Methali

Na Pelagia Daniel

  1. Jina jema hungara gizani. Kuna wakati mtu anaweza kuchafuliwa kwa mambo ambayo hajayafanya lakini ukweli siku zote hujitenga na uongo hivyo jina lake litang’aa hata katika sehemu ya gizani.
  2. Mjumbe hauawi. Mpeleka taarifa hufikisha taarifa kama alivyoambiwa na mtoa taarifa hivyo kama taarifa ni mbaya wa kulaumiwa ni mtoa taarifa.
  3. Mpofuka ukongweni, hapotewi na njia. Mtu anayepata matatizo ya macho na kushindwa kuona katika kipindi cha uzee hawezi kusahau njia kwa sababu anakuwa ameshazizoea hata kwa kukisia. Hii ni sawa na mtu mzima anayezizoea kazi au tiba hata akizeeka anaweza kuendelea kufanya shughuli zake.

Author: Gadi Solomon