USIMDHARAU ANA HAKI ZAKE

 

Msinidhulumu nina haki,

Msinidunishe kwa kuwa msichana,

Nina haki ya kupata elimu kama wengine,

Msinioze ningali mchanga kimawazo.

Niruhusu niboreshe maisha ya usoni,

Baba, mama, mbona mwautesa moyo wangu?

Mawazo yafifisha nafsi yangu,

Ndoto yangu mwaizima pole pole.

Kama upepo upumavyo kutoka kusini hadi kaskazini,

Ndivyo mwayapeperusha maisha yangu,

Niruhusu niboreshe maisha yangu,

Mila na desturi zilizopitwa na wakati zanizuia.

Masomo nipate, ulimwenguni nitambe,

Maisha yapate maana, heshima nipate,

Nijue kuandika, na kutangamana na wengine,

Nisipewe mkuki kwenda shida malishoni .

Imeandaliwa na Sylvester Kibet Kiplagat kutoka Gazeti la Taifa Leo Mtandaoni

Author: Gadi Solomon