Vitendawili

na Pelagia Daniel

1.       Mwalimu analala na mwanafunzi wanamsomea. Kinyesi na inzi
2.       Mwanamke mfupi hupiga kelele njiani. Kunguru
3.       Mwanamke mfupi hutengeneza pombe nzuri. Nyuki
4.       Mwanang’ang’a hulia mwituni. Shoka
5.       Mwepesi, lakini aweza kuvunja nyumba za mji wote. Tufani
6.       Mwezi wangu umepasuka. Kweme
7.       Mzee Kombe akitoa machozi wote hufurahi. Mvua
8.       Mzee Kombe akilia watu hufurahi. Mvua
9.       Mzizi wa miti hutokea mbali. Siafu
10.       Mzungu yuko ndani na ndevu ziko nje. Hindi

Author: Gadi Solomon