Nahau

na Pelagia Daniel

1.Kujipalia mkaa =  Ujitia matatani
2.Kumeza au kumezea mate = Kutamani
3.Kumuuma mtu sikio = Kumnong’oneza
      mtu jambo la siri
4.Kumpa nyama ya ulimi =
     Kumdanganya mtu kwa maneno
     matamu
5.Kumchimba mtu  = Kumpeleleza mtu
      siri yake
6.Kutia chumvi  katika mazungumzo  =
      Uongea habari za uwongo
7.Vunjika moyo = Kata tamaa
8.Kata maini = Kutia uchungu
9. Kujikosoa = Kujisahihisha
10.Kutia utambi  = Kuchochea ugomvi

Author: Gadi Solomon