KORONA


1. KOTE KOTE DUNIANI, VILIO NAVISIKIA,
MAMA HANA TUMAINI, FAMILI IMEPOTEA,
BABA YUKO MASHAKANI, WATOTO WAMEJIFIA,
UGONJWA HUU KORONA, UMEKUJA FANYA NINI?

2. UMEKUJA FANYA NINI? KORONA TWASIKITIA,
WASIWASI JAMIINI, HUU MWISHO WA DUNIA,
VIRUSI KUENEENI, ULIMWENGU WAZIMIA,
UGONJWA HUU KORONA, MUNGU WETU UTURINDE.

3. CHANZO CHAKE UTATANI, KWA WANYAMA HUTWAMBIA,
NA NDEGE HADI NYUMBANI, COVID TUNASIKIA,
NI CHINA HUKO WUHANI, NDIKO ULIKO ANZIA,
UGONJWA HUU KORONA, NI VYEMA TUJIHADHARI,

4. HEWA YA MAJI MBUKIZWA, MIKONO KUSALIMIA,
KUGUSANA UTAJAZWA, MTU KUMKUMBATIA,
KWA SONGAMANO UKUZWA, WENGI UTAWAFIKIA,
UGONJWA HUU KORONA, NI VYEMA TUJIHADHARI.

5. HIZI NI ZAKE DALILI, KIKOHOZI CHAANZIA,
YA MAPAFU HOMA KALI, NA KUSHINDWA KUPUMUA,
TENA MAFUA MAKALI, KICHWA NA UCHOVU PIA,
MAPIGOKO KWENDA MBIO, KORONA TUJIHADHARI.

6. NI VYEMA TUJIHADHARI, BARAKOA KUZIVAA,
MIDOMO PUA SITIRI, UMATI KUOGOPEA,
KUACHA NYINGI SAFARI, WATU KUWASOGELEA,
UGONJWA HUU KORONA, WASIKIZE MATABIBU.

7. MSISHIKANE MIKONO, MJA UKISALIMIA,
UNAWE YAKO MIKONO, SABUNI DAWA TUMIA,
USIPENDE SHIKA USO, VIRUSI TAJA ENEA,
UGONJWA HUU KORONA, NI VYEMA KUJIHADHARI.

8. NI WENGI WAMESHAKUFA, MOLA TUJE MUOMBEA,
AZIZIBE ZAKE NYUFA, HASIRA KUPUNGUZIA,
YASIJE ZIDI MAAFA, MUNGU BABA HURUMIA,
KORONA WATUMALIZA, MWENYEZI UTUSIKIE.

@Elly Wa Ukweli Sauti Ya Watu 2020

Author: Gadi Solomon