Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar:Kuingia kwa ukoloni wa Kiarabu

Na Muhammed S. Khatib (2)

 1. Wa kwanza mtangulizi
  Alojipa uongozi
  Kuanzisha ujambazi
  Kwa jina nawatajiya
 2. Huyo Seyyid Said
  Babaye Ahmedi
  Aliyetoka baidi
  Kuja kututawaliya
 3. Huku kavutiwa na mengi
  Ya faraja na msingi
  Hakuyagundua kwingi
  Ndipo akatufikiya
 4. Kwanza lililomvuta
  Si nchi yenye matata
  Tena haipendi vita
  Ila yapenda umiya
 5. La pili maji matamu
  Yasomwisha mtu hamu
  Na ladha yake timamu
  Meupe ya kuvutiya
 6. La tatu yake bahari
  Imetuliya shuwari
  Vyombo na zake ayari
 7. La nne ni biashara
  Kwetu imetiya fora
  Muhali kula hasara
  Bidhaa kuzifanyiya
 8. La tano ni atashiba
  Kwa ardhi ya rutuba
  Itampa matilaba
  Vipando vitaeneya
 9. Saidi bin Sultani
  Akabaki visiwani
  Pia akaenda Omani
  Tawala kukumbatiya
 10. Numba yake Sultani
  Ilikuwepo Mtoni
  Kila kitu kimo ndani
  Watumishi kwa mamia
 11. Utumwa ukazaliwa
  Watu wakanunuliwa
  Na hata kuadhibiwa
  Shida kuwaelemeya
 12. Wenyeji wakafurushwa
  Mashambani wakalimishwa
  Kwa mateso wakachoshwa
  Wengine wakajifiya
 13. Wakapandishwa minazi
  Kuwa wao ni wakwezi

Hiyo kama yao kazi
Lazima kuabudiya

 1. Karafuu kulimishwa
  Tena kwa kulazimishwa
  Hakuna kuahirishwa
  Lazima kuhudumiya
 2. Upalizi miti hiyo
  Na mengine mengineyo
  Ikafanywa kwa viliyo
  Nyoyo hazikuridhiya
 3. Walokuwa wakaidi
  Kutomtii Saiiadi
  Hawakuipata sudi
  Viboko liwaingiya
 4. Wengine waliuliwa
  Mashimoni kufukiwa
  Sababu wamechukiwa
  Kutumwa kutoridhiya
 5. Kwa hapo hakutosheka
  Bahari pia livuka
  Mrima kujipeleka
  Utumwa kuufatiya
 6. Na ndugu zetu wa bara
  Yaliwafika madhara
  Kama mbuzi wakiporwa
  Bila haki na sheriya
 7. Moja nane ziro saba

Mchana wa saa saba
Mwingereza kaomba toba
Utumwa kuangamiya.

 1. Sheria wakapitisha
  Utumwa kudhoofishha
  Kwani unadhalilisha
  Mtu ukimtendeya
 2. Wabunge wa Kiingereza
  Saidi walimfunza
  Aache kuwachuuza
  Waswahili wa Unguya
 3. Saidi hakusikia
  Kazidi kushikilia
  Yake yapate mwendea
  Faida kujipatiya
 4. Moja nane nne tano
  Yakafikwa mapatano
  Baada ya mzozano
  Saidi na Ingliziya
 5. Saidi akakubali
  Kuiachlia mbali
  Akaridhikwa muhali
  Kuwa hatoendeleya
 6. Utumwa wa siri siri
  Visiwani kunawiri
  Yeye ndiye mshauri
  Na fedha akitumiya
 7. Moja nane tano sita

Jambo kubwa lilipita
Msidhani kuwa vita
Ajali ilitokea

 1. Saidi alikaputi
  Yalimkuta mauti
  Kufika wake wakati
  Saa ilipotimiya
 2. Kama desturi yao
  Mtoto humrithi cheo
  Wa mwanzo mtoto wao
  Majidi akatokeya
 3. Na yeye kafanya yake
  Ya kuwatesa wenzake
  Alimfata babake
  Watu kuwatumiliya
 4. Na yeye akafariki
  Kwa kifo kisicho haki
  Bila kupigwa mkuki
  Ajali ilitimiya
 5. Moja nane saba ziro
  Ikawa kinyang’anyiro
  Ukazuka mgogoro
  Uluwa kupiganiya
 6. Mnada ukapitishwa
  Baraghashi kuapishwa
  Kila mtu kujulishwa
  Kiti atakikaliya
 7. Baraghashi akakaa

Na wala hakuzubaa
Visiwa kuvitwaa
Tawala kukumbatiya

 1. Katika uhai wake
  Naye akafanya yake
  Na tija kumleteya
 2. Alipenda starehe
  Muhali kuzisamehe
  Hazi mwishi starehe
  Ngoma na karamu piya
 3. Naye Bargashi kufa
  Kaja nduguye Khalifa
  Naye kashika wadhifa
  Kiti akakikaliya
 4. Naye hakukaa tuli
  Bila kufanya amali
  Alipitisha thakili
  Mrija akautiya
 5. Alinyonya Unguja
  Kwa kutumia mirija
  Na chumi kuufuja
  Kwa mali kujirithiya
 6. Moja nane tisa ziro
  Kikawa kinyang’anyiro.
  Mwingereza kama hiro
  Nchini akahamiya
 7. Kajitia kwa matao
  Hakutaka mmzubao

Akafanya hapa kwao
Kuifanya mahamiya

 1. Khalifa akafariki
  Ni haki ya makhuluki
  Si kipya kitendo hiki
  Mola kakijaaliya
 2. Ali akajitokeza
  Unguja kuja ifyonza
  Ingawa siye wa kwanza
  Enziwe litaangaliya
 3. Zanzibar katawaliwa
  Watu wawili wakawa,
  Mwingereza twamjuwa
  Na Mwarabu asiliya
 4. Moja nane tisa tatu
  Muda miaka mitatu
  Katawala hapa kwetu
  Hemedi Thuwainiya
 5. Baada ya kifo chake
  Pakatokea makeke
  Yakitaka kiti chake
  Ufalme kuwaniya
 6. Akatokea Khalidi
  Ni kijana mkaidi
  Mfalme kuwaniya
 7. Humudi hakukubali
  Kukosa huo usuli
  Akajiandaa kweli

Kiti kukipiganiya

 1. Saa tatu asubuhi
  Mwingereza kajivuta
  Akayaanza matata
  Tayari akapaniya
 2. Ilimfika taabu
  Khalidi lipojaribu
  Beitili Ajaibu
  Kukaa akajutiya
 3. Alipigwa makombora
  Na kumfika hasara
  Akabaki akizurura
  Hajui pa kuendeya
 4. Na yake mastakimu
  Yakajaa nyingi damu
  Pasiwe aliyedumu
  Roho nyingi kupoteya
 5. Khalid akahiari
  Kuepusha hatari
  Akaenda Dari Salama
  Kwa mtumbwi kukimbiya
 6. Akafika mikononi.
  Mikono ya Jerumani
  Akafadhiliwa ndani
  Mata kuyakimbiya
 7. Humidi kapata kiti

Juu yake akaketi
Kazi kusanya na noti
Mali kujilimbikiya

 1. Kazidisha usuhuba
  Na pia mengi mahaba
  Mwingereza kawa baba
  Pamoja wakiongeya
 2. Uzungu akiupenda
  Na pia akiuganda
  Na Ulaya alikwenda
  Kila mwaka kutembeya
 3. Moja tisa moja moja
  Kwa tena hana haja
  Akakimbia Unguja
  Ulaya akahamiya
 4. Huku harudi tena
  Hakutaka kukuona
  Sababu alizozana
  Na yakeye familiya
 5. Akatawa Khalifa
  Mwenye ndevu za sharafa
  Akazidisha ulofa
  Nchini ukazidiya
 6. Baada ya kutawala
  Akaleta ukabila
  Na kufanya kila hila
  Wanyonge kuwaoneya
 7. Huyu alifanya mambo
  Weusi kufanya chambo
  Yaongoke yake mambo
  Ulowa kumzidiya
 8. Katesa Waafrika
  Kazidisha mashaka
  Kawa kwao patashika
  Dhiki ikawajilia
 9. Aliyahodhi mashamba
  Na kukodisha majumba
  Ilimjaa kasumba
  Ya watu kuwaoneya
 10. Mashamba yakawa yake
  Yeye na aila yake
  Wapate waneemeka
  Mali kuwajaaliya
 11. Mikarafuu minazi
  Iliwapa matumizi
  Si vuli si kiangazi
  Mali iliwajaaliya
 12. Wanyonge kitaka kazi
  Hufanywa ndio wakwezi
  Wanawake vijakazi
  Majumbani kueneya
 13. Alitia ukabila
  Mpaka katika kula
  Asohusu utawala

Hana atojipatiya

 1. Wakipewa kazi ngumu
  Asofanya mwanadamu
  Kwao iliwalazimu
  Viboko kuwalemeya
 2. Alikusanya Wahindi
  Kawaweka kwa makundi
  Kawafundisha ufundi
  Uchumi kuupambiya
 3. Walimiliki viwanja
  Wenyeji wakiwapunja
  Kwa kutumia ujanja
  Ardhi kutawaliya
 4. Wahindi kutoza kodi
  Kubwa isiyo idadi
  Walifanya makusudi
  Utajiri kuwajiya
 5. Kodi za aridhi yote
  Mjini pole popote
  Walisimama kidete
  Wahindi kujikumbuya
 6. Walifungua maduka
  Kuuza kanzu na shuka
  Sufuria na mashoka
  Na zana za kupikiya
 7. Na maduka ya chakula
  Hayakutaka suala

Hayo waliyatawala
Mapato kujikumbiya

 1. Majumba walikodisha
  Kwa njia ya kupangisha
  Na mwezi unapoisha
  ‘Bana kuba’ kakujiya
 2. Wasiolipa malipo
  Marufuku kwa mkopo
  Hufukuzwa hapo hapo
  Japo hana pa kwendeya
 3. Wengine walishtakiwa
  Kwa madeni kudaiwa
  Kortini wakihojiwa
  Kifungoni kuingiya
 4. Wanyonge wengi walifungwa
  Kwa nazaa wakitingwa
  Kesi zikivurugwa vurugwa
  Ili jela kuingiya
 5. Sonara litajirika
  Na mali wakalimbika
  Na matumbo kuwashuka
  Haramu walipapiya
 6. Vilipotea vishamba
  Na hata pia vijumba
  Na viguo kwa mitumba
  Rahani loshadidiya
 7. Na hata hiyo mifugo

Ya wanyama si ya ngogo
Nayo ilipata pigo
Raha nini kupoteye

 1. Watu wakifukarika
  Maafa yakawafika
  Hali zao kudhofika
  Malofa wakabakiya
 2. Mwafrika akabaki
  Hana anachomiliki
  Mnyonge hatamaniki
  Mwepesi anaeleya
 3. Ubaguzi wa elimu
  Hakika ulihitimu
  Hapa kwetu ulidumu
  Nchini kuseleleya
 4. Elimu kibaguliwa
  Mwafrika hakupewa
  Hata kuishuhudiya
 5. Na waliobahatisha
  Chumba cha nane kufika
  Walifika kwa mashaka
  Tena wachache sikiya
 6. Dhamiri ya wakoloni
  Waafrika wawe duni
  Daima wawe gizani
  Wasijue pa kwendeya
 7. Elimu ya sekondari
  Ninakupeni habari

Akiipata tajiri
Na mabwanyenye

 1. Nisemayo ni dhahiri
  Wao walifanywa thori
  Eti kwani mafakiri
  Elimu kujipatiya Unguya
 2. Watoto wa kibepari
  Na wa watu washuhuri
  Haikuwa taksiri
  Elimu kujipatiya
 3. Lipata elimu njema
  Ya kutenda na kusema
  Na kuongeza hekima
  Maisha yawe sawiya
 4. Wanyonge walikoseshwa
  Na wengi walifelishwa
  Hali zao kudhoofishwa
  Ujingani kuingiya
 5. Watoto wa wakulima
  Wakabaki nyuma
  Wamekoseshwa kusoma
  Sipate kuendeleya
 6. Wakapandishwa minazi
  Daima wawe wakwezi
  Watoto waso ujuzi
  Hiyo ndo yao kadhiya.

stephenjmaina@yahoo.com
smaina1tz.nationmedia.com

Author: Gadi Solomon