IJUE HISTORIA KWA UFUPI KUHUSU TAASISI YA AKADEMIA YA AFRIKA YA LUGHA (ACALAN)

Tarehe 9 Desemba 2000 aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Mali, Alpha Oumar Konare alianzisha chombo kwa ajili ya Akademia ya Afrika ya Lugha (MACALAN) kupitia Tamko la Rais N”00.630/PRM.

Kutokana na chombo hicho Akademia ya Lugha  za Kiafrika (ACALAN) ilizaliwa mwezi Januari 2006.

Baada ya kuthibitishwa  katika mkutano wa kawaida wa wakuu wa nchi za serikali wa nchi wananchama wa Umoja wa Afrika kama asasi ya kitaaluma ya Umoja wa Afrika.

Acalan ikapewa jukumu la kuendeleza na kuhimiza matumizi ya lugha za Afrika ili ziweze kutumika katika nyanja zote za maisha katika Afrika sambamba na lugha zilizorithishwa na ukoloni Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kispanishi.

Taasisi hiyo kwa sasa inafanya kazi kwa ukaribu na Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (KAKAMA), huku ikiongoza na Katibu Mtendaji, Dk Lampha Dampha.

Author: Gadi Solomon