Mnara wa Babeli, chanzo cha lugha nyingi duniani

By Dk Levy

Ikapita miaka mingi. Wana wa Nuhu nao wakazaa watoto wengi sana. Watoto wao walikua na kuzaa watoto wengi zaidi. Na hapo ndipo kukawa na watu wengi zaidi duniani.

Mmoja wa watu hao alikuwa kijukuu wa Nuhu jina lake Nimrodi. Alikuwa mbaya aliyewinda na kuua wanyama na wanadamu. Nimrodi pia alijifanya mfalme atawale watu wengine. Mungu hakumpenda Nimrodi.
Wakati huo watu wote waliongea lugha moja. Nimrodi alitaka awakusanye ili awatawale. Unajua alichofanya? Aliwaambia watu wajenge mji na ndani yake kuwepo na mnara mkubwa na mrefu sana.
Hawa ndezi wa kale waliamini wakijenga mnara mrefu watafika mbinguni kwa Mungu. Bange za namna hii hazijawahi kuvutwa tena hapa duniani. Alijaribu kuzivuta Hitler lakini akashindwa.
Mungu hakupendezwa na mnara huo. Alitaka watu watawanyike na kukaa duniani pote. Lakini bwege yule alisema: ‘Njooni! Tujenge mji na mnara mrefu tufike mbinguni. Ndipo tutasifiwa sana!’
Watu hao kama majuha walitaka eti waheshimiwe kuliko ‘Saa Godi’. Kwa hiyo Mungu aliwaachisha kujenga huo mnara. Unajua namna alivyofanya? Aliwafanya waanze kuongea kila mtu na lugha yake. Mungu fundi nyie.
Aliyeomba tofali aliletewa udongo. Aliyeomba maji aliletewa jiwe. Na yule wa nyundo akapewa kaptula. Masela wale wakashindwa kuelewana tena. Ndiyo sababu ule mji ukaitwa Babeli au Babiloni yaani ‘Mchafuko’.
Kwa sasa tungetumia neno kama ‘dishi limeyumba’. Maji kukorogeka, ‘netiweki ziro’ au ‘skrini chenga’. Basi watu wale wakaanza kuondoka Babeli. Walioongea lugha moja walikwenda kukaa pamoja eneo lingine.
Na huu ndiyo ukawa mwanzo wa lugha mbalimbali duniani. Sasa jiulize kabila lako, na useme mlifanya nini kule Babeli. Kufyatua tofali, kubeba zege au kuuza msosi kwa wajenzi? Au nyie ndiyo wale mainjinia?
‘Enewei’ kila jambo lina mwanzo wake, ingawa linaweza lisiwe na mwisho wake. Dunia ipo hapa ilipo kwa sababu, wala siyo kwa bahati mbaya. Lakini yaliyopo ndani ya dunia yenyewe mengi yapo kwa bahati mbaya tu.
Na kadiri siku zinavyosonga mambo ya bahati mbaya yanazidi kuongozeka kwa kasi. Asilimia kubwa tunatengeneza vitu vya bahati mbaya kwa tabia na nyendo zetu. Kila baya lipo kwa bahati mbaya. Yes! Ndo ukweli.
Lakini zamani mambo hayakuja kwa bahati mbaya. Yalikuja kwa nia nzuri ya kujenga, kuimarisha, kubomoa, kuhifadhi, kudumisha, kulinda, kuokoa ama kutibu. Hivi umewahi kujiuliza nani aligundua mchanganyiko wa nyanya na kitunguu?
Kabla ya kuwaza aliyegundua gari. Basi jiulize aliyegundua nyanya na kitunguu. Kwamba ukiviweka pamoja vitaunda mboga tamu. Kuna watu walipoteza maisha ndipo tukajua hii ni sumu na hii ni dawa.
Hivi sasa watu tunaishi kama kuku tu. Kila kitu tumewekewa hakuna jipya. Hata wazungu wameacha kuwaza sana kama zamani.
Ndio maana wanaleta vitu vya bahati mbaya zaidi na kutulazimisha nasi tuvitende.

Vitu vinavyotengenezwa ama kubuniwa na wazungu kwa sasa. Ni vitu ambavyo vinarahisisha tu utendaji kazi wa vitu vilivyotengenezwa au kubuniwa ‘long taim’. Kama kuachana na mkaa na kuleta gesi. Kurahisisha tu.
Sasa mambo ya bahati mbaya yanateka dunia. Hata huku kwetu tumeambukizwa vitu vya bahati mbaya. Usishangae toto linamnunia mama au baba yake. Toto linambishia mjomba au shangazi yake. Hizi ni bahati mbaya.
Kuna makosa ambayo zamani watoto tulichezea mboko za kutosha. Lakini leo hii makosa hayo hayo yamegeuka kuwa ni kitu cha halali kwa mtoto. Tumeamua kuishi na vitu vya bahati mbaya sana.
Zamani watoto tuliishi majumbani kama tupo kambi za mafunzo ya kijeshi. Ndo maana tumekuzwa sasa na ‘fulu’ adabu. Kuheshimu watu, utu, busara, hekima na kujitegemea tukiwa na umri mdogo.
Zamani usiposalimia kwa kuwaamkia wakubwa asubuhi utapigwa kipigo cha haja. Usiposalimia wageni unapigwa tu. Lakini leo hii haya mambo ‘hayapogo’ kabisa, mitoto inaishi kama simbiisi za Udizungwa.
Zamani wakati wa chakula ukinawa kabla ya wageni unakula stiki. Ukilia bila sababu unapigwa. Ukinyanyuka wakati wa kula kabla ya wakubwa zako kuinuka unapigwa. Na hapo tuelewane, unapigwa kama kibaka. Dadeeeeki.
Enzi zetu wakubwa wakiwa wamekaa, ukaenda kusimana pembeni yao kama zuzu unapigwa. Yes! Na ukikaa ikiwa wakubwa wamesimama unapigwa tu. Unaweza kudhani utani utani hivi. Uliza!
Ukitumwa dukani ukachelewa kurudi unapigwa. Ukichelewa kurudi toka shule unapigwa. Ukiwahi kurudi toka shuleni unapigwa. Haya yote yalikuwa makosa makubwa hatukutandikwa kwa bahati mbaya.
Ukililia wageni wakati wanaondoka, wakishasepa utapigwa. Kujipitisha wakati wageni wakiwa wanakula unapigwa.
Na hii mama asingesubiri wageni waondoke, unadakwa na kipigo fasta.
Kujibu ovyo ovyo wakubwa unapigwa. Kutukana watu wazima, watoto au rika lako unapigwa. Ukiwa mbishi bila sababu unapigwa. Ukipigwa ukalia unapigwa ili unyamaze. Ukipigwa ukanyamaza utapigwa ili ulie. Dadeeeeeki.
Ukipigwa shuleni ukaenda kusema nyumbani, unapigwa tena. Ukianza kula nyama kabla ya wakubwa unapigwa.
Ukila kwa jirani ukabainika unapigwa. Siyo kula tu, hata ukihisiwa unadowea kwa jirani kichapo kitakuhusu.
Ukianza kunawisha wenyeji badala ya wageni, mkimaliza unaitwa chumbani unapigwa. Ukianza kunawisha watoto badala ya wakubwa unapigwa.
Ukikutana na mtu mzima ana mzigo halafu hujampokea unapigwa.
Ukienda kusema homu kama umepigwa unapigwa tena. Mtu mzima akipita kama mnacheza ‘boli’ hamjajishughulisha naye unapigwa. Ukienda nyumba za watu, ukaona kitu au ukasikia stori ukaileta nyumbani unapigwa.
Ukipewa hela na mtu asiyefahamika au hata anayejulikana hapa inategemea na mazingira gani unapigwa. Mtoto ukianza kuchagua chakula unapigwa. Ukianza kuwa na marafiki wasioeleweka eleweka unapigwa.
Mtu mkubwa akikuchongea nyumbani hata kama siyo cha ukweli unapigwa.
Ukikaa na wakubwa ukaanza kucheka bila sababu unapigwa. Ukimuuliza Baba/Mama umetoka wapi unapigwa. Dadeki.
Endapo umepigwa na ukasusa chakula unapigwa. Ukilala bila kula unapigwa. Na ukiitwa ukaja kimyakimya bila ya kuitikia unapigwa. Ukipiga mwayo, chafya ama kukohoa bila kuziba mdomo unapigwa. Ukisinzia kabla ya kula usiku unapigwa.
Shuleni ukipelekwa ofisi za walimu kwa kosa moja. Utapigwa na waalimu wote. Hata asiye na sababu ya kukupiga naye atatafuta sababu hapo hapo. Anaweza kukupiga kwa kosa la kutoshika sehemu uliyochapwa.
Kizazi cha sasa hakiwezi kuelewa faida ya vipigo hivi. Ndo maana watoto wetu wa kiume wanataka kushindana na dada zao kwenye matumizi ya ‘dresing tebo’. Zamani kila jambo lilikuwa na sababu, leo kila jambo la bahati mbaya.
Hata Mnara wa Babeli haikuwa bahati mbaya. Ndiyo chanzo cha lugha nyingi duniani. Dunia nzima tungeongea lugha moja ingekuwa dunia ya kindezi sana. Sasa mimi naanzaje kuongea Kihindi au Kichewa kwa mfano?

Author: Gadi Solomon