Tamasha la Swahili Society kuwasha moto Marekani

Gadi Solomon, Swahili Hub

Dar es Salaam. Tamasha la Swahili Society linatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi Novemba 2 katika Jimbo la Marryland nchini Marekani. huku likiwakutanisha wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo atakuwa Balozi Liberata Mulamula ambaye  ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Lugha za Kiafrika Chuo Kikuu cha George Washington.

Hivi karibuni Gavana wa Marryland, Larry Hogan aliandika barua kwa Swahili Society USA akisema mojawapo ya majukumu ya lugha ya Kiswahili ni pamoja na kutangaza utamaduni wa Mswahili, pamoja na mila.

Alisema tukio hilo kubwa linatarajiwa kuwa na washiriki takribani 300 pamoja na wengine kutoka mataifa mbalimbali siku ya mjadala, chakula cha jioni, vichekesho na maonyesho ya mavazi ya ubunifu.

Pia, alisema Kiswahili kimekuwa nyenzo muhimu ya kuwaunganisha wanajamii waswahili ambao ni wakazi wa Maryland.

Tamasha la Swahili Society litahusisha mijadala inayohusu kuuenzi utamaduni wa Kiswahili ambayo walengwa watakuwa ni watoto na vijana.

Pia mjadala mwingine utahusu historia ya Kiswahili, hali ya Kiswahili sasa duniani pamoja na matarajio ya hapo baadaye.

Vilevile mjadala mwingine utazungumzia Kiswahili na Sanaa ambapo itaangaziwa jinsi ambavyo wasanii mbalimbali wamekuwa na mchango katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili duniani.

Pia baada ya mijadala hiyo, jioni kutakuwa na chakula cha jioni sambamba na maonyesho mbalimbali ya kiutamaduni.

Author: Gadi Solomon

2 thoughts on “Tamasha la Swahili Society kuwasha moto Marekani

  1. I would really love to explore this site as I carry out reading and doing resaech on the courses I pursue

Comments are closed.