-
Somo La Kwanza
-
Somo La Pili
-
Somo La Tatu
-
HATUA YA NNE
-
NAHAU ZA KISWAHILI
-
VITENDAWILI
-
METHALI
Nahau
NAHAU ZA KISWAHILI
Maelezo mafupi yanatakiwa kukushirikisha katika utajiri mkubwa wa lugha ya Kiswahili katika hadithi, misemo methali, nahau, vitendawili na semi mbalimbali.Hakika hizi ni tunu zenye maarifa, hekima na sanaa iliopo katika jamii ya Waswahili.
Maudhui yaliyomo humu yanalengo l kutumika nyumbani na shuleni. Wazazi, walezi na pia walmu wataweza kutumia fursa zao kuwafunza watoto na vijana kwa kuwajengea wezo na umahiri wa kutumia Kiswahili
Nahau ni nini?
Ni Maneno ya kawaida yenye maana ya uficho ambayo haiendani na maana ya kawaida. Kwa maana nyingine nahau ni Maneno ya kawaida ambayo hayana maana ya kawaida. Kwa mfano iko nahau isemayo”kalia kutu kavu.” Huwezi kupata maana yake kwa kufikiria pekee tu bali kwa kujifunza. Hapa mtu kuwa katika hali ya hatari.
Kwa nini nahau zipo?
Nahau hutumika kutoa ujumbe kwa njia ya uficho. Njia hii hupunguza makala hutoa heshima. Kwa mfano unasema.
“Babu ameaga dunia” Babu amefariki dunia.
“Mjomba ana mkono wa birika” Mjomba ni mchoyo. Angali mifano ya nahau ifuatazo:
1. Acha mkono (Ametuacha mkono)= fariki, kufa,aga dunia.
2. Achiwa mikoba (Fundi John amemwachia mikoba mwanawe wa pili) = Kurithishwa madaraka au majukumu.
3. Bwaga manyanga = Shindwa, kubali kushindwa
4. Changa la macho+uongo, utapeli/danganywa.
5. Veza upatu= Changishana fedha na kupeana kwa zamu
6. Debe shinda= Mtu asiye na uwezo au ujuzi wa jambo fulani.
7. Kaa chonjo= chukua tahadhari, jiepushe na jambo
8. Kaa pwetepwete= legea mwili, kaa kizembe bila kufanya lolote.
9. Kata mbonji= lala usingizi,
10. Kausha/kaushia= nyamazia jambo kwa kujifanya kama hujaona au kusikia jambo.
11. Kutokuwa na kichwa miguu= kukosa mwelekeo au msimamo’
12. Kwa udi na uvumba= Tekeleza jambo ka namna yoyote ile iwezekanavyo
13. Piga jeki= Toa msaada kwa mtu hashspale anapkuwa amekwama (kibiashara au kifedha).
14. Tumbo moto= Hofu, wasiwasi
15. Tupa karata = bahatisha,
16. Piga kitabu= soma sana, soma kwa bidi
17. Vua macho= Tazama kwa makini, sehemu/mahali
18. Vunja mbavu= Chekesha sana
19. Vuta pumzi= Pata mapumziko
20. Weka uzibe= Zuia jambo nyima mtu
21. Zunguka mbuyu/pita mlango wa nyuma= toa rushwa/hongo.