Matembezi ya hisani kuadhimisha siku ya Kiswahili Duniani

Maadhimisho ya kuelekea siku ya Kiswahili duniani yanaendelea kupamba moto ambapo leo tarehe 4 yanatarajia kufanyika matembezi ya hisani yatakayoanzia viwanja vya Mwembeyanga hadi uwanja wa Uhuru majira ya asubuhi hadi saa saba mchana, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji mkuu Profesa Ibrahimu Juma. Matembezi hayo yataambatana na hotuba pamoja na burudani. Majira ya jioni inatarajiwa kuwa na tamasha la wasanii na Sanaa katika uwanja wa Uhuru.

Ukiwa ni mwendelezo wa kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani tangu ilipoanza tarehe 1 Julai ikiwa ni tamasha la utamaduni na kuzinduliwa rasmi tarehe 2 julai na waziri mkuu Kassimu Majaliwa ambapo. Tamasha hilo lilikuwa ni utekelezaji wa agizo la rais la kutambulisha utamaduni wa Watanzania pale alipokuwa kwenye tamasha la utamaduni Mwanza. Kilele chake itakuwa siku ya Alhamis tarehe 7 Julai mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani.

Author: Gadi Solomon