Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ahimiza kutumia fursa za Kiswahili duniani

Gadi Solomon, Swahili Hub

Ufupisho: Kongamano la Tatu la Kiswahili la Kimataifa Zanzibar limefungwa leo Ijumaa Desemba 19. Kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa “Fursa za Soko la Kiswahili Duniani Katika Maendeleo ya Fasihi na Isimu.” Kongamano hili limehitinishwa kwa washiriki kufanya utalii wa kifasihi kwa kutembelea maeneo yaliyotajwa kwenye kitabu cha Kuli kilichoandikwa na Mwandishi Shafi Adam Shafi.

Zanzibar. Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema serikali itaendelea kuhimiza matumizi ya kugha ya Kiswahili.

Akuzungumza wakati wa  kufunga Kongamano la  Tatu la  Kiswahili la  Kimataifa, Waziri wa  Ofisi ya Makamu wa  Pili wa Rais, Mohamed Abood aliyemwakilisha mgeni rasmi,  alisema kongamano hilo litakuwa chachu ya kutangaza lugha ya Kiswahili kimataifa.

“Kiswahili kimevuka mipaka na sasa imekuwa lugha ya dunia ambayo inatumika kufundishia katika vyuo mbalimbali,” alisema Balozi Idd.

Aliongeza kuwa,Watanzania hawana budi kuendelea kitunza na kuendeleza Kiswahili kwa kuzingumza ili kweze kuenea zaidi na zaidi.

Balozi Idd alisema miongoni mwa mada zilizojadiliwa zimeonyesha fursa mbalimbali za Kiswahili ambazo zikitumika vyema zitasaidia kuongeza pato kiuchumi.

“Fursa za ukalimani, tafsiri na kufundisha Kiswahili kwa wageni ni maeneo ambayo yatawasaidia kukuza uchumi,” alisema Balozi Idd.

Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (Bakiza), Mohamed Seif Khatib alisema licha ya kujadili masuala mbalimbali, pia kongamano hilo limewapa nafasi washiriki kufanya utalii wa kifasihi kuona maeneo mbalimbali ambayo yametajwa kwenye kitabu cha Kuli.

Kongamano hilo limehitimishwa kwa maazimio 10 ambayo yamewasilishwa serikalini.

Author: Amani Njoka