Vitendawili

Na Pelagia Daniel

1.       Mpini mmoja tu lakini majembe hayahesabiki. Mkungu wa ndizi
2.       Msitu ambao haulii hondohondo. Mimba
3.       Mti mkubwa, lakini una matawi mawili tu. Kichwa na masikio
4.       Mti mnyanya mti kerekeche mti ah mti ah!. Ngoma na upatu
5.       Mti wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya thelathini. Mwaka
6.       Mtoto asemea pangoni. Ulimi mdomoni
7.       Mtu mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika tano. Mawazo
8.       Mvua hema na jua hema. Kobe
9.       Mvua kidogo ng’ombe kaoga kichwa. Jiwe
10.       Mwadhani naenda lakini siendi. Jua

Author: Gadi Solomon