HERI YA KUZALIWA: RAIS WETU MAGUFULI

Amani Njoka-Swahili Hub

1. Tunafuraha nyoyoni

     Oktoba 29 Jumaini

     Siku hii kwetu Shani

     Kuzaliwa Magufuli

2. Twamshukuru Manani

   Yake kubwa Ihsani

    Kutupa mtu makini

  Rais wetu Magufuli

3. Rais aliye makini

    Muda wote yu kazini

   Atumiki maskini

    Mchana hata usiku

4. Mungu wetu wa mbinguni

    Mwema aso na hiyani

    Ampe heri maishani

   Rais wetu kipenzi

5. Rais huyu shupavu

   Hana chembe uvivu

   Changamoto azisovu

    Tanzania inapaa

6. Kiongozi msikivu

   Mwingi wa unyenyekevu

   Hodari tena mwerevu

   Mipango apangilia

7. Kiongozi mwadilifu

   Moyo wake mkunjufu

   Mambo yake ni sufufu

  Maendeleo mubashara

8. Chuo Huria Tanzania

    Mema kinamtakia

    Furaha mia kwa mia

    Siku yake kuzaliwa

9. Tanzania twajivunia

    Rais Magu aminia

   Nchi aipambania

   Wiz wizi achukia

10. Tunamuomba Jalia

      Azidi kumsimamia

      Umri kumpatia

      Nchi aitumikie

Mtunzi: Dkt. Mohamed Omary Maguo

Mshairi wa Kisasa, Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Author: Gadi Solomon