MISEMO YA KISWAHILI NA MAANA YAKE

Wahenga ni wazee wenye akili waliotutangulia. Walifikiria na kutunga misemo kwa lengo la kuadabisha, kuonya, kukumbusha wajibu wa kila kundi katika jamii. Ipo misemo ambayo inawagusa vijana, wazee, watu wazima, wanawake, wanaume.

Mathalani vifo vya wajawazito vilipokithiri enzi hizo, wahenga walibaini chanzo ni ulaji wa mayai kipindi chote cha mimba na kusababisha mtoto kunenepa sana huko tumboni na kushindwa kupita kwenye njia ya uzazi. Hivyo, wakaanzisha msemo kama, ‘Mama mjamzito akila mayai, mtoto atazaliwa bila nywele’ ili kuzuia ulaji wa kupindukia wa mayai kwa wajawazito.

Tupitie misemo hii ya wahenga;

1. Huwezi kusukuma gari bovu ukiwa umekaa ndani yake

Hii inamaanisha lazima uteremke chini. Maana hiyo inakwenda mbali zaidi kwamba unapohitaji kutatua tatizo ni lazima uwashirikishe wengine waliokuzidi maarifa.

2. Samaki anayefumba mdomo wake, hashikwi na ndoano ya mvuvi

Ni ushauri kwamba ujiepusha kuzungumza kila jambo kwani kuna watu wengi huenda wana hamu ya kukunasa kupitia kukosea kwako. Kumbuka hakuna binadamu mkamilifu chini ya jua.

3. Maskini hana hoja, ana haja

Inatukumbusha kwamba tufanye kila njia kuukimbia umaskini.

4. Hujafa hujauumbika

Kila mtu anathamani, uhai ni suala la muda tu.


5. Mwenye kuni hula vilivyoiva, lakini mwenye pesa hula vitamu

Ni busara inayotukumbusha kutojisahau na mafanikio tuliyonayo kwani kuna neema katika kuongeza bidii.

Author: Gadi Solomon