Mbunge Maige ashangaa kukipuuza Kiswahili

KWA UFUPI

Mbunge Athuman Maige ameshangazwa na kasumba ya kuendelea kutumia lugha ya Kiingereza huku msingi wa watoto hao ukiwa ni lugha ya Kiswahili kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.

Mbunge huyo ambaye amekuwa akipigia Kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishiam amewahi kuwasilisha hoja binafsi akilitaka Bunge kuridhia lugha ya Kiswahili kutumika katika nyanja zote za elimu.

“Duniani kote hakuna nchi iliyoendelea kwa kutumia lugha ya watu wengine, Uingereza wanatumia kiingereza, Wachina kichina, lakini Tanzania tunatumia lugha ya kufundishia ni Kiingereza, watoto wanasoma Kiswahili darasa la kwanza hadi la 7,”- Athuman Maige

Kauli ya Maige inaungwa na watalaamu mbalimbali wa Kiswahili ambapo miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa ni kuchagua shule za mfano ili kuanza kutumia Kiswahili kwa masomo yote, iwe sekondari au chuo kikuu.

Author: Gadi Solomon