
JINA LA MTUNZI: Shung Thong Xhi
Mawasiliano: 0623410370, 0693548469
INSTAGRAM: @Shungthong
UTANGULIZI: Wiki iliyopita tulianza sehemu ya kwanza ya hadithi tamu ya Mfalme Izana, sasa endelea…....
“Nimekuja kuonana na kiongozi mkuu wa mila…!?”
Wale vijana walio kuwa nje pale waliinamisha nyuso zao wakati Mizana anaongea kuonyesha heshima!.
“Karibu mtukufu Mizana!…”
“Asante……!”
“Hivi unavyo tuona tayari tumesha jiandaa kujongea kwenda huko kwenye mlima wa miungu yetu kwenda kuomba shauri! Hivyo nakuomba wala usijali mtukufu Mizana kila jambo lita kwenda sawa!”
Aliongea hivyo ili kumtuliza Mizana kisha akainama kuonyesha heshima kabla hajaondoka mbele ya uoni wa Mizana pamoja na msafara wake.Mizana aliwageukia watumishiwake wawili wakike kisha akawageukia askari kadhaa ambao alikua ame ongozana nao, na kuwaambia tuna wafuata hawa! Waliinamisha vichwa vyao wakiwa na maana ya utii! Japo ilikuwa ni kosa kubwa sana kwenda kwenye mlima wa miungu uitwao Mizio, watu wote walio fanya au waliojaribu kusogea eneo lile hawa kufanikiwa kurudi! Imepita miaka mingi mpaka leo hakuna anaye weza kueleza nini kilikuwa kinatokea japo tafiti kazaa zimesha fanywa!. Mpaka leo hakuna anaye weza kueleza kwa usahihi kwasababu vilikuwa ni vitu vya ajabu sana!.
Walianza safari kuelekea huko wakiwa na hofu kuu! Ili kuwa ni baada ya kuanza kupita kwenye miti minene na mikubwa ya msituni walihisi hali ya hewa ime badilika ghafla! Mizana baada ya kuliona hilo wakiwa kilimni,aliwageukia askari wake pamoja na watumishi wake na kuwauliza,
“Mpotayari kufa kwaajili ya Mizana!…?”
“Tupotayari kumtumikia! Kufa kwaajili ya Mizana!”
“Mpotayari kufa kwaajili ya Izana…!”
“Tupotayari kumtumikia! Kufa kwa ajili yake…!”
Walijibu kwa pamoja vichwa vyao vikiwa chini!,Mizana aliwaangalia na kuinua kinywa chake kisha akasema,
“Mna mkiri kuwa Izana ndiye atakuwa Maya wenu…….!”
Walitulia kimya bila ya kujibu! Na kumfanya arudie kwa kusema
“Mna mkiri kuwa Izana ndiye atakaye kuwa Maya wenu…!?”
“Ndio tuna mkiri Izana mtukufu kuwa ndiye Maya wetu…!”
Sentensi hiyo ilimfanya mwana mama huyu atabasamu kwa mbali na kuwa nyooshea fimbo yake wale watumishi wawili wakike ambao ni Ipraya ambaye ndiye mkubwa pamoja na Iaya ambaye ndiye mdogo kisha akamnyooshea fimbo askari ambaye ndiye aliye kuwa na umri mdogo zaidi kuliko wale wenzake kisha akasema;
“Nawaombeni mrudi mkamwangalie Maya wenu na kumuudumia!”
Walibaki wakitazamana wasijue cha kusema ndipo yule askari kijana aitwaye Eona akasema;
“Tumesha kula kiapo kuwa tuta kulinda iweje leo tukuache……!”
Aliuliza kwa unyenye kevu sana huku moyo wake ukimuenda mbio kwasababu kwa taratibu zao zilizo kuwepo ilikuwa hairuhusiwi kuhoji kauli ya mkubwa wako! Kufanya hivyo ulikuwa unastaili adhabu ya kifo!.Nawale wafanyakazi wakike pia waka sema;
“Eeeee……..Mtukufu Mizana tunakuomba usitufanye tukukosee! Hatuwezi kamwe kuondoka na kukuacha mwenyewe!”
Mizana akawasogelea karibu na kuwa tazama kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema;
“Mposahihi………!”
Kisha akawaamuru askari walio kuwa wamewashikilia tayari kwa kosa la utomvu wa nizamu;
“Waacheni…”
Kishaakavua pete ambayo ipo kidoleni mwake na kuikabidhi kwa Ipraya yule mtumishi wa kike mkumbwa na kusema;
“Nawaombeni……!”
Kabla hajamalizia sentensi yake waliinama chini na kusema;
“Uparikiwe eeeee…..mtukufu Mizana….!”
Kisha kwa huzuni walianza kugeuka na kuondoka wakiwa na huzuni! Hawakuweza kuya zuiya machozi! Kwani walijua Mizana kwenda kule hatoweza kurudi! Mizana naye hakuweza kujizuiya machozi alijikuta tu analia! Moyo wake ulimuuma lakini alikuwa anajua kuwa hana njia nyingine ya kufanya zaidi ya kujihatarisha maisha yake! Baada ya kuona kuwa walikuwa wamesha potelea kabisa kwenye poromoko aliwageukia wale watumishi wengine pamoja na askari na kuwaambia…”
“Duweeeeeeeee…!
Kimizi hicho akiwa na maana ya tuondokeeeeeeeeeeeeee!.Ipraya pamoja na wenzake wakiwa wanashuka kuelekea kwenye mji ama ngome yao iliyo kuwa inaitwa “MIZI-ORO” wakiwa na maana ya ardhi iliyo barikiwa! Waliweza kuona wingu zito lenye rangi ya moto likitanda ghafla kwa upande ambao Mizana alikuwepo na ulitokea muwako wa kutisha wa moto! Sauti za vilio na kusaga meno zilisikika na kunyamaza ghafla!.Ardhi ilitetemeka mpaka kwenye mji wa Mizi-Oro! Mpaka kwenye ngome za wajerumani!.
“Ni kitu gani hichi…!?”
Wajerumani walijiuliza,tetemeko lilikuwa kubwa sana na lilisababisha uharibifu wa majengo pamoja na mali nyingine!.Kwa upande wao Ipraya pamoja na wenzake waliangua kilio baada ya kusikia na kuona hivyo walijua tayari habari ya Mizana ilikuwa imeishia hapo! Hakuna aliye kuwa anajua nini kinachoenda kutokea kwenye jamii hiyo iliyo kuwa na nguvu sana Afrika mwishoni mwa miaka ya 1800s.
****************…………..*****************************…………….********************
Ilikuwa ni siku yenye pilika pilika sana ndani ya ofisi za Cansela Von Soden, pilika pilika hizo zililetwa na maandalizi kwa ajili ya kumpokea mkuu wa majeshi mpya baada ya yule wa zamani kufutwa vyeo!.
“Mmmmm………………………………h”
Jenny bado alikuwa na maswali ndani ya kichwa chake juu ya tukio la siku iliyo kuwa imepita nyuma,alijiuliza mbona leo amekuwa mchangamfu kupita kiasi…..!?”
Wakati anayawaza hayo alistuliwa na sauti ya Akliye kuwa anamuwaza ikimwambia;
“Ebu nenda kaandae mafaili na uyapeleke kwenye ile meza mahali pale….”
Wakati jeni anaondoka kwenda kutekeleza agizo Cansela akamuita na kumwambia;
“Umesha pata chai…!?”
Swali ambalo hakuwa amelitegemea! Kwa hali ilivyo kuwa huenda Cansela aliuliza hivyo sio kwa sababu labda alikuwa anamjali sana Jenny bali huenda aliuliza hivyo kwa sababu alikuwa na furaa sana siku ya hiyo!.
“Aaaaaaaaaaaa………………………….aah”
Hakujua hata ajibu nini! Alikuwa ameduwaa tu! Bila ya kusema jambo lolote!
“Basi tutapata chai pamoja leo…………!”
“Aaaaaaaaaaaa…………..h….”
Alijitaidi kuficha shauku yake na kusema akitoa tabasamu hafifu!
“Asante nitafurahi!”
Alisema nakumfanya Cansela atabasamu pia.Baada ya muda sio mrefu sauti za matarumbeta zililia wakati gari kadhaa zilizo kuwa zina kuja kwa kasi zikionekana kwa mbali,zilipo funga breki zilitimua vumbi kiasi kwamba hata usingeweza kumuona jirani yako aliye kuwa amesimama karibu yako zaidi!.
“Khooooooo……………….ooooooo…………..ooooooooooooooooooh”
Sauti za watu wakikohoa ndizo zilizo sikika! Baada ya sekunde chache vumbi lilipungua na mlango wa gari uli funguliwa na anaonekana mtu mwenye urefu wa kutosha akiwa amekatia nywele zake vyema na kuzichana kiumaridadi kwa kwenda nyuma. Alitembea juu ya kitambaa maalumu na kusimama eneo lililokuwa lime andaliwa, wimbo wa taifa la ujerumani uliimbwa na kufuatiwa na makofi ya nguvu! Na vifijo.
“Cansela Von Soden huyu ndiye ambaye tulikutambulisha kupitia barua kuwa atakuja kufanya kazi pamoja na wewe kama mkuu wa majeshi, anaitwa mr Otto!”
“Ok karibu sana nimefurai kukuona nimefurai pia!”
Wakati hayo yanaendelea Jenny alijiuliza;
“Kama ile barua ilikuwa ina muhusu huyu Otto sasa nini kilimstuaaa……!?”
Wawili hawa walikuwa wanafahamiana vyema ingawa wakati wanatambulishwa kila mmoja alijifanya hamjui mwenzaake! Baada ya hayo walijongea wote kwenye meza na kuanza kupata chai kwa pamoja,Jenny naye alikuwa pale kwenye meza ya heshima akipata chai pamoja na mabosi zake! Alijisikia raha sana!.
“Huyu ni nani ndio mke wako ……..!?”
Swali ambalo lilimboa sana Cansela na kuhisi jamaa alikuwa anamziaki! Kwani alikuwa anamjua mke wake vizuri kabisa! Lakini alijikaza na kusema;
“Aaaaaaaaaa……………hapana huyuuu………………!”
Jenny alikuwa antamani kama atambulishwe kuwa yeyendiye aliye kuwa mke wa Cansela ingawa hakuwa na uhakiaka sana na jambo hilo!.
“Huyu ni sekretari wangu….!”
Alisema japo kwa kujilazimisha! Lakini haliyake ilibadilika baada ya swali hilo na alijua kuwa lazima linge fwata swalilingine la namna hiyo hiyo! Wakati anawaza hivyo alisikia swali ambalo alikuwa anajua huenda lingeulizwa tu!
“Shemeji yangu yupo wapi….!”
“Leo hayupo sawa hivyo ndio mana hajaweza kufika mahali hapa siku ya leo….!”
Akainuka na kusema;
“Naomba tunywe tufurahi baada ya kumpata mkuu huyu wa majeshi aliye tukukaaaa…..”
Sauti za shangwe zilisikika na kumfanya Otto aachie meno yote njenje kama mwendawazimu anaye tawanya mienge! Cansela baada ya kusema hivyo aliomba udhuru na kujongea nyumbani kwake! Akiwaacha watu wakisheherekea.Jenny tayari alikuwa ameshagundua jambo wakati ule miamba hii miwili ilipokuwa insemeshana! Akiwa anawaza hayo yule mkuu wa majeshi mpya ama unaweza kumuita Otto alimshika mkono binti huyu mrembo na kumuomba ampekeke maliwato.
“Usijali…..”
Akamsaidia kuinuka kwa maana alikuwa amesha lewa tayari!.Kuchaguliwa kwa Otto kama kiongozi wa jeshi kuliwashitua wengi kwa sababu mtu huyu alikuwa amehusika kwenye uvunjaji wa sharia kama unyanyasaji wa kijinsia pamoja na silaha haramu lakini bado alikuwa amepewa cheo cha kutukuka na kuwaacha walio kuwa wanastaili waendelee kusota na kutumikishwa siku zote!
Walipofika maliwatoni Otto alimuomba binti amsaidie kufungua maji ya bomba! Wakati binti anafanya hivyo,Otto aliishika sketi ya binti na kuishusha! Jenny alistuka na kutaka kupiga kelele lakini huyu jamaa alitoa bastola na kumwambia kama ange fanya hivyo basi ange mmwaga ubongo wake!.Bila ya huruma alimtazama binti na kumwa mbia kwa sauti yake ya kukoroma;
“Naomba utoe mwenyewe nguo moja baada ya nyingine…! “
Binti machozi yalimbubujika! Alihisi kama anaota hivi! Alitamani tukio hilo liwe ndoto! Alijaribu hata kumuomba msamaha ili asimtende hivyo lakini Otto alisisitiza avue nguo! Baada ya kutoa nguo tu zilisikika sauti za viatu zikiingia kwenye kodroo ya choo na kusikika sauti ya mtu akifungua mlango wa choo chapili! Otto alimsogelea binti karibu na kumuwekea bastola kichwani huku akimnong’oneza,
“Olewako upige kelele!…..”
Baada ya yule mtu aliye kuwa ameingia kujisaidia kuondoka! Inasikitisha kuwa Jenny alifanyiwa unyama wa kubakwa tena kinyume na utaratibu!.
*****************………………********************…………………**********************
“Izana………..Izana…………………..!?”
Ipraya aliita kana kwamba alikuwa amechanganyikiwa!
“Yupo chumbani kwake amelala…………..”
Mtumishi mmoja alimjibu na kumfanya ahememe ,
“Huuuuuuuuuuuuuuuuuu………………………………uuuuuuuuuuuuuuuuuuh”
Mana alikuwa na wasiwasi,alijongea kwa haraka mpaka chumbani kwa binti huyo mdogo.Alijiegemeza pembeni ya kitanda cha Izana na machozi yalianza kumtoka kimya kimya!aliwaza;
“Mtoto huyu hana baba wala mama nabado ni mdogo! Sasahivi ni kama hatuna kiongozi kabisa kwa sababu Mizana naye amesha poteza uhai! Hakuna anaye jua hili! Vipi ikijulikana wapinzani wata pata nguvu sana! Nita mwambia nini Izana atakapo niuliza kuhusiana na mama yake!!?
Yalikuwa ni maswali juu ya maswali yasio na majibu ndani yake! Alimgeukia Iaya ambaye ni mtumishi mdogo na kisha akamtazama Eona yule askari kijana aliye kuwa amejiegemeza kwenye kona ya mlango na kisha akasema;
“Hakuna anaye jua kama Mizana hayupo tena! Na mambo bado ni magumu sana hivyo nawaombeni hii ibaki kuwa siri mpaka hapo mambo haya yatakapo tulia!…..”
Waliweza kuitikia kwa kutingisha vichwa tu! Wakionyesha ukubali! Wakati hilo linaendelea chakula kilikuwa kina letwa upande wa chumba cha Izana,Eona alimzuiya yule mtu na kukichukua chakula kile mikononi mwake! Ipraya alikichukua chakula kile na kukimwaga! Iaya pamoja na Eona walibaki wana shangaa kuwa Ipraya alikuwa anafanya jambo gani!.
“Huu sio wakati wa kumuamini mtu yeyote yule! Lazima tuwe makini sana kwani adui sasa anamuwinda huyu mtoto!”
***************…………………*******************…………………….********************
“Aaaaaaaa……………………aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah!”
Cansela Von Soden alistuka kidogo baada ya kupita kwa haraka na kumsalimia sekretari wake lakini hakuwa amesikia majibu yoyote yale hivyo alirudi taratibu na kutupia macho kwa umakini kuelekea ofisi ya Jenny.Aligundua kuwa hakuwa amefika mahali pale ama unaweza kusema hakuwepo! Aliwauliza wafanyakazi wengine kama walikuwa wame muona,lakini kila mmoja alimwambia kuwa hakuwa amefika.
“Lakini hii sio kawaida yake huyu! “
Alijua huenda kutakuwa na tatizo!
“Atakuwa anaumwa ama! Lakini mbona haja toa taarifa zozote zile….!?”
Alijiachia maswali ambayo hakuwa na majibu nayo hata kidogo,aliamua kupotezea na kuamua kuingia ofisini kwake moja kwa moja,muda ulipita na alitoka nje kidogo kuchukua kahawa lakini hakumuona Jenny!.Alipo tazama saa yake aligundua kuwa tayari ilikuwa imesha fika saa nne asubuhi! Hapo nafsi yake ikaanza kupata mashaka ya wazi.Aliamua kujongea moja kwa moja hadi kwenye gari yake na kuanza safari ya kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Jenny.Alipo fika aliita lakini kulikuwa kimya sana hivyo aliamua kusukuma geti kwa nguvu! Akiita;
“Hellooooo……………………….ooooooooooooooooooooooooooooooooooow!”
Alijitokeza kijana ambaye alikuwa amevalia nguo zilizo muonyesha kuwa alikuwa ni mlinzi,yule kijana alisema kwa heshima;
“Karibu baada ya kumuona Cansela mahali pale….”
“Nina muulizia Jenny,nimemkuta…..!?”
Akaacha kama swali kwa kijana, yule kijana akasema;
“Hapana yupo hospitali…”
“Hospitali……”
Akaitikia kwa mshangao sana kana kwamba alikuwa hana uhakika na alichokuwa amekisikia!;
“Ndio hospitali…….”
“Ok! Sawa nashukuru…”
Akarudi ndani ya gari akitafakari kuwa inaweze kana vipi wakati jana alimuacha Jenny akiwa ni mzima wa afya! Bila kupoteza muda aliamua kuwasha gari kuelekea hospitali ambayo Jenny alikuwa amelazwa.Watu walistuka walipo muona Cansela mahali pale hospitali akiwa amekuja kama mtu wa kawaida hana msafara! Hana walinzi! Alipita moja kwa moja hadi kwa dokta wa pale ambaye alikuwa ni mwanamke na kumuuliza kuhusu Jenny.
“Ndio tuna mgonjwa kama huyo alikuja tangujana na hali yake haikuwa nzuri! Alikuwa kama hajielewi lakini kwa sasa yupo vizuri!”
“Naweza kumuona…”
“Hapana tumempumzisha kwanza! Lakini usijali tuta mruhusu jioni,na anatakiwa awepo mtu wa karibu wa kumuangalia mpaka afya yake itakapo boreka!”
************
Cansela alipewa chumba maalumu kwaajili ya kumsubiria mgonjwa wake,Jenny alipo fumbua macho alishangaa kumuona Cansela yupo mahali pale akiwa na tabasam pana pamoja na kishada cha maua mikononi mwake!Jenny machozi yalimtoka jambo ambalo lilimstua Cansela Von Soden sana!.Wakiwa njiani ndani ya gari walikuwa kimya tu mda wote, baada ya kushuka kwenye gari Cansela Von Soden aliweza tu kumwambia;
“pole sana Jenny….”
Lakini alivyogeuka na kutaka kuondoka aliya kumbuka maneno ya daktari kuwa amwangalie kwa ukaribu,alirudi mpaka ndani na kumuuliza Jenny kama alikuwa na chakula ambacho kilikuwa tayari kimesha andaliwa.
“Usijali…..!”
“Najali….”
Jenny hakuamini alipo muona bosi wake akiingia jikoni kwaajili yake! Ni sawasawa umuone Rais wako anaingia jikoni! Hiyo ingekupa raha sana eh! Lakini hiyo haikuwa hivyo kwa Jenny.Kila alipo kumbuka kitendo alicho tendewa na Otto moyo wake ulimuuma sana! Hakuwa na furaha hata kidogo!,baada ya muda mfupi tayari Cansela Von Soden alikuwa tayari amesha muivishia chakula chenye asili ya kijerumani mrembo Jenny.
“Karibu chakula……”
Alimkaribisha na yeye aka kaa na kuanza kula huku akimsihi kuwa ajitaidi kula,Jeni alipopiga kijiko na kukiweka mdomoni mwake alishangaa kuona jinsi bosi wake alivyo kuwa amekipika chakula kile! Kilikuwa na ladha ya kuvutia sana sana! Alijilazimisha hivyo hivyo mpaka akamaliza chakula chote kwenye saani!.Cansela alipo hakikisha kuwa mgonjwa wake amesha panda kitandani aliamua kuondoka, alipo fika nyumbani kwake alishangaa kumkuta mke wake akiwa amesimama mlangoni akimsubiri.
“Sasa hivi saa ngapi mume wangu……!?”
“lili kuwa niswali ambalo lilimstua kidogo Cansela na kumfanya aangalie saa yake,
“Aaaaaa……………………..h”
Alionyesha mshangao wa wazi alipo ona kuwa ilikuwa ni saa tano usiku wakati huo!,
“A’m real so sory! There was an emergence…….!”
Akiwa na maana ya kuomba msamaha na anasema kuwa walikuwa na dharura,baada ya kusema hivyo alimkumbatia mke wake huyo na kumbusu na kwakuwa sio kawaida kutokea jambo kama hilo basi hakuona shida sana.Mkewake huyo alikuwa amemuandalia mumewake chakula na tena alikuwa ameijaza saani vya kutosha!.
“Nitaweza kula kweli na nisipo kula nita mwambia nime kula wapi…..”
Aliwaza,
“hapa lazima nitumie akili mana wanawake huwa wana vichwa vibovu hapa nikimwambia ukweli yataibuka mambo…………..ngoja nijifanye naumwa tumbo la kuhara….!”
Akahesabu;
“Moja!mbili!tat……………………………”
Kimoyo moyo kabla haja inuka na kukimbia ghafla kuelekea chooni! Jambo ambalo lilimstua sana mke wake!.
******************…………….******************…………………************************
Wale wazee wa mila wakiwa wame kaa takribani siku nne lakini hawakupata majibu yoyote yale! Walitoa kafara mpaka wanyama wote walio enda nao waliisha! Walicho kuwa wana weza kufanya ni kutulia kwa muda! Wakiwa wame kaa chini wakiwa wame kata tamaa walisikia mtetemo kwa mbali! Mtetemo ambao uliwafanya watazamane kwa hofu iliyo kuwa na furaha ndani yake!.Mara ghafla waliona kimvuli kilicho kuwa kina ongezeka ukubwa,walipo tazama juu waliona jiwe kubwa jeusi likidondoka kuelekea mahali pale walipokuwa wame kaa!.
“Eeeeeeeeeeee…………………………………….eeeeeeeeeeeeeeeeeh”
Walipiga yowe la uoga na kuanza kukimbia hovyo!yani ilikuwa ni kidogo tu lile jiwe liuwe mtu!lilitua kwa kishindo kisicho elezeka na kusababisha gogo la mti kuruka na kumpiga vibaya kiongozi wa mila ambaye alidondoka ama alirushwa hatua mita kadhaa! Vumbi lilikuwa limetanda kila kona! Baada ya vumbi kuisha vilisikika vlio mahali pale,walikuwa hawataki kuamini kama kiongozi wa mila naye amepoteza uhai baada ya kupigwa vibaya na gogo!.Walijitaidi kumuamsha kwa kufanya maombi na kumuwekea dawa za asili lakini haikusaidia!.
Ilikuwa ni kama jamii hii ilikuwa inapokea adhabu kutoka kwa mungu! Ulipita muda kidogo zilianza kusikika radi za ajabu ajabu mahali pale.Wote walitulia kwa hofu na taaruki walianza kuangalia upande ambao huenda jiwe lingine linge tokea! Wakiwa na taaruki giza lililo kuwa lime tanda likapotea na mwangaza ukaonekana! Ndipo likaoneka jiwe linguine dogo likishuka kutoka juu lilikuwa na mng’ao wa ajabu!.Wakati huo kiongozi wa mila alistuka kutoka kama kwenye usingizi wa kifo!.
“Khoooooooooo………………………oooooooooooooooooooooooooooooooo……….h”
Alikohoa na kusema;
“ tukimbieni mahali hapa kwanzaaaa……………..aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa”
Walianza kujongea kushuka chini ya mlima lakini hawa kuwa na baati kwani walikuwa wamechelewa kuondoka mahali pale! Kile kijiwe kidogo cheupe chenye mng’ao kilipo dondoka juu ya jiwe lile kubwa jeusi lile jiwe jeusi lilisambaratika kwa kuvunjika vunjika! Ulitokea mlipuko mkubwa kama mlipuko wa bomu la anatomikia!.Vipande vya mawe vilivyo kuwa nancha kali vili wachinjachinja vibaya sana! Hakuna aliye kuwa amebaki zaidi ya mkuu wa mila ambaye alikuwa hata hajiwezi! Na kijana mmoja tu machachari aitwaye Eono.
Eono alipo taamaki aliona wenzake wote walikuwa wamegawanyishwa vipande vipande!.
“Alihisi kudata! Alihisi kuchanganyikiwa! Alikuwa haamini kilicho kuwa kimetokea!
“Aaaaaaaa………………aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah”
Alilia kwa sauti sana! Alikuwa hata hajui mahali pa kuanzia wala pakuishia tena alijua kama wenzake wote wamekufa hata na yeye anastaili kufa alikuwa hana matumaini ya kupona! Wakati anatafakari hayo huku anaugulia maumivu ya dhati! Alisikia mtu akikoroma kwa upande wa chini,hakuweza kuamini alijongea nakukuta mtu huyo ambaye alikuwa anakoroma kwa maumivu amefunikwa na mawe hata asionekane sura wala miguu! Mawe yaliyo kuwa yamemfunika yalikuwa ni makubwa sana! Alikuwa hawezi kumsaidia rafiki yake huyo aliye kuwa ndani ya mawe.
Jinsi alivyo sikia mtu huyo akikoroma ndivyo Eono alipo ingiwa kama na kichaa hivi au hasira hivi,alienda na kulishika jiwe ambalo lilikuwa limefunika kwa kiasi kikubwa.Eono alibakia mdomo wazi na kuishangaa mikono yake alipo liinua jiwe lenye uzito wa juu na kulirusha mbali! Aliye kuwa amefunikwa na mawe yale alikuwa ni mkuu wa mila naye pia hata alisahau maumivu yake akiwa amebaki kushangaa jambo ambalo kijana alikuwa amelitenda! Ilikuwa inashangaza sana!.aliweza tu kusema,
“Niwewe huyoooo……………………….”
“Mmmmmmmh………………….hapanaaaaaaaaaaaaaaaaa!”
Alitingisha kichwa kukataa,lakini yule mzee akasema;
“Niwewe………..maana hakuna mtu mwingine zaidi yako aliyepo mahali hapa!”
Baada ya kumsaidia kukaa yule mzee akasema,
“Najua mimi siwezi kupona……………….”
Huku akiugulia maumivu makali na kukohoa
“Khooooooooo……………………oooooooooooooooooooooooooh”
Akavua pete iliyo kuwa kidoleni mwake pamoja na mkufu na kumkabidhi mikononi mwake na kusema;
“Kijana hii ni adhabu kutoka kwa miungu! Na miungu ime kuchaguwa wewe kuwa kiongozi wa mila!….na hayo uliyo ya ona ndiyo yatakayoooo………….”
Kabla hajamaliza sentensi ambayo kijana alikuwa haelewi ina maanisha nini alikata roho na kumfanya kijana alie kwa sauti kuu;
“Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa………………………..aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhhhhhhhhhhhhh”
Nasuti yake iliweza kusafiri umbali mrefu na kufika mpaka miji wa Mizi-Oro na mpaka kwenye ngome ya wajerumani ilifika na kumfanya Otto aulize;
“Nisauti ya nini hiyooo……………………!”
Kijana huyu alimfanyia kiongozi yule wa mila maziko anayo staili, alikuwa anatafakari sana juu ya maneno ya mwisho ya mzee yule.Alikuwa anaona kuwa haiwezekani yeye kuwa kiongozi wa mila kwani alikuwa ni kijana mdogo ambaye hata miaka ishirini haijafika! Tena yeye alikuwa sio wa uzao wa mzee huyo!.
“Sasa itawezekana vipi……..!?”
Alijiuliza na kuinuka taratibu kulifuata jiwe moja hivi na kujaribu kuliinua lakini hakuweza! Alipo kuwa anafanya hivyo aridhi ilianza kutetema na mawe yakaanza kuporomoka! Ilibidi akimbie!.
************
“Tiiii…………………………iiii………………………”
Sauti za ngoma zilikuwa zinasikika,zilikuwa ni sherehe maalumu kwaajili ya kumtawadha kiongozi mpya ama unaweza kusema ‘Maya’.Watu walikuwa wana nong’onezana wakati wanamsubiri huyo binti wa Miziya ama mfalme awasili katika viwanja hivyo maalumu,yule askari mwenye umri mdogo aitwaye Eona.Alikuwepo eneo lile la tukio akiwa pamoja na mtumishi mdogo wa kike aitwaye Iaya,walikuwa wanashuhudia mambo yalivyo kuwa yana enda.Baada ya muda kufika,wakati ambao binti mfalme huyo aitwaye Onie aliwasili.Watu walishangaa na kuanza kuulizana kwani wengine walikuwa hawamfaam! Hiyo ilisababishwa na kuto tambuliwa kwa Onie kama mtoto wa Miziya ama mflme!.
Mwanzoni kwenye kikao cha kutoa mapendekezo walikuwa wamesema kuwa Onie angeshika hatamu hiyo ya uongozi mpaka Izana atakapo kuwa na umri wa kutosha wa kuweza kuwa kiongozi lakini hilo hawakulisema!. Nasasa mji wa Mizi-Oro ulikuwa unaingia kwenye dhahama ya kutisha! Ng’ombe wa kafara alilazwa juu ya madhabau maalumu na kiongozi walio mchagua wao akafanya matambiko jambo ambalo lilikuwa kinyume na utaratibu wao! Kwani kiongozi wa mila mkuu ndiye aliye takiwa kufanya hivyo.
Kisu kilipo zama ndani ya shingo ya yule mnyama na damu kumwagika na kugusa udongo, wingu zito jeusi lilitanda na kusababisha giza zito mpaka kwenye ngome za wajerumani!.Otto aliuliza kwa mshangao,
“What the hell is going on……!”
Aliikuta nafsi yake ime ingiwa na hofu ya kutisha mpaka akajishangaa!.Eono naye kwa upande wake aliliona tukio hilo na kumfanya aseme,
“Mambo yamesha haribikaaaa…………”
Akili yake ilikuwa ikiya tafakari maneno aliyo ambiwa na kiongozi wa mila,alikuwa ameambiwa;
“Na hivi ndivyo itakavyo kuwa…….”
Bado maana ya maneno hayo alikuwa haielewi! Alijiuliza kwa mshangao na hofu!;
“Nini maana ya maneno hayaaaaa………………”
Hawa watu walikuwa wamekusudia kuvunja na kuvuruga utaratibu wa mila desturi na tamaduni zao kwani licha hata ya giza kuwa nene wao waliwasha mienge na kuendelea na sherehe zao hizo za kishetani!.Giza lile lilikuwa kama ishara ya kuwaonya juu ya jambo walilo kuwa wanalifanya!, taji ya dhahabu ambayo ilimwagiwa damu ili kuoshwa maalumu kwaajili ya Maya huyo ama mfalme mwanamke huyo kuvaa ilibadilika rangi na kuwa “Nyeusi”.Giza lilianza kutoweka baada ya tukio hilo na wakati huo Eono alifika mahali pale na kushuhudia taji yenye rangi “Nyeusi kichwani kwa binti huyo!
“Aaaaaaaaa……………….aaaaaaaaaaaaaaa….hhh”
Hakuweza kuzuiya mshangao wake! Alikumbuka lile jiwe lenye rangi nyeusi na kujiuliza;
“inamaana kama lile jiwe lilivyo tuuwa wote kule mlimani ndivyo itakavyo kuwa!”
Hakuweza kuelewa jambo lolote! Moyo wake ulikuwa na hofu kuu,wakati hayo yote yakiendelea babu mmoja alisimama na kusema;
“Wewe mtoto haramu hauwezi kuwa Maya wetuuuu………………..”
Aliongea kwa hasira na jaziba! Na kwa hali ilivyo kuwa alikuwa amemtukana kiongozi wa ngazi ya juu zaidi na adhabu yake ili kuwa ni kifo! Askari walimkamata yule mzee kwa nguvu ili kumwazibu lakini Maya alisimama na kusema;
“Mwacheniiiii………………………………………..!”
Akainuka kwenye kiti chake cha enzi na kumsogelea yule mzee ambaye alionekana kutokuwa hata na hofu moyoni mwake! Alimtazama kwa sekunde chache kabla yule mzee haja mtemea mate Maya! Alivyo fanya hivyo alipingwa gwara na kujikuta amedondoka chini! Wakati huu Maya Onie alikuwa amesha kuwa na hasira lakini alipo geuka na kutazama pembeni alimuona mama mmoja akilia sana pamoja na watoto wake,akajua kuwa ilikuwa ni familia ya yule mzee.Maya Onie akajongea juu ya kiti chake na kukaa kimya kwa sekunde kadhaa alafu akasema;
“Aieee…eee….n”
Lugha ya kimizi ikiwa na maana ya acheneni! Yule mzee shoka lilikuwa shingoni mwake hivyo amri ya Maya Onie ndiyo iliyo muokoa! Jambo hilo halikuwaa la kawaida kwa mtu aliye onyesha dharau kwa mfalme kusamehewa! Jambo hilo lili wafanya watu wasimame na kushangilia kwa nguvu!
“Maya Onie………………………………….Maya Onie……………………..Onie…………………….”
Jambo hilo lilimfanya mama Onie atoe tabasamu baada ya kuona kuwa mwanae ame kubalika kama Mfalme mke! Iaya pamoja na Eona walipo ona jambo hilo waliogopa sana! Waliondoka haraka!.
****************
“Kunajambo gani limejiri huko………….!?”
Aliuliza kwa shauku na hofu!”
“Onie amevalishwa taji kuwa Maya na watu wame mshangilia kwa nguvu baada ya kumsamehe mzee aliye mletea dharau mbele ya hadhara!……”
“Eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee………………..h”
Ipraya baada kusikia hivyo alistuka na kujikuta amesema;
“Itakuwaje sasa……………………..!?
Kwasauti ya chini ambayo mtu wa pembeni yake hakusikia,walikuwa wana waza kuhusu mtoto huyo mdogo ambaye ndiye mwenye haki ya kuwa Maya! Walikuwa wana ogopa hila ambazo zingeweza kuibuka!.Ipraya alijongea hadi kwenye kitanda ambacho Izana alikuwa amelala,machozi yalianza kumdondoka!.
“Kwanini Mizana umeondoka ukatuachaaaa…….ona sasa majanga yanayo tokea! Tutafanya nini sisi sasa!? Tuta fanya nini…..!?
Iaya alimsogelea Ipraya na kumfariji! Akimwambia;
“Sikuzote haki haiwezi kupotea kamwe! Labda itachelewa tu kupatikana lakini haki haiwezi kupotea…. Mama yangu alikuwa ananifundisha kila kitu juu ya kumuomba Mungu kwani yeye ndiye mwenye haki!”
Alijitaidi kuongea kwa lugha na sauti ya upole ambayo ilisaidia kumtuliza Ipraya.Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwani walikuwa hawajui kuwa Onie atafanya nini kwa binti huyo mdogo ambaye ndiye inasemekana anahaki ya kuwa Maya ama mfalme mwanamke.Watu walikuwa hawajui hatua ambazo miungu yao itachukua! Watu walikuwa hawajui kama Mizana alikuwa amekufa! Wakati vita hiyo baridi inaibuka wajerumani nao walikuwa wanajiandaa kuanzisha vita upya na jamii hii!.
****************
“Sasa hapa nita fanya nini maanaaa…………………!”
Eono alikuwa anawaza jinsi atakavyo iambia jamii juu ya yeye kuchaguliwa kuwa kiongozi wa mila kwa sababu alikuwa sio mtoto wa familia ya mzee wa aliye kuwa kiongozi huyo! Watoto wa familia hiyo wata muelewa atakapo waambia kuwa baba yao amekufa na yeye ndiye aliye teuliwa kama kiongozi wa mila! Kufanya hivyo huenda ange onekana kuwa mlafi wa madaraka!.Swali lingine alilo kuwa analiogopa ni kuwa kwa nini yeye amepona kama kweli wengine wamekufa!, aliwaza mengi sana lakini mwishoni ali amua kujongea kuelekea nyumbani kwa aliye kuwa kiongozi wa mila.
Alipo fikaka watu walimuangalia kwa mshangao mkuu! Walimzunguka kwa mshangao naye akawasalimu na kuwaambia;
“Nina habari ya kuhuzunisha…………………………………aaaaaaaaaa”
Aliwasimulia yalio kuwa yamejiri huko na kwamba kiongozi wa mila amepoteza uhai!
“Eeeeeeeeeeeeeeeeeee……………………………………eeeeeeeeeeeeeeeeh”
Vilio vilisikika! Watu waliomboleza kwa kugaragara chini! Sasa Eono alikuwa anakabiliwa na jambo gumu sana la kusema kuwa yeye ndiye amechaguliwa kama kiongozi wa mila ingezua taaruki!.Akiwa anayatafakari hayo aliingiza mkono wake kwenye mkoba wake nakutoa pete pamoja na kidani ambacho kilikuwa kina valiwa na kiongozi huyo mkuu wa mila! Watu walivyoona hivyo ndio wakazidisha kulia kwa nguvu zaidi!.Ndipo Eono akafanya jambo ambalo liliwashangaza wengi jambo ambalo lili vifanya vilio vinyamaze ghafla kanakwamba kulikuwa hakuna jambo lolote lilikuwa limeendelea!.
Hiyo ilikuwa ni baada ya Eono alijivalisha pete na kile kidani mbele yao! Alafu akasema;
“Mimi ndiye mkuu wenu wa mila ninaye fuataa……………………………………..!”
*************………………..******************……………..******************************
“Amenitoa usichana wangu…………………………………………..u”
“Usilieeeeee……………………………………….eeeeeeeeeeeee”
Yule daktari mmama alikkuwa anamfariji Jenny kutokana na kitendo ambacho alikuwa amefanyiwa na yule mkuu wa majeshi mpya ama Otto,ni jambo lililokuwa linamvuruga sana na kumuumiza! Alikuwa anajiona kama sio mwanadamu wa kawaida,aliiona thamani yake ilikuwa imeshuka kabisa! Lakini yule mama daktari alimwambia kuwa asiwe na hofu!.
“Fanya kama haujui kilicho tokea na mimi sita mwambia mtu yeyote yule….wanadamu tumeumbiwa matatizo lakini hatuja umbiwa kushindwa matatizo! Mungu ametupa nguvu ambayo ni chemichemi ya kila mmoja wetu,chemchem ambayo ni neno lake.Hivvyo nakutia shime kuwa usikate tamaa juu ya jambo mbalo limetokea, jipe moyo kwa kuwa yote hayo yamepita!”
Wakati hayo yanaendelea mlango ulisikika ukigongwa,Jenny alijifuta macho yake,akajiweka vyema na kwenda kufungua mlango,
“Karibuuuu………………….”
Alikuwa ni Cansela Von Soden.Alipo ingia na kumtazama Jenny aligundua kua alikuwa analia! Aliuliza tu kwa mshangao;
“Ulikuwa unaliaaaaaaaa………………………………”
Kabla haja msalimia yule mama daktari na kukaa.Jenny akasema;
“Hapana huku akitingisha kichwa.!”
Kabla Jenny haja jibu yule mama dktari alisimama huku akiangalia saa yake na kusema;
“Jamani acha niendeee…………………….!”
“Karibu tena! “
Jenny alisema kwa changamko na tabasamu japo hafifu na kumfanya daktari yule naye atabasamu! Akijua kuwa yale maneno machache ambayo alimwambia Jenny yalimsaidia,aliweza tu kujibu kwa furaha;
“Nashukuru Jenny……………………………….!”
Kisha akaondoka.
“Nikuandalie nini…………………………………………………!?”
Jenny aliuliza huku anasimama.
“Hapana Jenny mimi nimepita hapa kukujulia hali tu wala usijali………mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh! Sikunyingine nita kula usijali……! Naaaaaaa…. Acha niwai basi wewe endelea kupumzika mpaka utakapo kuwa vizuri utaniambia!”
Jenny alikuwa kimya tu ana mtazama wakati anaongea na kusema,
“Tumekumisi sana kule ofisini………………….!”
Sentensi ambayo iliufanya moyo wa binti uruke ruke na kujiisi kama alivyo kuwa mwanzo japo kwa dakika chache!.
****************………………***********************…………………********************
“Itawezekana vipi……..!…..unajua ukikaa kimya juu ya jambo hilo nini kitakacho tokea…!?”
Lili kuwa ni swali ambalo lilimfanya Maya Onie ainamishe kichwa chini wakati mama yake anaendelea kusema,
“Mimi kama mama yako ni lazima unisikilize!………..hauna haja ya kuionea haya jamii hii kwa kuwa bado haujui nini kilicho kuwa kime tokea nyuma!…..wakati ukifika nita kwambia nakuomba utekeleze jambo hiliiiii……………………………….!”
Aliinamisha kichwa na kuondoka! Akimuacha Maya Onie akimsindikiza kwa macho,wakati huo hakuweza kuyazuiya maneno ya mama yake! Yalikuwa yanajirudiarudia kichwani mwake.
“Mmmmmm……………………………………………mh!”
Aliwaza;
“Ayaasemayo mama ni ukweli mtupu! Nakumbuka jinsi ambavyo tumeteseka lakini siwezi kuuwa mtu! Lakini nitafanya kama mama alivyo kusudia ilinimridhishee………….!”
Alijisogeza karibu na kitanda chake na kukaa huku mawazo yakiwa bado yana muandama!;
“Kwani mama anasiri gani mbona kila siku………! Tangu nikiwa mdogo ananisisitizia kuhusu siri na hani ambii akidai kuwa ni mdogo!……sasa hivi nimekuwa nina miaka kumi na nane! Lazima aniweke wazi asinifanye kuwa mimi ni mtoto mdogo…..”
Alimuita mpambe wake aitwaye Eo ambaye ndiye aliye kuwa amempigia debe tangu mwanzo na kumwambia;
“Wewe nimekuchagua uwe kiongozi wa maswala ya juu hivyo nakuomba usiniangushe! Ninataka kichwa cha yule mzee aliye nitemea mate na kuni dhiaki!…….”
Aliongea kwa amri sana mpaka Eo alistuka na baada ya kusema hivyo akaongezea kwa kusema;
“Nakuamuru uende………………………..”
Eo aliinamisha kichwa kabla ya kuondoka na kusema;
“Kama utakavyo eeee……………..h ……..mtukufu Maya…!”
*******************
Eono naye akiwa anapita hana hili wala lile alistuliwa na kugongwa na vijana waliokuwa wame shikilia mfuko ulio kuwa na kitu hivi!.
“Aaaaaa……..h”
Eono alishangaa na kusema moyoni mwake kwa mshangao wa hali ya juu;
“Hawa jamaaaa…………………….namna gani hawa……………………………!”
Hakuweza kuwaelewa hata kidogo! Lakini kule walipotokea vijana hawa wakikimbia zilikuwa zinasikika sauti za watu wakilia kwa sauti za maombolezo! Eono alikimbia na kuelekea eneo la tukio na kuukuta mwili wa mzee ambaye aalimkumbuka vyema kuwa ndiye aliye mkemea Maya ambaye hastaili kuwa Maya na kumtemea mate usoni! Aliweza kusea tu kwa sauti ya kunong’oneza ambayo hakuna mtu aliye weza kumsikia;
“Mayaaaaaaa……………………………………..aaaaaaaaaaaaaaaaaaa……………..h”
Aliinuka haraka na kuanza kukimbia kuwa fuatilia wale vijana ambao alikuwa na imani ndio walio kuwa wameya tenda hayo! Alikimbia huku na huko kwenye vichaka! Moyo wake ulichoka na kukata tamaa kuwa alikuwa amesha wakosa!.Alijilaza kwenye nyasi akiwa na uchovu mwingi ulio sababishwa na mawazo! Akiwa pale chini akitazama mbala mwezi alisikia sauti kama zawatu hivi wakiongea! Kwa mshangao,na taadhari alisimama taratibu na kuwaona vijana ambao hakuweza kujua walikuwa ni wakina nani. Alijisemea moyoni mwake;
“hawa watakuwa ni wawindaji hawa…..”
Aliporudidisha uso wake kwa upande wa pili aliweza kuuona mfuko ulio kua umelala juu ya dibwi la damu nzito!
“Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa……………….aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa…………………h”
Alishangaa! Aliukumbuka ule mfuko na kuwatambua vijana hao vyema kuwa ndio walio msukuma mda ule baada ya kufanya mauaji ya kutisha! Alianza kuwaza afanye nini?.Moyo wake ulikuwa unaogopa sana! Akiwa anawaza yale alikumbuka jinsi alivyo weza kulisukuma jiwe kumbwa kule mlimani! Jambo hilo lilimfanya apate nguvu na kuamua kujitokeza mbele yao!.Wale vijana walistuka na kushika silaha zao! Wakiwa tayari kujiami!.
“Nyinyi wauwaji mnafikiri mnaweza kujificha juu ya maovu yenu mnayo ya fanya………………………..!?’
Akaacha kama swali kwao kabla mmoja wao haja uliza akiwa anajiamini;
“Nani wewe…………………………………….h!?”
“Naitw Eona………….. mimi ndio mwamuzi wa mizi……!”
“Haaaaaaaaaaaaaa………………………………aaaaaaaaaaaaaaaa…………………..h”
Aliposema hivyo wale vijana waliangua kicheko cha kejeli! Kwasababu mwamuzi ni mtu mwenye nguvu nyingi sana tena ambazo sio za kawaida ndiye anaye takiwa kupewa cheo hicho!.Walimtazama kwa dharau sana! Mmoja wao ambaye alikuwa ndio kama kiongozi ali mteuwa mmoja wao na kumwambia;
“Mtaunyaaaaa……………………….”
Lugha ya kimizi akiwa na maana ya mmalizie mbali! Na wengine waka kaa wakiendelea kuota moto! Yule muuaji ambaye alikuwa amechaguliwa kwa dharau alimpatia Eono silaha na yeye akabaki bila ya silaha yoyote!. Aliuangalia mwili wa kijana ulivyo mdogomdogo basi akamdharau! Eono naye kwa dharau na madaha alitupa silaha pembeni na kusema kwa kujiamini;
“Hata mimi sina haja ya kutumia silaha nita kumaliza kwa mikono yangu mwenyewe………….”
“Haaaaaaaaaaaaaaaa…………………….aaaaaaaaaaaaaaaaaaa………………h”
Maoni Mapya