
Na Pelagia Daniel
- Msitu ambao haulii hondohondo. Mimba
- Mti mkubwa, lakini una matawi mawili tu. Kichwa na masikio
- Mti mnyanya mti kerekeche mti ah mti ah!. Ngoma na upatu
- Mti wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya thelathini. Mwaka
- Mtoto asemea pangoni. Ulimi mdomoni
- Mtu mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika tano. Mawazo
- Mvua hema na jua hema. Kobe
- Mvua kidogo ng’ombe kaoga kichwa. Jiwe
- Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote. Mgomba
- Mwadhani naenda lakini siendi. Jua
Maoni Mapya