Tabia ni ngozi ya mwili

Na Pelagia Daniel

  1. Ukilima pantosha utavuna pankwisha, pantosha ni ufupisho wa pananitosha na pankwisha ni ufupisho wa pamekwisha. Methali hii ina maana ya kuelezea kuwa ukifanya kazi kidogo utapata pato dogo, na ukifanya kazi nyingi utapata pato jingi, hivyo unapaswa kufanya kazi nyingi.
  2. Tabu ya leo ndiyo raha ya kesho, methali hii hutumiwa kumhimiza mtu afanye bidii na asijali shida au tabu anayoipata leo, kwani raha yake ataiona kesho. Lima leo uvune kesho.
  3. Tabia ni ngozi ya mwili, kwa kawaida ngozi ya mwili ni yako huwezi kuibadilisha ukaifanya rangi nyingine. Tabia nayo ni hivyohivyo ni vigumu sana kuibadilisha.

Author: Gadi Solomon