Mhadhiri UDSM awataka Watanzania watumie fursa za Kiswahili Afrika Kusini

Subira Kawaga, Swahili Hub

Dar es Salaam. Nguli wa Kiswahili Anna Masoke wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema Afrika Kusini ni moja ya nchi ambayo kiswahili kinapigwa chapuo.

Akizungumza katika kipindi cha Lulu za Kiswahili cha TBC 1 hivi karibuni, alisema zipo lugha rasmi kumi na moja (11) zinazotumika nchini Afrika Kusini.

Akizungumzia kuhusu utafiti uliokuwa uliofanywa na Prof Aldin Mutembei wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam huko Afrika kusini pamoja na wadau wengine kama Prof Hassan Kaya na Balozi wa Afrika Kusini, Meja Jenerali mstaafu Gaudence Milanzi, alielezea namna ambavyo  lugha ya kiswahili ina dumisha urafiki uliyopo kati ya Tanzania na Afrika kusini.

“Afrika Kusini ni Jamhuri ambayo ina uchumi mkubwa katika Afrika, na moja ya kitu kinachotuunganisha ni lugha ya Kiswahili. Tanzania tumekuwa watu wa kwanza kueneza lugha ya Kiswahili kule Afrika Kusini tangu enzi za ukombozi,” alisema.

Aliongeza kuwa, hata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa chuo cha kueneza lugha ya Kiswahili Afrika Kusini. Hivyo kama kiswahili kitapokelewa kwa nguvu Afrika Kusini,itakuwa mchango  mkubwa na msukumo mkubwa wa katika nchi nyingine za Kiafrika kama vile Botswana.

Baadhi ya mikakati inayofanikisha maendeleo ya Kiswahili nchini Afrika Kusini ni pamoja na;-

 kuanzishwa kwa mafunzo ya lugha  ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2011 ambapo, Anna Maseke  alikuwa Afrika Kusini kushiriki mkutano huo uliozaa matunda kwa ufundishaji wa somo la Kiswahili.

“Jambo la msingi linalopaswa kufanywa ni kuandaa mazingira  katika ngazi za elimu kuanzia shule za msingi, sekondari na katika vyuo,” alisema Masoke.

Aliendelea kutaja  vyuo vikuu vitatu anavyo visimamia katika somo la Kiswahili  ambavyo ni; Kwazuna Tower, Zulu Land na Kenya ambapo wanafunzi wao wa uzamivu (PHD) hupeleka mitihani yao kwake.

Sasa hivi wanaofundisha lugha ya Kiswahili Afrika Kusini ni baadhi ya watu wanaotoka DRC Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), ambao wanajua Kiswahili.

Kwa upande wa Tanzania kwa sasa hakuna tangu aliyekuwepo Afrika Kusini Dk Rajabu Chipila kumaliza masomo ya Uzamivu, kutokana na kwamba mkataba ulikuwa ni kwamba;watu wanakwenda kusoma masuala ya uzamivu huku wakifundisha Kiswahili. Mkataba huu ulilenga kutupa faida sisi na wao pia (Afrika kusini).

“Mbinu iliyopo sasa hivi ni kuandaa mazingira ya watu wa Afrika Kusini kukubali lugha ya Kiswahili na ndio maana tunadhani njia bora zaidi ni kutumia lugha zao ili kujua lugha ya Kiswahili,” alisema.

Pia amezungumzia juu ya mikakati ya ziada iliyopo katika kulikamilisha hilo akieleza kwamba, baada ya mwaka 2012 kuanza ufundishaji wa lugha ya Kiswasili vyuoni, wao wenyewe pia wamekuwa na jitihada za kuleta wanafunzi huku kwetu na kurejea kwao kuendelea kufundisha kiswahili kama wakina Zukule na Kokepu.

Wanafunzi hao walijifunza Kiswahili hapa nchini na kwenda kukifundisha kwao. Vilevile baada ya Kiswahili kukubalika SADC, zipo jitihada za kuweka miundombinu ya namna ya kukiendeleza Kiswahili ikiwa sio tu Afrika Kusini hata nje ya hapo.

Pia kuandaa zana za kufundishia, hata hivyo

 kwa sababu Uviko uliibuka mwaka 2019 na Kiswahili kukubalika SADC ilikuwa ni 2018.

Kupitia kazi data kutoka Bakita, wataalamu mbalimbali wa lugha ya Kiswahili watachaguliwa ili kukifundisha Kiswahili Afrika Kusini, ingawa bado mchakato huu haujaanza rasmi.

Kwa sasa hali ya Kiswahili Afrika Kusini ni kubwa ukilinganisha na hapo awali. Hii imesababiswa na kutokea kwa msuguano wa Waafrika Kusini katika kuhimiza lugha ya Kiafrikana ambao ulileta machafuko na watu kuuwawa.

Kinachofanyika sasa ni kuwafanya waone kwamba Kiswahili sio adui bali ni rafiki na kutambua kwa namna gani Kiswahili ni mwendelezo wa ukombozi.

Masoke alisema, “Baadhi ya sababu zinazopelekea kukosekana kwa wafundishaji wa lugha kutoka Tanzania na badala yake kongo na kenya , ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa mshawasha(utayari/upenzi) wa kujifunza Kiswahili ukilinganisha na wageni wanapokuja kujifunza lugha hii.”

“Hapa kwetu msukumo wa kufanya watu wajivunie na kujigamba na kukinadi Kiswahili ni mdogo. Sisi tu hatuwezi kunadi mambo mengine tofauti na lugha ya kiswahili hivyo, bado tuna huo udhaifu. Hivyo inabidi tuongeze nguvu katika kukinadi Kiswahili.”

Kwa upande wake Meja Jenerali mstaafu ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania huko Afrika Kusini, Gaudence Milanzi alisisitiz kukieneza zaidi kiswahili Afrika kusini kupitia lugha zao.

“Lugha ya Kizulu inatumika kufundisha Kiswahili kwani kuna vitabu ambavyo vimeandikwa kwa lugha mbili ambayo ni Kizulu na Kiswahili vinavyotumuka kufundishia katika vyuo mbalimbali Afrika kusini kikiwemo Chuo kikuu cha Kwazulu-Natal.”

Pia alieleza ni kwanini zinatumika lugha za kikabila kujifunza Kiswahili huku akitolea mfano katika baadhi ya lugha za Kiafrika ikiwemo Kisandawe na Kizulu kwamba katika lugha hizo yapo maarifa mbalimbali yanayogusa nyanja zote, ambayo hupaswa kujulikana hivyo lugha ya Kiswahili iwe ni kiunganishi cha maarifa yote yatokanayo na lugha hizo.

Author: Gadi Solomon