Rais mstaafu Mwinyi atunukiwa heshima kuwa mlezi

Rais Mstaafu wa Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi ametunukiwa heshima ya kuwa mlezi wa kwanza wakati wa kikao cha Mpango wa kutumia lugha za asili za Afrika (Kiswahili) kufundishia lugha za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na maarifa na falsafa asili za Kiafrika (African indigenous languages, knowledge and home grown philosophies) kilichofanyika Jiji la Durban Afrika ya Kusini wiki hii.

Rais mstaafu wa Tanzania, awamu ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi (katikati waliokaa), katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kikao kazi cha Mpango wa kutumia lugha za asili za Afrika (Kiswahili) kufundishia lugha za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na maarifa na falsafa asili za Kiafrika (African indigenous languages, knowledge and home grown philosophies) ili kufikia Malengo ya Mpango wa Maendeleo Endelevu na Afrika tuitakayo. Katika kikao kazi hicho, Mhe. Mwinyi ametunukiwa heshima ya kuwa Mlezi wa kwanza wa mpango huo. Pichani, Rais Mstaafu, Mhe. Mwinyi, akiwa na Wajumbe katika Jiji la Durban Afrika ya Kusini wiki hii.

Kikao kazi hicho cha Mpango wa kutumia lugha za asili za Afrika (Kiswahili) kufundishia lugha za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na maarifa na falsafa asili za Kiafrika kimelenga kufikia malengo ya Mpango wa Maendeleo Endelevu na Afrika tuitakayo.

Mwandaaji wa kikao kazi hicho ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mifumo ya Maarifa ya Kijadi (Indigenous Knowledge Systems), Profesa Hassan Kaya kutoka Chuo Kikuu cha KwaZulu Natal akishirikiana na Mgoda kutoka Kigoda cha Mwl. Nyerere ambao ndio waandaaji.

Katika kikao kazi hicho, Mhe. Mwinyi ametunukiwa heshima ya kuwa Mlezi wa kwanza wa mpango huo.

Author: Gadi Solomon