Methali ya ‘Ukitaka salama ya dunia, zuia ulimi wako’ imejaa mafunzo

1. Ukienda kwa wenye chongo, fumba lako jicho.
2. Ukimpa shubiri huchukua pima.
3. Ukimuiga tembo kunya, utapasuka msamba.
4. Ukimwamsha aliye lala utalala wewe.
5. Ukinyofoa mnofu, ukumbuke kuguguna mfupa.
6. Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.
7. Ukiona moshi, chini kuna moto.
8. Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
9. Ukiona vinaelea, vimeundwa.
10. Ukiona zinduna, na ambari iko nyuma.
11. Ukistahi mke ndugu, huzai naye.
12. Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
553. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliye nona.
14. Ukitaka salama ya dunia, zuia ulimi wako.
15. Ukiujua wa mbele, nina ujua wa nyuma.
16. Ukupigao ndiyo ukufunzao.
557. Ukuukuu wa kamba siyo upya wa ukambaa.
18. Ulimi hauna mfupa.
19. Ulimi unauma kuliko meno.
20. Ulipendalo hupati, hupata ujaaliwalo.
21. Ulivyoligema, utalinywa.
22. Umeadimika kama la jogoo.
23. Umegeuka mung’unye waharibika ukubwani.
24. Umejigeuza pweza, unajipalia makaa?
25. Umekuwa bata akili kwa watoto?
26. Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
27. Umeruka mkojo unakanyaga mavi.
28. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
29. Unajenga kwa mwenzio na kwako kunaporomoka!
30. Unakuja juu kama moto wa kifuu.
31. Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
32. Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.
33. Ushikwapo shikamana (Ukibebwa usijiachie).
34. Pema ukipema usipopema si pema tena
35. Usiache mbachao kwa msala upitao.
36. Usiache tawi kabla ya kushika tawi.
37. Usiandikie mate na wino ungalipo
38. Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
39. Usijifanye kuku mweupe.
40. Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno
41. Usile na kipofu ukamgusa mkono.
42. Usimgombe mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
43. Usiniache njia panda.
44. Usinikumbushe kilio matangani.
45. Usinipake mafuta kwa mgongo wa chupa.
46. Usinivishe kilemba cha ukoka.
47. Usione simba kapigwa na mvua.
48. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
49. Usisafirie nyota ya mwenzio.
50. Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
51. Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu.
52. Usitukane wagema na ulevi ungalipo.
53. Usitukane wakunga na uzazi ‘ungalipo.
54. Utakosa mtoto na maji ya moto.
55. Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.
56. Utaula na chua kwa uvivu wa kuchagua.
57. Vita havina macho.
58. Vita si lele mama.
59. Vita vya panzi, neema ya kunguru
60. Waarabu wa pemba, hujuana kwa vilemba
61. Wache waseme.
62. Wafadhilaka wapundaka.
63. Wagombanao ndio wapatanao.
64. Watu wanahisabu nazi, wewe unahisabu makoroma.
65. Mafahari wawili wapiganapo nyasi ndizo huumia.
66. Watetea ndizi, mgomba si wao.
67. Wazuri haweshi.
68. Wema hauozi.
69. Wengi wape.
70. Mungu si Athumani

Author: Gadi Solomon