MALENGA NAYANGU NANE, NAONGEZA YAWE KUMI

1.Nimekuja ninayangu, imefurika dayari,

Sisemi siri za watu, niko kwenye msitari,

Hapa takumbusha vitu, wala sisemi na kiti,

Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi.

2.Kwani huku sio kwetu, mbona kama utumwani,

Waliobeba mitutu, wanalilia sikonzi,

Jamaa wa bakurutu, amenitoa machozi,

Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi.

3.Ni ya ule mwaka tuu, yasojirudia rudi,

Tutakumbuka mabutu, na ile ya mawe keki,

Ninalikataa gundu, naeleza umakini,

Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi.

4.Hapa roho yangu kwatu, nikiyatoa machozi,

Bora kulilia buku, kuliko shilingi sitini,

Nimeyaona nadubu, yenye sura staili,

Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi.

5.Sasa tano toka matatu, ninasubiria chenji,

Nakwambia sithubutu, kukupa wewe mcheti,

Hata ufunge mayenu, najua unanichiti,

Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi.

6.Hili la sita la babu, nakumbuka ile suti,

Kuna walio na utu, sio walio na miti,

Chuma kimepata kutu, hamna tena cha kiki,

Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi.

7.Yule Bwana wa kishapu, kesharudi kule Lindi,

Arusha mimi ndo kwetu, natokea kikatiti,

Utaja nikuta meru, kama ukija asubuhi,

Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi.

8.Jamanimeona fuvu, sijui kiwili wili,

Kazi yangu kuhutubu, ninaandika mithali,

Haya mazuri si upupu, kama rangi ya kijani,

Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi.

9.Mjomba nakushukuru, uloeleza ni kweli,

Nampa heshima kuku, kuwalisha mabosi,

Akibadilika kunguru, dunia itavaa shati,

Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi.

10.Hii ndo beti ya tunu, tunapenda uswahili,

Alogundua kiduku, kajipaka pilipili,

Muiteni aje huku, aje ale matikiti,

Malenga nayangu nane, naongeza yawe kumi.

Author: Gadi Solomon