KISWAHILI KWA SHULE ZA SEKONDARI (Kidato cha 1 – IV)

Vitendawili

VITENDAWILI

Huu ni usemi unaotolewa kwa njia ya fumbo unaoumbwa na pande mbili. Upande mmoja ukiuliza swali na upande wa pili ukijibu swali. Kwa mfano”: ”Popo mbili zavuka mto= macho. Kitendawili hakipigwi wala hakisimuliwi bali hutegwa. Vitendawili hutegwa hivi:

Kutega kitendawili

Mtega kitendawili huanza kwa kusema;

Kitendawili—

Naye msikilizaji huitika

Tega—

Kisha mtegaji kitendawili hukisema kitendawili chenyewe.

  1. Abeba mishale kila aendako= Nungunungu.
  2. Aenda mbio ingawa hana miguu =nyoka
  3. Afahamu sana kuchora lakini hajui achoracho = konokono

4.Amezalia hali, amekufa hali na amerudi hali=Nywele

  1. Anaota moto kwa mgongo=Chungu kiwapo jikoni.

Leave a Reply