maktaba

Mwananchi

Mwananchi

Tangu mwaka 2004 Maktaba ya MCL ilipoanzishwa, mfanyakazi, mtafiti au msomaji wa kawaida anayofursa ya kusoma magazeti haya kwa utaratibu maalumu kutoka kwa mkutubi na pia uongozi wa MCL.

Kwa bahati mzuri gazeti la Mwananchi linachapisha taarifa kuhusu michezo, sanaa, siasa, biashara, teknolojia, ufundi magari, uchumi,burudani kama mavazi na mapambo.

More info →
Mwanaspoti

Mwanaspoti

Hili ni chapisho mahsusi kwa ajili aina mbalimbali za michezo na kwa bahati nzuri liko toleo kwa ajili  wasomaji wa Kenya wanaopenda sana kusoma gazeti ili la Mwanaspoti.

Kwa kuwa michezo ni fani inayopendwa sana na watu wengi wa jinsia zote, wadau wengi wa Kiswahili wanapenda sana kulisoma gazeti hili.

More info →
Taifa Leo

Taifa Leo

Gazeti la Taifa Leo ni gazeti la Kiswahili linalochapwa na The Nation Media Group nchini Kenya. Taifa Leo ni miongoni mwa magazeti mawili ya Kiswahili (Mwananchi na Taifa Leo) ambayo yanatumika katika mradi wa Swahili Hub kusambaza na kukuza Kiswahili Ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na duniani kwa ujumla.

More info →
KISWAHILI KATIKA VYOMBO VYA HABARI NDANI NA NJE YA TANZANIA

KISWAHILI KATIKA VYOMBO VYA HABARI NDANI NA NJE YA TANZANIA

Kitabu hiki kimeandaliwa na  Victor Eliah ambaye ni mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)  upande wa runinga ya TBC1. Kitabu  hicho kimezinduliwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwezi Mei 2019 na kinapatikana sokoni kwa sasa.

More info →
KAMUSI KUU YA KISWAHILI

KAMUSI KUU YA KISWAHILI

Kamusi Kuu ya Kiswahili ilizinduliwa rasmi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  mwezi  Juni 19, 2017 kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma. Kamusi hiyo inapatikana kwenye maktaba yetu pia inauzwa katika maduka ya vitabu.
More info →