-
🔴#LIVE: MORNING MWANANCHI: Aliyepinga hukumu ya miaka 30 jela, sasa afungwa maisha
🔴#LIVE: MORNING MWANANCHI: Aliyepinga hukumu ya miaka 30 jela, sasa afungwa maisha -
Waziri Mkuu Majaliwa awatwisha zigo Ma DC,Wakurugenzi Tanga
Wakuu wa wilaya wachukue hatua kwenye miradi ambayo iliingiziwa fedha 2021 mpaka sasa haijakamilika wahusike wachukuliwe hatua. -
Serikali kuifanyia mageuzi ya kibabe Tazara
Dar es Salaam. Ili kuongeza ufanisi katika usafirishaji mizigo kupitia reli, Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imesema inafanya jitihada kuboresha Shirika la Reli la Tanzania na Zambia, (Tazara) kwa kuongeza uwezo wa idadi ya mizigo itakayosafirishwa na reli hiyo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile alipofanya ziara kwenye ofisi kuu za Tazara na baadaye kwenda katika karakana za shirika hilo zizizopo jijini Dar es Salaam. -
Wanaume Rombo walalamikia nyani wa kiume kusumbua wake zao
Rombo.Wanaume wanaoishi pembezoni mwa mto Mlembea, Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro wamelalamika wake zao kuvamiwa na nyani wa kiume na wakati mwingine kuhatarisha usalama wao.
Wamesema nyani hao wamekuwa ni tishio kwa wake zao na watoto na kwamba wakati mwingine huwavamia wakiwa mashambani, kuiba watoto wadogo wa kike na wakati mwingine wakitaka kuwabaka.
Pamoja na uvamizi huo wa nyani, wamesema nyani hao wamkuwa wakiingia ndani na kula vyakula, kula mifugo na hata mazao yaliyopo mashambani hali ambayo imewafanya kutelekeza mashamba yao wakihofia mazao yao kuliwa na nyani hao.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara, uliofanyika katika kijiji cha Samanga, kilichopo kata ya Kirongo Samanga wilayani humo, wananchi hao walimtaka mbunge wa Rombo, Profesa Adolf Mkenda ambaye alikuwa kwenye mkutano huo ni kwanini nyani hao serikali imeshindwa kuwaondoa kwenye makazi ya wananchi na kuwapa usumbufu huo.
Akijibu kero hiyo ya wananchi katika mkutano huo wa hadhara, Mbunge wa Rombo ambaye ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema hajaridhika na uondoaji wa nyani katika maeneo ya wananchi kwa kuwa bado ni wengi na wamekuwa kero kwenye maeneo ya wananchi. -
Kimbembe, Mkandarasi uwanja wa Mkapa akijbu maswali ya Waziri Ndumbaro na Rais TFF ziarani leo
Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.
#samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano #magufuli #kikwete #mayele #singidabigstars #magoliyamayele #magoliyasimba #magoliyayanga #highlights #azamsportsfederationcup #chama -
Naibu Waziri aibukia NIT atoa maagizo mazito "Miradi ya Rais Samia ikamilike kwa wakati"
Dar es Salaam. Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, (NIT), kimewataka Watanzania kwenda kufanya ukaguzi wa magari yao ikiwa ni njia moja wapo ya kuzuia hatari ya kutokea kwa ajali.
Hatua hiyo imebainishwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa wasiofanya ukaguzi wa magari yao mara kwa mara kwani kufanya hivyo kunapunguza ajali ambazo zimekuwa kama jinamizi linaloendelea kuwatafuna Watanzania walio wengi.
Akizungumza kwenye ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David M. Kihenzile iliyofanyika chuoni hapo leo Septemba 29, 2023, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa, amesema gari linapaswa kuwa bora na ubora unatokana na ukaguzi wa mara kwa mara ili mtumiaji awe na uhakika. -
Simba Yaingia ubaridi dhidi ya Power Dynamos,"ni mchezo mgumu" Ahmed Ally awaita mashabiki Chamazi
Simba Yaingia ubaridi mechi dhidi ya Power Dynamos, "ni mchezo mgumu" Ahmed Ally awaita mashabiki Chamazi -
Exclusive: Mshiriki wa BSS mara mbili amshauri Msigwa jambo la kufanya kuinua vipaji mtaani
Ikiwa ni siku kadhaa tangu aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa aapishwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, mshiriki wa mashindano ya kusaka vipaji ya Bongo Star Search (BSS) mara mbili, Edward Mchiwa amemtaka Katibu Mkuu huyo kuandaa matamasha mengi ya kuinua vipaji vilivyopo mtaani, kwani kuna vipaji vingi ambavyo vinakosa mahali pa kuonekana.
Mchiwa ameyasema hayo alipozungumza na Mwananchi Digital kwenye viwanja maarufu vya Nyerere Square jijini Dodoma. -
Waziri Ummy alia na vijana kutofanya mazoezi, lishe bora 'mchicha tunamwaga maji'
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema watu wanaofanya mazoezi kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza changamoto wanayopitia ni kupoteza maisha wanapofanya mazoezi pembezoni mwa barabara huku akilia na vijana kutopenda mazoezi. -
Naibu Waziri wa Fedha acharuka VIKALI, awa MBOGO kwa taasisi zilizokiuka kanuni za manunuzi ya umma
Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande ameviagiza vyombo husika vya jinai ikiwemo Takukuru kuchukua hatua stahiki kwa taasisi zote zilizokiuka kanuni zilizowekwa akidai kuwa Serikali haitavumiulia Taasisi zinazokiuka sheria, kanuni, miongozi ya ununuzi wa umma na kurudisha nyuma juhudu za kuleta maendeleo zinazofanywa na Serikali.
Kauli hiyo ameitoa leo Ijumaa Septemba 29, 2023 baada ya kupokea ripoti ya ununuzi wa umma kutoka kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ambapo uchunguzi na ukaguzi maalumu uliofanywa na mamlaka hiyo umebainisha kuwa Serikali imepata hasara ya Sh 8.77 bilioni kutokana na ukosefu wa uwajibikaji, ufanisi, uwazi na uadilifu kwenye taassisi 12 zilizochunguzwa.
“Ukizingatia mambo haya matatu utafanya kazi kwa uadilifu, uwajibikaji na uwazi kabisa. Kwanza lolote unalolifanya duniani jua Mungu anakuona, ukiaminiwa, jiaminishe na la tatu subiri kichache upate kingi. Fanyeni uadilifu katika utendaji wenu wa kazi wa kila siku,” amesema Chande. -
PPRA yaibua madudu fedha za umma
Uchunguzi na ukaguzi maalum uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma(PPRA) kwa taasisi 12 umeonyesha kuwa Serikali ilipata hasara ya Sh8.77 bilioni kutokana na ukosefu wa uwajibikaji ufanisi, uwazi na uadilifu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Dk Leonada Mwagike ameyasema hayo leo Ijumaa Septemba 29, 2023 wakati akikabidhi Ripoti ya Tathimini ya Utendaji ya mwaka wa fedha 2022/23 kwa Naibu Waziri wa Fedha Hamad Chande. -
MANDONGA atanganza ngumi mpya, 'Huyu atapasuka....'
Bondia, Karim Mandonga 'Mtu Kazi' ameibukia jijini Mwanza na kutangaza ngumi mpya aliyoiita 'Ngumi Sato, ngumi Sangara' atakaypitumia katika pambano lisilo la mkanda dhidi ya mpinzani wake, Salum Maarifa kutoka jijini Mwanza.
Maoni Mapya