UMEZIMA MSHUMAA, TWAIKUMBUKA NURUYE

  

1.Haya mambo ni magumu, kuyasikia vichwani,

   Anayoyajua MUNGU, si kazi yetu wageni,

   Limetujia wahumu, wala hatukutarajii,

   Umezima mshumaa, twaikumbuka Nuruye

2.Mekuja na kasi ya bomu, ndo mana sisalimii,

   Msije jua nafahamu, Mimi  mwenyewe wa juzi,

   Najua huyu wa tatu, walioweka  misingi,

   Umezima mshumaa, tutakumbuka Nuruye.

3.Naandika hii ya tatu, japo machozi ni mengi,

   Sitaki leo kulaumu, namshukuru mwenyezi,

   Alotujaalia Kuku, tunofurahi ni seti,

   Umezima mshumaa, twaikumbuka Nuruye.

4.Hii namba nne Ndugu,  bado niko Mikocheni,

  Twajua haya ya juu, pua zetu zenda chini,

  Hakuna wa kubisha katu, haya mapenzi ya maanani,

  Umezima mshumaa, twaikumbuka Nuruye.

5.Nakumbuka Chama cha Tanu, na kile  Afro-shirazi,

   Mazuri hatusahau, alotenda hayati Mwinyi.

   Khali aliziruhusu, hii kazi yake Ali,

   Umezima mshumaa, twaikumbuka Nuruye.

6.Alipanga nawalowakuu, kuweka sawa ya nchi,

   Zikamiminika simu, mpaka kapata anko Chali.

   Kule Unguja na huku, sote twalia kusini,

   Umezima mshumaa, twaikumbuka Nuruye.

7.Hizi zangu si sababu, kukosa Amani moyoni,

  Twalia machozi tuu, twaona yalivyo hivi,

  Hi ni pekee kalamu, natengeneza Penseli,

  Umezima mshumaa, twaikumbuka Nuruye.

8.Hii namba nane kwenu, naleta ujumbe hivi,

   Mlokwisha onja tunu, mnajua uhalali,

   Nimetulia si mwehu, nimejitilia koti,

   Umezima mshumaa, twaikumbuka Nuruye.

9.Tuyachukue ya hatamu,  tuyabebe yalomali,

   Kama ukijaza fomu, utafika usaili,

   Hizi ndizo zile duru, wa muumba kurudikwe,

   Umezima mshumaa, twaikumbuka Nuruye.

10.Nimezima vitu vyangu, naomboleza nafsini,

    Nimeshika langu shavu, naitafakari khali,

    Kwaheri kwaheri wetu, umeenda hivi hivi,

    Umezima mshumaa, twaikumbuka Nuruye

Author: Gadi Solomon