Waaswa kujifunza lugha zaidi ya Kiswahili na Kiingereza

Mwandishi, Mwanaspoti

Kifupi: “Mwandishi anayefahamu lugha zaidi anayefahamu lugha nyingi anaweza kufanya katika mazingira mazuri zaidi kwa nafasi na kujiamini.” Usher.

Dar es Salaam. Licha ya maswala ya kimichezo, waandishi wa Wanawake wa habari za michezo wametakiwa kuongeza maarifa na ujuzi wa lugha ngingi ili kurahisisha kazi zao za kiandishi. Pia, kutawafanya wawe na weledi na upekee katika kufanya kazi zao.

Hayo ni miongoni mwa maneno yaliyozungumzwa na Mkufunzi wa semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Usher Kamugisha alipokuwa akizungumza kwa washiriki wa semina hiyo ilifamyika jijini Dar es Salaam.

Suala la utamaduni wa kujisomea vitabu pia liliibuka kama msisitizo kwa waandishi hao kuongeza maarifa na ujifunzaji wa lugha zingine zaidi ya Kiswahili na Kiingereza. “Unaweza kujua lgha moja au mbli, mfano Kiswahili na Kiingereza lakini Afrika Magharibi wanajua Kifaransa, hivyo lazima ujifunze lugha tofauti.”Aiongeza. Pia, suala la kujisomea vitabu halikubaki nyuma kwa kusisitiza kuwa vitabu vinaweza kumsaidia mtu kujifunza vitu vingi ambavyo vitamuongezea ubora katika kazi zake.

Usher ambaye anafanya kazi na taasisi za Supersport, FIBA na BBC alisema “Hata suala la lugha, kitabu kinaweza kuwa msaada mkubwa kwako. Kuangalia YouTube lakini kwa ajili ya kujifunza na vitu mbalimba.”

Semina hiyo ya Waandishi wa wanawake wa habari za michezo imefanyika kwa siku jijini Dar es Salaam na kumalizika jana, Alhamisi na kufungwa Makamu wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani ilihudhuriwa na washiriki wapatao 27 kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Author: Gadi Solomon

2 thoughts on “Waaswa kujifunza lugha zaidi ya Kiswahili na Kiingereza

Comments are closed.