikilizaji au
msomaji anatakiwa ajibu maswali ya Ufahamu wa
kusikiiza na kusoma
Ufahamu unajumuisha ufupisho. Ufupisho ni htima ya
kubaini mawazo makuuna madogona kuweza kupunuza
maneno yasiyo ya lazima sana ia kuathirimaana a
misingi ya aya au kifungucha habari. Mara nyini
maneno haya ni vivumishi, vielezi na vihusishi. Wakati
mwingine hata sentensi nzima inaweza kutokuwa ya
lazimakatika habari hiyo. Ka hiyo inaweza kuondolewa
bila kuleta madhara katika maana ya kiini cha habari.

Katika kufundisha Ufahamu unaweza kuandaa kifunu
cha habari/matini kulingana na kiwango cha wanafunzi
kisha kuwapa maswali ua Ufahamu waisome na kisha
wajibu maswali yanayofuta. Majibu yao yawasilishwe
darasani na kujadiliwa.
Taratiu hizo ndizo zinazounda Msingi wa Ufahamu.
Matumizi ya lugha ya kisanii.
Lugha ya kisanii ni mpangilio wa maneno
unaoshawishi fikra kwa njia rahisi. Ni mmaneno
yanayomvuta msomaji au msikilizaji kuendelea kusoma
au kusikiliza. Utaratibu huu hujumuisha takriri silabi,
takriri maneno, takriri sentensi, maneno ya msinyao,
vielelezo vya sauti, maneno yanayojenga taswira kali na
butu, misemo, misimu, na tamathali nyinine za semi.
Lgha ya kisanii huumika kwenye mazungumzo na
katika uandishi wa riwaya, tamthiliya na mashairi. Kwa
hio hapa unaona kanuni ya kutumia lugha ya kisanii
katika mawasilianomuhimu a ya kila siku. Lugha hii
inaweza kujitokeza kwenye matmzi ya nahau,
methali,msimu, tamathali za semina miundo mingine.
Katika ufundishaji na ujifunzaji unawea kuwaongoza
wanafunzi wako wa kidato cha pili wakusanye nahau,
methali, misemo mbalimbali zinazopatikana kwenye
tarafa au kata yao. Waziwasilishe darasani na

kuzichambua. Wape wanafunzi mazoezo kkadhaa ya
kuitumia semina nahau hizo katika sentensi au hhabari
wanazotunga wenyewe. Hatimaye waziandikie
ufafanuzi au maelezo ya maana, matumizi na umuhimu
wake katika jamii.
Waongoze wanafunzi katika kuziboresha kazi zaona
kuzihifadhi kwenye mafaiali na rafu za darasani mwao.
Wape wanafunzi nafazi ya krejea kwenye maandiko
hayo waliyoyakusanya.
Kwa hyo hapo utaona kanuni ya kwashirikisha
wanafunzi katika kukusanya na kuhifadhi kkazi za
kisanii.
Kanuni hizi zilizofafanuliwa ndizo zinazounda Msingi
wa kufundishia matumizi ya lugha ya Kisanii.
Mawasiliano ya Masafa
Mawsiliano ya Masafa ni upelekeji wa habari kwa mtu
au watu walio mbali. Watu huwasilianaili kufikisha
ujumbe. Kutoa maelekezo, kushawishi au kuhamasisha,
kutoa ushauri au mapendekezo , kujibu hoja, kuweka
kumbukumbu, kshukuru na kupongezha. .
Mtu anapowasiliana na mwenzake anaweza kutumia
simu, barua, barua pepe, utaratibu mwingine, nk Hata
hivyo mtu hupenda aju hali na hadhi ya mtu
anayewasiliana naye. Hali hiyo husaidia uteuzi wa

maneno, mpangilio wa maneno hata urefu wa matini.
Kwa mfano kama mtu huyo ni wa rika lake anaweza
kutumi ahata utani wa kiwango hicho. Kama mtu huyo
ni mzee basi mzungamzaji anaweza kutumia lugha ya
heshima inayolingana na umri na hadhi ya huyo mzee.
Kwa hiyo kuna kanuni ya kujua unawasiliana na njia
zinaotumika kuwasiliana . Kanuni hizi ndizo
zinazounda Msingi wa Kufundishia Mawasiliano ya
Masafa.
Kanuni za Lugha
Kanuni zinazotawala lugha ni matamshi na lafudhi
sahihi, kutamka au kuandika neno katika mo sahihai,
matumizi ya miundo kwa usahihi ma kutumiamaneno
kwa maana sahihi.
Matamshi au kuandika neno kimmakosa
linawezakubadili maana iiyokusdiwa Hebu tuchunguze
kaui zifuatazo na kujiuliz maswali:
Wewe nu mvivu? Wewe ni mvuvi.
Je kauli hizi zinamaana moja? Toa sababu a majibu
yako.
Ni kauli ipi ina sauti kali?
Je, sauti hiyo kali inaashiria nini?

Kauli ya kwanza ni swali ambalo muuzaji anaweza
kujibu bila kukasirika. Lakini kauli yapli ni kaui thabiti.
Hapa mzungmzaji ana hakika kuwa huyo mwingine ana
tabia ya kutopenda kujishughulisha katika kazi.
Kauli hii ya pili inaweza kuzusha ubishi na hata
ugomvi. Kwa hiyomatamshi huweza kubadili maana ya
kilichokusudiwa.kama mtu alitoa kauli ya piliakiwa na
maana ya kauli ya mwanzo, wanaweza kushangaa na
kushtuka anapokabiliwa na shutuma na misukosuko ya
kuambiwa amemkshifu mwenziwe.
Kuweza kumudu matumizi ya kauli nne za lugha ni
msingi mmojawapo wa kufundishia Kiswahili. Kanuni
za lugha zimefuatwa, zinaimarisha matamshi sahihi,
zimetumia maneno katika maumbo yake kwa usahihi,
kutumia maneno katika mpangilio sahihi.
Kwa hiyo misingi inayotwala ufundishaji wa somo la
Kiswahili ni:
a) Matumizi ya matamshi sahihi
b) Kuzingatia maana za maneno
c) Kutumia maneno katika maumbo yake sahihi
d) Kuzingatia mpangilio sahihi wa maneno katika
sentensi.

Leave a Reply