Penye wengi hapaharibiki neno

Na Pelagia Daniel

  1. Sanda ya mbali haiziki, sanda maana yake ni nguo ambayo huvishwa maiti akazikwa nayo. Methali hii ina maana ya sanda ambayo iko mbali na sehemu ilipo maiti haiwezi kuvishwa maiti, ni sawa na fimbo la mbali kushindwa kuua nyoka.
  2. Riziki hufuata kinywa, unapotaka kula chakula (riziki) huna mahali pengine utakapokipeleka isipokuwa kinywani kwa sababu kinywani ndipo palipokusudiwa kuingia riziki sikioni au puani haiwezi kuingia. Methali hii ina maana ya riziki uliopangiwa wewe haiwezi kwenda kwa mtu mwingine hata mtu akijalibu kuizuia usiipate.
  3. Penye wengi hapaharibiki neno, methali hii ina maana ya mahali ambapo pana watu wengi, watakuwako wabaya na wazuri. Hivyo pakitokea jambo litakalotaka kuleta mafarakano lazima atatokea mmoja katika hao akasuluhisha badala ya kufanya mambo yaharibike.

Author: Gadi Solomon