MKWE WA RAIS – 6

NA MTUNZI MUSTAPHA MTUPA

ENDELEA SEHEMU YA SITA…

Ilichukua dakika kama 30, baadaye akarudi huku akiwa na tabasamu usoni kisha akasema

“Kijana tunashukuru, na samahani kwa kukupotezea muda” alionge maneno hayo na kutoka ndani ya chumba hicho na baada ya dakika mbili waliwasili maaskari wawili ambao walimuamuru Fred awafuate, aliwaongozana nanao  na safari yao ikakwama kwenye sehemu ambayo alitakiwa kupewa makaratasi ya kusaini, kisha akapewa kiasi cha pesa na nguo za kuvaa na kuruhusiwa kutoka kituoni hapo.

Aliona ni kama miujiza tu inaendelea kumtokea, hakujua yule binti alikuwa nanini hasa hadi akashikiliwa vile, wale watu walikuwa wanapigana kwa sababu gani hasa, yote hayo yalikuwa ni maswali yaliyotawala kwenye ufikirivu wake, lakini hakuwa na jibu alilopata.

Alipotoka kwenye kituo cha polisi nje aliita taksi na kuanza safari ya kurudi alipokuwa anaishi, akafika nyumbani saa moja usiku, aliingia moja kwa moja hadi chumbani kwake, bila ya kuoga wala kula akajitupa  na jinamizi la usingizi likampitia hadi kesho yake asubuhi na mapema ambapo aliamka na kuhisi uchovu mwili mzima lakini alijinyanyua kiuvivu ili ajiandae kwa ajili ya kwenda kazini.

Alipotoka sebuleni alikutana na Thoby ambaye alisalimiana naye na akaongea naye habari nyingine..hakutaka kabisa kumgusia kile kilichomtokea jana yake.

Alijiandaa na kuelekea kibaruani kwake mapema kabisa kama ilivuokuwa kawaida yake.

Alianza kufanya kazi aliyopangiwa na kiasi cha saa tano hivi asubuhi, meneja wake alimuita na kumwambia kulikuwa na wageni wake wangehitaji kumuona.

“Wageni gani tena hao jamani..yale mambo ya jana hayajaisha tu” Fred aliongea kimoyo moyo huku hali ya wasi wasi ikimtawala.

Hakukuwa na namna zaidi ya kwenda kusikiliza wito na alijongea hadi kwenye mlango wa chumba alichoambiwa kuwa aende na kabla ya kuingia akakutana na mzungu mmoja hivi alivaa suti nyeusi…akamsimamisha na kumkagua  kisha akamruhusu kuingia kwenye chumba hicho ambapo alikutana na sura ya yule dada wa kizungu huku mkononi akiwa ameshika ua, pembeni yake kulikuwa na wazungu wengine wanaume wawili ambao itoshe kusema walikuwa ni walinzi wake

Haiba yao haikutofautiana sana na haiba ya yule mmoja aliyemkagua mlangoni.

“Pole sana na asante kwa kuniokoa..”yule dada aliongea huku akitembea kumsogelea Fred na alipomfikia alimpa lile ua aliloshika, kisha akamkumbatia kwa sekunde kadhaa.

Butwaa likamkumbwa Fred, kwa sababu hakutarajia kile ambacho kilifanywa na dada huyo.

“Niatwa Linda” baada ya kumbatio yule dada alinyoosha mkono wake na kutaja jina lake.

Kwa kusita Fred naye alinyoosha mkono na kujitambulisha.

“Kijana tunakushuru sana kwa ujasiri wako, lakini kilichotokea iwe siri yako, hatutaki rais wetu ajue”mmoja kati ya wale walinzi aliongea huku akionyesha kuwa hatanii kwenye mazungumzo yake.

Maneno yake yakasababisha  Fred apate mshangao na akajikuta anauliza “Rais wenu!? mbona sikuelewi”

“Ooh wewe hujui kama huyu ni mtoto wa Rais wa Lithuania?”yule njemba akajibu kwa kuuliza swali.

“Ningejua nisingeuliza” Fred naye akajibu kwa kujiamini.

“Jamani, mambo yasizidi sasa, tumekuja hapa kumshukuru na sio kumtisha, kwanza naombeni mnipishe nina mazungumzo naye binafsi” mazungumzo  hayo ya mabishano yalikatishwa na Linda ambaye alitoa amri iliyo sababisha wale walinzi wasitie neno zaidi ya kutii na kutoka kwenye chumba hicho.

“Samahani sana kwa maneno yao, wale wanajua kucommand tu, hata sehemu za kuelekeza” Linda akamwambia Fred.

“Usijali, kawaida tu hiyo”

“Inawezekana ikawa umeshangaa na hadi sasa hujajua mimi ni nani hasa,  kama nilivyokwambia naitwa Linda, mimi ni mtoto pekee wa rais wa Lithuania, lakini sipendi na nachukia sana kuwa na hii stutus, maana sina uhuru”Linda alijitambulisha mwisho akaanza kulalamika juu nyadhifa yake.

Fred alishtuka sana kusikia vile, hakutegemea kabisa kama muda wote huo alikuwa anaongea na mtu mwenye wadhifa mkubwa kiasi hicho na badala ya kutia neno alibaki amepigwa na butwa tu, huku akitumbua macho kama Simba jike anayewinda.

“Hellow”Linda alimshtua Fred ambaye baada ya kusikia anasalimiwa kama ishara ya kuitwa alishtuka na kurudi kwenye hali yake.

Huku akiwa na kigugumizi Fred akasema”m..i…m..i naitwa Fred, natokea Tanzania, Afrika”

“Woow Tanzania, huko ndio ipo Zanzibar..?”

“Ndio”

“Natamani siku moja kwenda hapo”

Linda alionekana kuwa alishasikia kuhusu Zanzibar, sehemu ambayo watalii wengi Duniani hupendelea kutembelea.

“Una muda gani hapa Saudia? Unafanya kazi pekee au unasoma?”Linda alimpachika Fred swali lingine.

“Amna sisomi.. nipo hapa kufanya kazi, sina muda mrefu sana.”Alijibu Fred kwa ufupi.

“Oooh ok, mimi nipo hapa nasoma soma namalizia miaka yangu miwili ya mwisho”

“Oooh hongera sana, Mungu atakujaalia utamaliza tu”

“Aa asante, Aamh na..naomba nikushukuru tena kwa wema wako,”Linda aliongea hivyo huku akifungua pochi yake kisha akatoa bahasha ambayo alimuomba Fred aipokee.

“Hii ni nini Linda?”

“Pesa hii nimekupa kama asante kwa wema wako”

“Hapana Linda sikufanya ili nilipwe, niliamua tu kujitolea na kukusaidia” Fred aliongea huku akivibandanisha viganja vyake vya mikono kuashiria shukrani.

“Wewe! Unakataa pesa?”kwa mshangao huku  bado akiwa amenyoosha mkono wale ulioshika bahasha Linda alimuuliza Fred.

“Sijakataa pesa, lakini nakataa msaada wangu kununuliwa kwa pesa, mimi nilikusaidia kama zawadi, sikuwa nahitaji malipo,”Fred alienedelea kusisitiza na kukataa bahasha ile.

Baada ya kumlazimisha kwa muda Linda alikata tamaa na mwisho ikabidi akubaliane na matakwa ya Fred.

Walichukua kiasi cha dakika 30 hadi wanamaliza kuzungumza na wakati anaondoka Linda alimuachia Fred Business Card,kisha akamwambia kuwa ampigie wakati wowote ikiwa anahitaji msaada wake.

Fred alirudi kumalizia kazi yake na akajikusanya kurudi  mahali anapoishi, kuupumzisha mwili wake.

Wakati anaingia mlangoni alikutana na viatu vyakike ambavyo kwake vilikuwa ni vigeni, lakini pembeni ya viatu hivyo pia kulikuwa na viatu vya Thoby na kwa akili ya kiuandamizi alifahamu tu kwamba mshikaji wake alikuwa amefungia siku hiyo.

Kabla ya kuingia ndani akamtumia meseji Thoby.

“Kaka salama..?!”

“Salam.. vipi Mgiriki?

“Nipo nje hapa naona viatu vyakike, nikasema nisije nikaingia, nikaharibu sherehe”

“Hahaha…acha ujinga wewe ingia uende chumbani kwako, muda wa hayo mambo bado, mtoto namtengeneza kwanza”

“Poa poa, Komando la Cuba”

Kwa kipindi kifupi ambacho Thoby na Fred walikuwa wamejuana wawili hao walitengeneza urafiki ambao uliwafanya waishi kama ndugu hata kiasi chakuwa na utani mwingi.

Fred aliingia ndani na kujitupa kitandani, muda wote huo taswira ya Linda ilikuwa inatembea kwenye mirija ya ubongo wake.

Kiuhalisia Linda alikuwa ni mzungu lakini umbo lake lilikuwa ni kama mswahili wa Mbagala, alikuwa ana umbo la Kiafrika haswa, nyuma alijazia, mguu wa bia.

“Aaah nawaza nini? zigo kama lile nitaliwezea wapi”

Baada ya kuona mawazo ya mwanamke yule yanazidi kumtawala, Fred akajikuta anajikatisha tamaa mwenyewe na mwisho akatasamu.

Kwa kuwa ilikuwa bado jioni alijifunika shuka na akashtuka mida ya saa mbili usiku ambapo alielekea jikoni kwa ajili ya kuandaa msosi.

Wakati anatoka kwenye chumba chake alishuhudia mwanamke mmoja hivi mwenye haiba ya kichina akitoka chumba cha Thoby huku ameshika viatu na pochi yake akitembea kwa mwendo wa haraka.. wakapishana bila hata ya kusalimiana.

Fred alimuangalia mwanamke yule na hakutaka kujishughulisha naye sana zaidi alipuuza na akaenda jikoni kuandaa msosi, kisha akaupiga na akalala.

“Ngo ngo ngo, ngo ngo ngo” akiwa katika usingizi mzito, kwa mbali Fred alisikia wa chumbani kwake mlango unagongwa ishara ya mtu kubisha hodi.

Hakujali sana…alijua labda ni mawenge yake ya usingizi na pengine hiyo ilikuwa  ni ndoto.

“Ngo ngo ngo, Ngo ngo ngo” mlango ukagongwa tena.

Raundi hii alishtuka kutoka usingizini na kukaa kitako.

“Thoby kama una njaa nenda kale jikoni, nimebakisha chakula”kiuvivu Fred aliongea.

“Unaweza kufungua mlango tafadhali”alisikia sauti ya mwanaume ikimjibu lakini ajabu haikuwa sauti ya Thoby kama alivyodhania.

Kidogo wenge la usingizi likamtoka na akanyanyuka taratibu kuelekea mlangoni kujua ni nani aliyekuwa akibisha hodi kwa muda huo.

Mara baada ya kufungua mlango alistaajabu kuona kilicho mbele yake.. hata akaishiwa nguvu.. asijue hata aseme nini..

………………SIKU MOJA NYUMA………..

“Imeshindikana mkuu, tulikuwa karibu kumteka,  lakini yule jamaa akaja kuingilia kati, akazidisha namba ya wapinzani mwishowe akaondoka na lengo letu.

“Shiiit! Mmeshafuatilia huyo jamaa background yake? Nataka  alipe kwa alichofanya, tumpe adhabu itakayomfanya ajue ukubwa wa kosa alilofanya”

“Tumefuatilia lakini cha ajabu anakaa nyumba moja na Thoby, inawezekana yeye ndio alimtuma kwa sababu  ilikuwaje hadi yeye akagundua sehemu tuliyokuwa tunafanya tukio, zaidi ilikuwa ni siri kati ya yetu”

“Kama ni hivyo na huyo Thoby mwenyewe awajibishwe sitaki kuona hata wakipumua..najua mshanielewa namaanisha nini..”

Hayo yalikuwa ni mazungumzo baina ya tajiri mmoja maarufu duniani dhidi yawafanyakazi wake wakiwa kwenye jengo moja la kifahari nchini Saudia.

Aliwapa kazi ambayo ilionekana kukwamisha na Fred kwa asilimia kubwa kwani yeye ndio anatajwa kwamba aliharibu mchongo.

Mbali ya ukweli kwamba Thoby alikuwa akijifanya kazi kama daktari nchini Saudia kwenye hospitali ya (Akswa Hospital), pia alikuwa ni mmoja wa wanachama wa kundi la kigaidi lililokuwa linaongozwa na tajiri aliyeitwa Dashki Zomoni ambaye alikuwa ana uraia pacha wa Urusi na Lithuania.

Asilimia 70 ya utajiri wake ulitokana na uuzaji wa madawa ya kulevya na biashara nyingine haramu.

Lengo lake kubwa kwa muda huo lilikuwa ni kumpindua rais wa Lithuania ambaye ni baba yake Linda.

Hivyo katika harakati hizo akawatuma watu wake kumteka Linda ili kumpa shikinikizo baba yake aachie madaraka.

“Tumekuelewa mkuu, subiri majibu mazuri, tunakuhakikishia kwamba wakati huu hatutokuangisha.”

“Kazi njema”

Kesho yake, kikosi kazi kiliondoka kwenye mjengo wa kifahari wa Dashki uliokuwepo pembezoni mwa Jiji la Riyadh kuelekea kwenye nyumba ya Thoby kwa ajili ya kufanya walichotumwa.

Mmoja kati ya watu waliotumwa kufanya tukio nyumbani kwa Thoby alikuwa ni Mwanamke aliyeitwa Rachel ambaye ndio yule mwenye asili muenekano wa Kichina.

Walipofika nje ya mjengo Rechel ndio alitumika kama chambo.

“My honey upo nyumbani”Ujumbe mfupi ulisomeka hivyo kwenye kioo cha simu ya Thoby  ambaye baada ya kufungua ujumbe huo alitasamu.

“Nipo nyumbani mke wangu”

“Nipo chini hapa nakuja nikupe vitu vyako”

“Woow ni umenisuprise, kwanza umejuaje kama ninavihitaji sana”

“Tulia basi niingie ndani, nitakupa hadi ukinai”

Rechel alishuka kwenye gari iliyokuwa na wazee wa kazi kisha akapanda kwenye lifti iliyomfikisha ghorofa ya tano ambayo Thoby alikuwa anaishi.

“Nimefika nifungulie bhasi..”

“Sukuma bhana, nimeufungua muda mrefu”

Baada ya kufika Rechel alimtumia ujumbe mfupi wa maandishi Thoby ambaye pia alijibu.

Baada ya mrembo huyo kufungua  tu mlango, akakutana na sura ya Thoy ambaye alikuwa amesimama mbele yake huku akiwa tumbo wazi na amevaa kipensi tu.

 Thoby alimrukia Rechel na kumkumbatia, kisha akamuachia busu zito kwenye paji la uso.

“Jamani una haraka wewe..fungaga huo mlango basi”

Kwa tabu Rechel aliongea huku akijaribu kujitoa kwenye kumbatio hilo.

Mlango ukafungwa na wapenda nao hao wakabebana hadi chumbani na wakarukiana tena.

 “Una asili ya china na Marekani, lakini ni kama umezaliwa Afrika”Baada ya kupewa alichokuwa anahitaji Thoby alimmwagia sifa Rechel ambaye kwa muda huo alikuwa kifuani kwake.

“Kwanini jamani?”

“Unajua namna gani ya kucheza  kwenye nafasi yako,”

“Staki bhana, wewe pia mbona unanipa ninachohitaji”

Wakati wakiendelea kupeana maneno ya kumtoa nyoka pangoni sambamba na kujazana sifa zisizokifani, Rechel alinyanyuka kifuani mwa Thoby na akasogea hadi kwenye kipochi chake kisha akachomoa simu na kubonyeza bonyeza na akarudi tena kitandani.

“Mnaweza kuingia”

Huo ulikuwa ni ujumbe ambao Rechel aliutuma kwa wenzake waliokuwa nje kwa muda huo.

Baada ya kurudi aliendelea kumpeti peti Thoby na ghafla mlango wao ukafunguliwa na zikaingia njemba zaidi ya saba.

“Umemsaliti bosi, umetuangusha leo tumekuja kwa kazi moja tu”

Mmoja ya wale majamaa ambaye alikuwa amejazia vilivyo alifungua mazungumzo baada ya Thoby kuonekana haelewi kinachoendelea.

“Jamani nimemsaliti bosi kivipi? Mbona siwaelewi?”

“Unajifanya hujui ee? Wewe si ndio ulimtuma jamaa yako aende kumuokoa mtoto wa Rais wa Lithuania kule ufukweni, usituchezee akili”

“Jamani jamani sio mi..mi..mi…mi” wakati Thoby anataka kuzungumza ili kujitetea ghafla akajikuta hawezi kutoa sauti na nguvu zikaanza kumuishia.

“Sindano imefanya kazi mapema sana, haya mtu wenu huyo mimi nawasubiria kwenye gari”Rechel ambaye muda huo alikuwa kitandani na Thoby aliongea maneno hayo na kunyanyuka kushuka kitandani.

Wakati Rechel anafanya yale aliyokuwa anafanya na Thoby alimchoma sindano ya kumuua nguvu kupitia pete aliyokuwa amevaa mkononi.

Hii ilikuwa ni mbinu iliyotumiwa ili kufanya mchakato uwe rahisi kwani waliamini kama wangemfuata bila ya kumlegeza huenda jamaa angewazidi nguvu kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kupambana.

Rechel alikusanya vitu vyake na kutoka nje, sasa wakati anatoka ndio akakutana na Fred ambaye kwa muda huo alikuwa akienda jikoni kujitengenezea chakula.

Wale majamaa waliokuwa kwenye chumba cha Thoby ni kama walikuwa wanachinja kuku wa kizungu kwani hawakupata tabu hata kidogo, walimchoma visu kadhaa na wakasubiri kwa muda kuhakikisha kwamba alikuwa ameshafariki.

Kisha wakatoka nje na kuingia kwenye gari ambako walikutana na Rechel.

“Bado mtuhumiwa kamili, lakini nashauri tusubirie kwa muda kwa sababu atatusumbua.. acha apitiwe na usingizi halafu ndio twende.”alisema Rechel na hoja yake ikaungwa mkono na watu wote.

Hivyo walisubiri kwa masaa kadhaa kabla ya kuingia tena ndani na kwenda kwenye chumba cha Fred na kubisha hodi.

ENDELEA….

Mshtuko ulimkumba Fred kwa sababu mbele yake alikuwa anamuona mmoja kati ya majamaa ambao alikutana nao kule Ufukweni wakati anajaribu  kumuokoa Linda na alikuwa na watu wengine sita, lakini pia alikuwa amekutana na sura ya Rechel ambaye alimuona masaa kadhaa yaliyopita kwamba alikuwa na Thoby.

“Umeshangaa, unajiuliza tumejuaje mahali unapoishi sio, Jamani tufanye kazi”

Mmoja ya wale wanaume aliongea na kabla ya Fred kurudisha pumzi aliyoitoa kutokana na hofu akaona mmoja wao anatoa bunduki ndogo aina ya Pistol na wakati anashangaa akashtukia kitu cha baridi kimetua kwenye shingo yake.

Taratibu akajikuta anadondoka chini, huku damu zikimtoka na macho yakifumba…

“Tuondokeni, Kazi imeisha hapo, hawezi kupona huyo”

Kwa mbalii akiwa amedondoka chini baada ya kufyetuliwa risasi akawa anasikia sauti za wale waliomfanyia tukio wakiongea na baada ya hapo hakujua kilichoendelea.

Author: Gadi Solomon