Hapo zamani za kale katika kijiji cha inyonga mkoa wa Katavi palikuwa na familia moja iliyokuwa na baba na mama walioishi kwa mda mrefu bila kupata mtoto. Na ilipotokea mama akabeba mimba basi iliharibika kabla ya wakati wake. Waliteseka sana na tatizo hilo bila kupata msaada wowote. Ndipo alipotokea mzee mmoja anayejulikana kwa jina la Magoye aliyewaeleza kuwa kama wanahitaji msaada waende kwa mzimu Katabi anayepatikana milimani mbali kidogo na kijiji chao kilipo. Baada ya wazazi kupata habari ile kwao ilikuwa habari njema zaidi kesho yake wakaanza safari kuelekea inapopatikana milima hiyo wakiongozana na wazee wa kimila. Safari ilikuwa ndefu kiasi cha kuwafanya kutumia takribani siku tatu njiani. Hatimaye walifika milimani na kufanikiwa kumuomba mzimu Katabi awasaidie kupata mtoto na kumtolea sadaka. Baada ya maombi walianza safari ya kurejea kijijini kwao mwendo ukiwa ni uleule. Walifika salama na maisha yakaendelea baada ya siku kadhaa yule mama akapata ujauzito walioulea mpaka ilipotimia miezi ya kujifungua. Ilikuwa asubuhi na mapema ambapo Mbiti mke wa Lyaunga alipojifungua mtoto wa kiume wakaamua kumpa jina la Katabi na baada ya kubatizwa akapewa jina la Daniel. Baada ya siku kadhaa wazazi wale walifunga safari kurudi kwa muzimu Katabi kumshukuru kwa zawadi ya mtoto na kuhaidi mtoto wao atakapokua atawatumikia watu na kuwaongoza watu wake vizuri.Katabi alifungua kizazi chao kwa sababu waliiendelea kuzaliwa watu ndugu wengine wa Katabi. Ilipita miaka kadhaa ambapo Katabi alikuwa amekuwa mkubwa ambapo aliamua kuanzisha maisha katika kijiji cha jirani, watu walimpenda sana na kuamua awe mtemi wao wazee wa kijiji wakaamua kwenda kuomba katika milima ya mzimu Katabi na walipojiridhisha kuwa wamekubali, Katabi akapewa utemi na kuanza kuwaongoza watu wake kwa haki na amani. mwisho. Pelagia Daniel
Maoni Mapya