Mlimani sipandi

Na Pelagia Daniel

  1. Mke wangu mfupi, lakini huvaa nguo nyingi. Hindi
  2. Mlango wa nyumba yangu uko juu. Shimo la mchwa
  3. Mlima mkubwa wapandwa kuanzia juu. Sima/Ugali
  4. Mlimani sipandi. Maji
  5. Mlima umezuia kutazama kwa mjomba. Kisogo
  6. Mlima wa kupanda kwa mikono. Mlima
  7. Mlima wa kwetu hupandwa na mfalme. Nafasi kati ya mdomo na pua ya ngombe
  8.  Amejitwika mzigo mkubwa kuliko yeye mwenyewe. Konokono/Koa
  9. Mlima wa mwenyewe hupandwa na mwenyewe. Buibui na utando wake
  10. Mpini mmoja tu lakini majembe hayahesabiki. Mkungu wa ndizi

Author: Gadi Solomon