KISWAHILI KWA SHULE ZA SEKONDARI (Kidato cha 1 – IV)

Sentensi

Waeleze wanafunzi wachunguze na kujadili sentensi na maswali yanayoambatana nazo kama ifuatavyo:

Sentensi:
Sudan ni nchi kubwa’
Je, neno kubwa katika sentensi hii linafanya kazi gani? Hiki ni kivumishi kinachotia sifa kwenye nomino. Kwa hiyo ni kivumishi cha sifa. Vivumishi vya sifa ndivyo vingi katika matumizi ya kawaida ya kila siku. Maneno kama refu, fupi, chungu, safi, bovu, hodari, nene, nyembamba, nono, yanaingia katika kundi hili.

Sentensi:
Nilimwona nyani mwenye kibiongo
Swali: Yule nyani ana sifa gani?
Kama inavyoonekana nyani ana sifa ya kuwa na kibiongo. Kwa hiyo mwenye kibiongo ni kivumishi kinachotawaliwa na kiangama –enye. Kiangama hicho kinaweza kubadilika kulingana na upatanishi wa kisarufi
wa nomino itakayokuwa inazungumzwa. Kwa hiyo tunaweza kuwa na tungo kama hizi: kiti chenye sifongo

pale penye miti mingi, namba yenye tarakimu
sita. Kivumishi hiki huitwa kivumihi cha –enye.

Sentensi:
Hatukumwona mtu yeyote kule.
Swali: Ni mtu mwenye sifa gani hakuonekana?
Msemaji huyu alitarajia kuonana na mtu mwenye sifa za aina mbalimbali lakini hakumwona hata mtu mmoja. Neno yeyote huarifu zaidi na husisitiza kutokuwapo na katika mazingira husika. Kwa hiyo yeyote ni kivumishi kinachojikita kwenye kiagama –ote. Kiagama hiki nacho hubeba na huweza kubeba maneno kulingana na upatanishi wa kisarufi. Mfano, sikuona ndizi zozote juu ya meza, sina chochote mkononi, kesho sitakwenda kokote;
Niletee meza yoyote. Sina chochote mfukoni. Wewe una jambo lolote la kusema? Una uhuru wa kwenda popote?
Niitie mwanafunzi yeyote aje hapa.

Sentensi:
Wanafunzi watano wa shuleni kwetu waliingia kidato cha tano mwaka jana.
Swali: Neno watano linafanya kazi gani?
Kama kawaida lina arifu zaidi kuhusu nomino wanafunzi. Lakini taarifa hizi zinahusu idadi ya nonimo inakuhusu
idadi ya wanafunzi wanaoingia kidato cha tano. Hiki ni kivumishi cha idadi inayozungumza.

Sentensi:
Msitu wetu uliungua jana.
Swali: Je, neno wetu linafanya kazi gani?
Wakati mwingine neno ni lile lile lakini kazi yake ni tofauti katika sentensi. Angalia tungo hizi.
a) Wale wangu watarudi kesho
b) Wangu wameshinda

Sentensi (a) ina kiwakilishi ‘wale’ kinachovumishwa na kivumishi kimilikishi wangu. Setensi (b) ina kivumishi ‘wangu’
Kwa hiyo neno wangu katika sentensi ya (a) hufanya kazi tofauti na neno hili hilo katika sentensi ya (b). Sentensi:
Mwenye njaa apakue chakula ale. Je, maneno mwenye njaa yanafanya kazi gani? Waeleze wanafunzi wajadiliane
kivikundi kisha waasiliane darasani kwa majadiliano na masahihisho. Viwakilishi hivi hufanya kazi ya badala ya
nomino ambayo ingevumishwa na maelezo ya – enye.

Waongoze wanafunzi watunge sentensi tano zinazotumia viwakilihsi vya –enye. Waongoze wanafunzi wazijadili kwenye vikundi kuhakikisha kuwa ni za viwakilihi na vivumishi hazikuchnganywa. Baada ya hapo ziwasilishwe
darasani kwa kujadiliwa na kusahihishwa.

Sentensi:
Pia watunge sentensi tno zinazotumia viwakilishi vya –enye. Viwakilishi hivi hufanya kazi badala ya nomino
ambayo igevumishwa na maelezo ya –enye. Waongoze wanafunzi watunge sentensi tano zinazotumia viwakilishi vya –enye. Pia watunge sentensi tano zinazotumia vivumishivyya –enye. Waongoze wanafunzi wazijadili kwenye vikundikuhakikiha kuwa ni za viwakilihi na vivumishi havikuchanganywa. Baada ya hapo ziwasilishwe darasani kwa kujadiliwa na kusahihishwa.

Sentensi:
Yeyote katika kundi hilo anaweza kuhuhuria mkutano huo. Waongoze wanafunzi kujadili maswali haya katika vikundi na kuwasiliisha darasani:
1. Eleza tofauti baina ya kivumishi cha oote na kiwakilshi cha oote
2. Tunga sentensi tano zenye viwakilishi vya oote na tano zenye vivumishi vya oote.

Sentensi
Tulimwambia alete za watoto lakini yeye ameleta za watu wazima

Maswali:
1. Je, kiwakilishi cha a unganifu kimeundwaje
2. Je, za watoto wadogo na watu wazima katika sentensi hii zinaweza kuwa nini?
3. Je, maneno hayo yanawakilisha nini? Waongoze wanafunzi wajadili swali katika vikundi.
4. Waongoze wanafunzi wajadili katika vikudi kisha wawasiliane darasani
5. Mtu anaweza kusema, “cha wote kimeletwa mezani.” ‘Cha wote’ husimama badala ya jina la kitu kingine ambacho jina lake lina upatanishi huo wa kisarufi.

Kazi ya kufanya

Sentensi: Mwembamba siye tuliyemchagua

Swali: Je, neno mwembamba linawakilisha nini?

Fikiria maneno kama mrefu, hodari, mchafu, maneno ya aina hii tuliyaeleza katika aya za kivumishi. Maneno hayo yakitumika kueleza nomino basi yanafanya kkazi ya vivumishi vya sifa. Lakini maneo hayo yakisimama badala ya nomino basi yanafaya kazi ya viwakilishi. Kwa hiyo hivi ni viwakilishi vya sifa.

Kazi ya kufanya:

Sentensi: Ishirini wameletwa leo asubuhi
Swali: Je, neno ‘ishirini‘ linawakilisha nini?
Mtu angeweza kusema , Ng’ombe ishirini wameletwa leo asubuhi.
Swali: Je, neno ishirini linawakilisha nini?

Mtu angeweza kusema “Ng’ombe ishirini wameletwa” lakaini kama muktadha unaeleweka, basi anaweza kufupisha maelezo na kasema tu, ishirini wameletwa. Hapa neno ishirini linasimama badala ya ng’ombe. Kwa hiyo hicho ni kiwakilishi cha idadi.
Idadi ya kufanya:

Sentensi: Ambaye amekuja ni mpwa wangu
Swali: Neno ambaye linafanya kazi gani? Neno ambaye limetumika badala ya jina la mtu ambaye ni mpwa wangu. Hiki ni kiwakilishi cha amba. Kiwakilishi hiki kinaweza kuchukua mabadiliko kulingana na ngeli ya nomino husika. Waongoze wanafunzi wabaini viwakilishi katika sentensi zifuatazo:

1. Ambaye ameandika ni mwanangu.
2. Ambalo limeanguka ni lile lililoanguka siku chache zilizopita.
3. Ambalo hulijui litakusumbua mwanangu
4. Ambavyo vilivunjika ni vile vyake.

Mara nyingine viwakiwakilishi hakijitokezi kikiwa huruau kwa kijitegemea (viwakilshi nafsi huru ni kama mimi, sisi, nyinyi, wao). Laiki hudokezwa ndani ya kitenzi katikkatika tungo. Hivi ni viwakilishi nafsi viambata . Kuna viwakilishi nafsi viambata virejeshi. Hivi navyoviko vya aina kuu tatu, viwakilishi nafsi virjeshi ngeli. Hivi vimo kwenye tungo kama hizi:
5. a) Nilijikata jana
b) Wanajidanganya wenyewe
c) Anajidai sana yule
d) Anayeimba ni njiwa.
Herufi zilizokolezwa kwa wino huonesha virejesh katika viwakilishi nafsi ambacho hakijatajwa hapo kwnye tungo. Katika sentensi ‘Nilijikata’, ni hudokeza kiwakilishi nafsi ya kwanza umoja.
Katika sentensi ya pili ji inadokeza kiwakilishi cha nafsi ya tatu (wao) Kwenye sentensi ya tatu,
ji hurejesha kwenye nafsi ya tatu umoja (yeye)

Sentensi ya nne ye inadokeza kiwakilishi cha nafsi ya tatu umoja (yeye).
Kazi ya kufanya
Waongoze wanafunzi watunge sentensi tano zenye viwakilishi nafsi viambata virejeshi mmoja mmoja daftarini mwao.
Viwakilishi nafsi viambata vya ngeli . Hivi huonekana katika mifano hii ya sentensi:
a) Wamerudi makwao
b) Hamtashindwa safari hii
c) Halijui jambo hili.

Herufi zilizoklezwa wino zinadokeza viakilishi
nafsi huru katika tungo hizo kwa mfululizo huu: wao,
niynyi, yeye.
Shughuli
Waongoze wanafunzi watunge sentensi tano zenye
viwakilishi nafsiiviambata vya ngeli mmoja mmoja
daftarini mwao.
Viwakilishi viambata virejeshi ngeli. Hivi hujitokeza
kwnye sentensi kama hizi:
a) Niliowasha hauzimiki.
b) Kinachochimbwa ni kirefu.
c) Nilikokwenda kuna matunda mengi. d) Nilimoingia ni salama kabisa.
Herufi zilizokolezwa wino ni mofumo za urejeshi za viwakilishi vilivyojificha.

Katika sentensi:

a) o huwakilisha nomino ambayo haikitajwa wazi.
Nomino hiyo inakubali upatanishi wa kisarufi husika, nomino hizo ni kama moto, mkaa k. Katika setensi ya
b) –cho– inawakilisha jina la kitu chenye kukubali upatanishi wa kisarufi wa –cho-. Maneno hayo yanaweza kuwa kisima, kichuguu, na mengine ya namna hiyo. c) –ko– huwakilisha mahali mbali na mzugumzaji yaani huko. Maneno haya yanaweza kuwa kule, huko, kwenu nk. katika sentensi d) –mo-huwakiliisha mahali ambapo ni ndani. Maneno haya huweza kuwa ndani, shimoni, chumbani nk.

Kazi ya kufanya:
Waongoze wanafunzi watunge sentensi tano zenye
viwakilishi viambata virejeshivya ngeli daftarini
mwao.Vitenzi (vifupisho vyake ni T, ts, t)
Vitenzi hufanya kazi ya kueleza hali ya kufanyika au
kutofanyika jambo. Hizo hali zavitenzi ukio ndizo
zinazoelezwa kuwa ni vitenzi. Una aina kuu tatu a
vienzi ambazo ni vitenzi vikuu, vitenzi viasidazi na
vitenzi vishirikishi

Kitenzi kikuu: (T)
Shughuli
Waongeze wanafunziwachuguze tug hizi:
1. Umekata mti mkubwa
2. Sikuwa nimekata mti mkbwa
3. Kaka yangu ni mfanyabiashara.
4. Waeleze anafunzi wajadili swali hili kivikundi. Je
neno umekata katika sentensi ya kwanza inafanya
kazi gani?
Tukio pekee linalofanyika katika sentensi hii ni
kukata. Kwa hiyo kitenzi umekata ndicho
kinachotawala sentensi hiyo. Kitenzi kinachofanya
kazi kuu ni katika sentensi huitwa kitenzi kikuu.
Kifupisho chake ni T.
Kitenzi kikuu kinafanya kazi kuu nne katka tungo.
Kwanza hutoa taarifa ya kilichofanyika. Katika
mfano huu taarifa ni kitendo cha kukata. Pili
hudokeza hali ya wakati. Katika mfano huu taarifa
ni wakati uliopitahali tmilifu. Tatu hudokeza hali
ya kauli. Katika mfano huu ni kauli a utendaji. Pia
kitenzi hudokeza nafsi katika hiyo kauli. Katika
mfano huu ni kauli ya utendaji. Pia kitenzi
hudokeza nafsi katika hiyo kauli. Katika mfano huu
ni nafsi ya pili umoja.

Shughuli:
Waekeze wanafunzi watunge watunge sentensi
tano zenye vitenzi vikuu.
Waongoze wanafunzi wajadili swali hili kwa
kubangua bongo:N sikuwa katika sentensi ya pili
hapo juu hufanya kazi gani?
Neno hilo linalisaidia neno nimekata ili kuleta
maana iliyokusudiwa. Katika sentensi hii maana
hiyo imo kwenye ukanushi na wakati uliopita.
Kitenzi cha aina hii huitwa kitenzi kisaidizi.
Kifupisho chake ni ts. Kitenzi kisaidizi hutumika
pamoja na kitenzi kikuu na husaidia kueeza hali
inayozingira kitenzi kikuu. Kwa mfano , nilipokuwa
naye alikuwa anakwenda Itigi.Kitenzi kisaidiza
hapa kinaonesha kuwa katika safari yake ya
kwenda Itigi, palitokea mazingiraya kukutana.
Shughuli:
a) Waongoze wanafnzi wafahamishe dhima za
vitenzi visaidizi vinavyozijenga tungo zifuatazo:
 Wamekuwa wamepitia hapa mara nyingi
 Tuliwahikupata mazao kwa misimu miwili
mfululizo

b) Waongoze wanafunzi watunge sentensi tano
zenye vitenzi visaidizi

c) Waongoze wanafunzi wachunguze sentensi hii
kwa makinimejengewa uhusiano kwa kutumia
ni ma kujibu swali lake.kaka ni mfanyabiashara
d) Neni ni linafanya kazi gani katika sentensi hiyo?
e) Sentensi ‘kaka yangu ni mfanyabiashara’
inaonekana ina ina pande mbili. Upande mmoja
una maneno kakayangu na upande wa pili una
neno mfanyabiashara. Pande hizi mbili
zimejenga uhusiano kwa kutumia neno ni. Neno
ni limechukua nafasi ya neno kama anafanya.
Kwa hiyo sentensi ni ni kitenzi kishirikishi na
kifupisho chake ni t. Vitenzi vishirikishi huweza
kuwa katika ukanushi kwa kutumia neno si. Kwa
hiyo tunaweza kupata sentensi kama : Bwana
Ndorobo si mwalimu. Bi Dalaida si mhandishi.
Shughuli:
Waaongoze wanafunzi wachunguze tungo hizi
na kubaini vitenzi vishirikishi vinavyozijenga.
a) Kijiji chetu ni kizuri
b) Kitojo angali Mkuranga
c) Maneno ni na angali yaliyo katika tungo hizo
ni vitenzi vishirikishi
d) Vitenzi vishirikishi huweza kuwa vikamilifu au
vipungufu

e) Vitenzi vishirikishi huweza kuwa vikamilifu au
vipungufu.
f) Vitenzi vishirikishi vikamilifu hujengwa kwa
maneno kama kuja, kuwa, kwisha yakiwa
yametanguliwa na viambishi va akati, li,me,
na, ta. Kwa mfano
a) Alikuja kunichukua ili twende hotelini.
b) Tumekwisha pika ndizi na nyama
c) Watakuwa wanamsalimua mwalimu wao
d) Vitenzi vishirikishi zaidi ya kimoja
vikitumiwa kwa pamoja hufanya kazi ya
kama vitenzi visaidizi, kwa mfano:
a) Sikupelekwa shule ya bweni kwa sababu
nilikuwa ningali mdogo.
b) Sikuzungumza naye kwa kuwa nilikuwa
nawahi kwenda kupanda basi
c) Utakapokuwa unamwandikia Fares
barua, mtumie na piha hii.
Vitenzi vishirikishi vipungufu hushirikisha
pande mbili za tungo bila uoekana
wakati Dhahiri. Hii ina maana kuwa
tungo ake hazitaonesha waziwazi
maumizi ya alama wakati ambapo ni li,
me, na, ta.

Ifuatayo ni mifano ya tungo zenye vitenzi
vishirikishi vipungufu:
a) Kabunga ni mtunzi wa mashairi
b) Mimi ndimi mwenyekiti
c) Jose yu hodri sana kwenye Sanaa.

Shughuli;
Waongoze wanafunzi watunge zeny

vitenzi vishirikishi vikamilifu
kumi vipungufu.Kila mmoja aandike kwenye
daftari niUlake na hatimusahihisaaaaahaji
kurejesha majibudaraani kwa majadiliano
Kiunganishi (kifupisho chake ni U.
Shughuli;
Waaogoze wanafunzi wajadili maswali hayo
kivikundi kisha wawasiliane darasani kwa
majadiliano na masahihisho:
Neno hili (kiunganisi) linafaya kazi gani
katka lugha?
Je, linatofautianaje na kitenzi kishirikishi?
Shughuli:
Waandikie wanafunzi sentensi hizi ubaoni:
1. Lazima tuoge kabla hatujakwenda
shule.

2. Ametulipa kwa sababu tumefanya kazi
yake vizuri.
3. Umekija kwa usafiri gani?
4. Mtua na Faraja walisafiri hadi Ifakara
mwezi uliopita.
5. Wewe unapenda maembe, mimi
napenda maembe pia.
Wafafanulie kuwa maneno
yaliyokolezwa wino yanafanya kazi ya
kuunganisha dhana mbili za zaidi ziliz
kwenye sentensi. Katika sentensi ya
kwanza. Dhana ya kuoga huunganishwa
na dhana ya kwenda shule. Dhana hizi
zimeunganishwa kwa kuelezwa kua
jambo moja lifanyike kwnza ndipo la pili
lifanyikke. Katika sentensi ya tatudhana
ya kuja au kusafiri inaunganishwa na
dhana . Katika sentensi ya tatu, hana ya
kujau kusafiri inaunganishwa na dhana
ya chombo au mbinu ya kusafiria
inayotumika.

Maneno hayo na mengine yanayofanya kazi kama hizo ni
viunganishi. Kiunganishi ni neno au maneno
yanayotumika kuunganisha mawazo au dhana zadi ya

moja katika sentensi.Viunganishi si lazima vikao katikati
ya sentensi. Vinaweza kukaa popote katika sentensi.
Kinachounganisha ni dhana ya chombo au mbinu ya
kusafiria iliyotumika. Maneno hayo na mengine
yanayofanya kazi kama hizo ni viunganishi. Kiunganishi
ni neno au maneno yanayotumika kuunganisha mawazo au
dhana zaidi ya moja katika sentensi.Viunganishisi lazima
vikae katikati ya dhana au sentensi. Pia vinaweza kukaa popote katika sentensi.
Kinachounganishwa ni dhana auuelewa si maumbo ya
maneno.

Waongoze wanafunzi wafanye zoezi hili kwa
njia ya kubungua bongo.Eleza dhana zilizounganishwa
katika sentensi ya 2 hadi ya tano hapo ju.
Vielezi (Kifupisho chake ni E)
Wape wanafunzi sentensi hizi kwa kuwaandikia ubaoni:
1. Kesho mabondia wataingia ulingoni.
2. Yule mchezaji wa timu ya soka ya wanawake
alifunga mara tatu.
3. Mwivale anawapiga ng’ombe kikatili.
4. Azaria huja kwetu mara kwa mara

Leave a Reply