Taasisi ya AU inavyopambana kukuza lugha za Kiafrika

Na Pelagia Daniel

Katibu Mtendaji wa ACALAN, Dk Lang Fafa Dampha, hivi karibuni amekutana na Waziri wa Elimu ya Msingi wa  Kameruni, Profesa Laurent Serge Etoundi Ngoa, 13 Septemba, 2022.

Majadiliano ya viongozi hao yalihusu uteuzi wa muundo wa kitaifa kutumika kama taasisi ya kitaifa ya Chuo cha Lugha cha Kiafrika nchini Kameruni; maendeleo ya sera ya lugha ya taifa, makubaliano  ya Utekelezaji ya Dar es Salaam (Assembly Decision) - Kiswahili kama lugha ya kazi ya AU na Lugha ya Mawasiliano mapana Barani Afrika, wiki ya Lugha za Kiafrika, 24 - 30 Januari na lugha za Kiafrika katika mfumo wa elimu.
Baada ya majadiliano ya viongozi hao matokeo waliyoyapa ilikuwa: Wizara itashirikiana na Utamaduni na wadau wengine kuteua muundo wa lugha ya kitaifa nchini Kameruni, kuwa taasisi ya kitaifa ya Chuo cha Lugha za Kiafrika, maendeleo ya sera ya lugha ya taifa yataanzishwa kwa kushirikisha wadau wote husika;
Pia makubaliano katika Utekelezaji wa mpango wa Dar es Salaam (Assembly Decision) - Kiswahili kama lugha ya kazi ya AU na Lugha ya Mawasiliano Zaidi Barani Afrika utahimizwa hasa katika mfumo wa elimu;
Kamati ya kitaifa itaundwa na wizara zinazosimamia lugha za kitaifa kwa pamoja ili kupanga maadhimisho ya kila mwaka ya Wiki ya Lugha za Kiafrika, kuanzia Januari 24 hadi 30 nchini Kameruni.

Author: Gadi Solomon