kuhusu sisi

Swahili Hub ni mradi uliobuniwa na Kampuni ya Nation Media Group kwa kuanzisha shughuli za kukikuza, kukiendeleza na kukienzi Kiswahili.

Lengo ni kuwa na Kitovu cha Kiswahili kitakachotumika kama chanzo cha taaluma ya Kiswahili na mahali pa marejeo kwa wananchi wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Afrika na duniani kote.

Mradi huu ulianzishwa mwaka 2012 jijini Nairobi nchini Kenya, kwa kutumia Gazeti la Taifa Leo. Kwa upande wa Tanzania Gazeti la Mwananchi linatumika. Awali Mkuu wa Kitengo hiki alikuwa Nairobi- Mkuu wa Ubora (Group Quality Manager, Nation Media Group). Upande wa Tanzania kilikuwa chini ya  Meneja wa Mradi ( Project Manager).

Hata hivyo, baada ya mapendekezo na mabadiliko ya kimfumo, kwa sasa kitengo hiki kipo chini ya Mkuu wa Digitali na Data Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).

Shughuli za utekelezaji Swahili Hub zimehamishiwa nchini Tanzania- MCL na kwa sasa zinaratibiwa na Coordinator wa Swahili Hub.


MAKAO MAKUU

Makao Makuu ya Mradi wa Swahili Hub kwa hivi sasa yako Mwananchi Communications Limited (MCL), Tabata Relini jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, ambayo ni Kampuni tanzu ya Kampuni ya Nation Media Group iliyoko Media Centre, Kimathi Street, Nairobi Kenya.

MADA

Swahili hub inajishughulisha kufundisha Kiswahili kwa wageni na wenyeji pamoja na ukusanyaji wa habari na matukio ya Kiswahili duniani na kuchapisha katika Tovuti na mitandao yake ya kijamii. Pia kukusanya mashairi, tenzi, hadithi, tamthiliya, uchambuzi wa vitabu, n.k kisha kuyachapisha mtandaoni.

MIPANGO YA KAZI

Katika kipindi cha mwaka 2019/2020 Mradi wa Swahili Hub ulioanzishwa na Kampuni ya Nation Media Group utaimarisha ushirikiano na taasisi, asasi, na wadau wa Kiswahili Afrika Mashariki.Pia kutoa mafunzo ya Kiswahili kwa wageni na wenyeji kwa njia ya mtandao.