KONGOLE KWAKO DKT. SOVU WA AHMAD

Ahmad bin Sovu,
Kijana aso uvivu,
jasiri tena shupavu,
PhD kaipakuwa.

Mtu makini sikivu,
mjanja siyo mchovu,
Ameyafuta makovu,
Usomini kuingia.

Amenyaka Uzamivu,
Ya ubichi sasa mbivu,
Kwa udi nayo majivu,
Ndugu yetu jifukize,

Yamenona mashavu,
Na mwili sio mkavu,
Kajaliwa utulivu,
Mpole tena laini.

Ahmad sasa mpevu,
Mpya sio chakavu,
Ameukamata wavu,
Samaki atawavua.

Kijana ni kakamavu,
Imara siyo legevu,
Amejaa nyenyekevu,
Ahmad bin Sovu.

Dkt. Mohamed Omary Maguo,
Mshairi wa Kisasa,
Dodoma.

Author: Gadi Solomon