BURIANI


1.Kalamu ninaishika, kiwa na tele huzuni
Ya mwisho ninaandika, kisha nitoke dunyani
Si utani nimechoka,kuaga ninatamani
Kwaherini walimwengu,tutaonana peponi

2.Nitungieni shairi, Mwinyimsa aighani
Tungo ziwe na urari,vina vyote viwe ni NI
Mnivushe na bahari, nizikwe Kwale nyumbani
Kwaherini walimwengu, tutaonana peponi.

3.Nizikwe Kiisilamu, nivikwe hata na sanda
Dua nazo ni muhimu, niombeeni kipenda
Sema likuwa Mwalimu, wa hizi tungo kuunda
Kwaherini walimwengu, tutaonana peponi

4.Na chizi wangu Gazila,asikose mazishini
Memwachia zangu hela, zote zilizo benkini
Amjalie Jaala,myaka mingi duniani
Kwaherini walimwengu, tutaonana peponi

5.Ndugu zangu wa Tizedi, Johari nawathamini
Makanyila wangu badi, tutakutana peponi
Hosea nakuahidi, kukukaribisha ndani
Kwaherini walimwengu, tutaonana peponi

6.Mesh yule wa chuoni, riwaya’ngu malizia
Nimeipea Fulani, yakini takutumia
Ichapishe mwezi Juni, na watu wote uzia
Kwaherini walimwengu, tutaonana peponi

7. Saba beti nakomea, nilotaka mewambia
Buriani nawapea, ulimwengu nawachia
Maisha menilemea, kujiua nawazia
Kwaherini walimwengu, tutaonana kuzimu

Utunzi wa Ustadh Emmanuel
Malenga kutoka Akhera
Mzimu mtunga Nudhumu
Mwana Nguva

Author: Gadi Solomon