Meno ya mbwa hayaumani

Na Pelagia Daniel

Amani haiji ila kwa ncha ya upanga

Ukitaka Amani sharti uwe tayari kwa vita. Ikitokea mtu anataka vita au utesi (ugomvi) na wewe atafikiri mara mbili kabla ya kuendelea. Methali hii inatufundisha kwamba, tukitaka tusionewe au tusidhulumiwe, lazima tuwe tayari kujitetea. Hapo ndipo tutakapookoka.

Hasira hasara

Hasira si jambo zuri mara nyingi huleta hasara tu. Methali hii hutumiwa kuonya watu wasiwe na hasira kwa sababu zinaweza kusababisha hasara ya vitu au uhai wa watu.

Meno ya mbwa hayaumani

Meno ya mbwa yameumbwa kwa namna ambayo, akifumba mdomo wake, hayaumani kama yanavyoumana yetu sisi binadamu. Methali hii hutumiwa kuonyesha kuwa ndugu, jamaa au watu wanaoishi kwa umoja, hata wakigombana huweka mabo sawa na kurudi kama kawaida tu.

Author: Gadi Solomon