Majina ya wataalamu wa Kiswahili kusambazwa ofisi za ubalozi

Gadi Solomon, Swahili Hub

Da es Salaam. Kama ulipuuzia kujiorodhesha kwenye kanzidata, hii ni habari njema kwa watalaamu wa lugha ya Kiswahili nchini ambao walitii wito huo. Serikali imesema itayasambaza kwenye ofisi mbalimbali za ubalozi majina yaliyoorodheshwa kwenye kanzidata ya Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita).

Akizungumza hivi karibu wakati akizindua Mpango wa Kutahmini Uwezo wa Wakalimani katika ukumbi wa Bakita, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema tayari kuna wataalamu wa Kiswahili zaidi ya 1,000 ambao Bakita imewatambua kwenye kanzidata yake.

Pia,ameliagiza Baraza hilo lianze kuwaingiza kwenye kanzi data wakalimani ambao watakidhi vigezo kwenye kanzidata ya taifa ili watumike watakapohitajika na ikibidi waendelezwe zaidi.

Alisema suala la kuwapeleka walimu wa Kiswahili kwenye nchi ambazo zimeomba wataalamu linafanyiwa kazi kwa umakini na shughuli hiyo inakwenda vyema.

Alisisitiza kwamba Watanzania watambue kwamba sio rahisi kama watu wengi wanavyodhani kuwapeleka walimu wa kiswahili mara wanapoombwa. Alitolea mfano Afrika Kusini baada ya kutangaza kufundisha Kiswahili kwenye shule zake, wao upande wa serikali wameandaa andiko ikiwa ni hatua ya awali. Pia upande wa Afrika Kusini nao wanalazimika kubadilisha mtaalaa ambao mabadiliko hayo yanaratibiwa kisheria.

Dk Mwakyembe alisema ipo kasumba kwa baadhi ya Watanzania inapotolewa wito wao wanaanza kubeza na kujivutavuta. Mathalan alisema majirani zetu Kenya inakadiriwa tayari imeshaandaa zaidi ya watalaamu wa Kiswahili 40,000 wamejiandikisha kuchangamkia fursa ya kufundisha Kiswahili.

Akizungumzia kuhusu kazi ya kukusanya taarifa kwenye kanzi data, Katibu Mtendaji wa Bakita, alisema shughuli hiyo ni endelevu.

“Tumeweka utaratibu kuwafikia watu mbalimbali katika mikoa yote hapa nchini. Kazi nyingine ambayo inaendelea kwa sasa ni kuwafanyia tathmini wale wote wenye vipaji vya ukalimani kubaini uwezo wao iwe wamesoma taaluma ya ukalimani au hawajasomea.

Author: Gadi Solomon

5 thoughts on “Majina ya wataalamu wa Kiswahili kusambazwa ofisi za ubalozi

 1. Jaman sio tu hao kuna waandishi wengi tu vijana lakin nafasi hawana na hawana hata watu wa kumsupport katika fun yke

 2. Kama ni mchakato endelevu basi ni vema zaidi kufanyika kwa weledi na lengo liwe ni kuinua lugha yetu pendwa na sio watu kufanya kazi kwa maslahi yao wenyewe.Akhsante.

 3. Mimi ni Mwalim wa Kiswahili kwa wageni (Wazungu) mwenye uzoefu wa zaidi ya mika 7 nikiwa chini ya kampuni ya Kiswahili hapa Tanzania lakini pia Kama Mwalimu wa kujitegemea.

  MTAZAMO WANGU JUU YA BAKITA.
  Bakita inafanya vizuri na yawezekana ina malengo ya kupata wataalam wa Kiswahili wazuri na wenye ushindani Japo mfumo unaotumika wa kuwapata hao Walimu Tanzania naona kama umegubikwa usiri na kuna uwezekano mkubwa BAKITA kupata walimu wasio na uzoefu na wenye uwezo wa kawaida kutokana na kuwa watu wanaowapa fursa hizi za kuwafikia Walimu wanaishia kuwafahamisha ndugu,jamaa zao na rafiki.

  USHAURI WANGU KWA BAKITA.
  01.Utengenezwe mfumo wa kujisajili wa
  kieletroniki kama huu,halafu utangazwe
  magazetini na kwenye vyomba vya habari ili
  wenye taaluma hii ya kufundisha Kiswahili
  wapate fursa ya kujisajili kote Tanzania
  nakisha uwepo muda wa wataalamu kwenda
  kuwafanyia usahili kuona namna
  wanavyofundisha kwa kuandaa somo lolote
  kwa ufupi

  02.Kwa uzoefu wangu,Kuna Walimu wa
  Kiswahili cha mfumo wa shuleni
  yaani,Msingi,Sekondari pia vyuo ambao ili
  Anayehitaji kuongea Kiswahili aongee
  itamchukua miaka kadhaa kuweza kuongea
  PIA Kuna Walimu na Taasisi zinazofundisha
  wageni(Wazungu) Kiswahili na kumfanya
  mzungu azungumze kiswahili ndani ya
  kipindi kifupi na Mimi ni miongoni mwa
  walimu hawa.Ningeshauri BAKITA iungane
  na hizi taasisi pamoja na walimu
  wanaofundisha mfumo huu mfupi
  kukieneza kiswahili kwa haraka.Mfano hizi
  taasisi zikipewa Tenda maalum za
  kufundisha nchi zisizojua Kiswahili kwa
  miaka mitano yawezekana asilimia 80% ya
  Nchi hizo wakawa wanazungumza,maana ni
  mfumo rahisi.Waalim
  na Taasisi hizi wanauwezo mkubwa wa
  kuwafundisha watu wa aina zote wanaojua
  kiingeleza na wasiojua kama wachina na
  wajapani.
  03.Ningeshauri BAKITA pia iwatambue Walimu
  binafsi kwa kuwapa namba na Cheti.
  04.Bakita iwe na Mihuli maalum ambayo mwalimu anayetambulika au Taasisi watapaswa kuilipia kwaajili ya kuitumia kwenye vyeti vyao.Mfano Mimi mwenyewe Kama mwalimu vyuo vikuu kadhaa kikiwepo cha Marekani na Uingereza walinipigia na kunipongeza juu ya kufundisha Kiswahili wanafunzi wao na kufikia viwango wanavyovitaka kwa muda mfupi lakini swali lao ni Je ! Nina vyeti vyenye vitambulisho kitaifa ? Hivyo uwepo wenu BAKITA ni wamuhimu Sana lakini pia kututambua waalim binafsi utachochea kasi ya kukieneza Kiswahili Duniani kuliko kutupuuza.
  ASANTE SANA.

Comments are closed.