Vitendawili

na Pelagia Daniel

1.       Nikija kwenye ndege wananifukuza, na nikienda kwenye wanyama hawanitaki. Popo
2.       Nikimpiga huyu huyu alia. Utomvu wa papai
3.       Nikimpiga mambusu. Puliza kidole wakati unapojikwaa
4.       Nikimwita hunijibu nani. Mwangwi
5.       Nikipewa chakula nala bali natema. Shoka
6.       Nikitembea walio wafu huniamkia na walio hai hukaa kimya. Majani makavu na mabichi
7.       Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo. Kivuli
8.       Ni kitu gani ambacho kutoa ni kuongeza? Shimo
9.       Nikitupa mshale wangu mchana huenda mbali sana, lakini niutupapo usiku hauendi mbali. Jicho
10.       Nikiwaambia ondokeni hukataa, lakini mjomba akitokea wote hukimbia. Umande na jua

Author: Gadi Solomon