METHALI ZA KIAFRIKA ZILIZOJAA MAFUNZO NYUMA YAKE

1. Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
2. Mpofuka uzeeni, hapotewi na njia.
3. Msafiri kafiri.
4. Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
5. Msasi haogopi mwiba.
6. Msema kweli hukimbiwa na rafiki zake.
7. Msema pweke hakosi.
8. Mshika kisu, hashiki makalini.
9. Mshale kwenda msituni haukupotea.
10. Mshoni hachagui nguo.
11. Msi bahati, habahatishi.
12. Msi mbele, hana nyuma.
13. Msishukuru mja, hamshukuru Molawe.
14. Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu.
15. Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
16. Mvumilivu hula mbivu.
17. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
18. Mtaka lake hasindwi.
19. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
20. Mtaka unda haneni.

Author: Gadi Solomon