Methali

Na Pelagia Daniel

  1. Ukenda kwa wenye chongo, fumba lako jicho. Methali hii ina maana ya pale unapokutana na watu wajuaji katika mambo ambayo hayako sahihi bora na wewe uungane nao kwa sababu ukitaka kuwakosoa hawatakubaliana na wewe.

2. Ukupigao ndio ukufunzao. Mambo yote yanayokufanya uumie na wakati mwingine kukata tamaa ndio mambo ambayo yatakufunza.

3. Watu wanahesabu nazi, wewe unahesabu makoroma. Methali hii ina maana pale ambapo watu wanahangaika kutafuta mafanikio watu wengine wanakuwa wanahesabu mambo maovu.

Author: Gadi Solomon