Vitendawili

na Pelagia Daniel

1.Nilijenga nyumba yangu nikaiacha bila kuiezeka majani; lakini niliporudi nilikuta imekwisha ezekwa majani. Mahindi machanga

2. Nilijenga nyumba yangu yenye mlango mmoja. Jani la mgomba la nchani

3. Nilimkata alafu nikamridhia. Kupanda mbegu

4. Nilimtuma askari vitani akaniletea kondoo mweusi. Fuko

5. Nilipandia majanini nikashukia majanini. Mwiba

6. Nilipigwa na tonge la ugali la moto nilipopita msituni. Manyigu

7. Nilipitisha mkono wangu chini la ardhi, nikamshika beberu mkubwa sana. Kiazi kikuu

8. Nilipoangalia kwenye magereza ya Wazungu, nikaona wameketi juu ya mabati. Pelele

9. Nilipofika msituni nilikuta chungu cha pure kinachemka. Mzinga wa nyuki

10. Nilipoingia Rumi, alitoka mtu na wake kumi; kila mke na tundu kumi, kila tundu na kuku
kumi; kila kuku na mayai kumi. Mayai, kuku, tundu, wake, kumi kumi kumi. Wangapi
walikwenda Rumi? Hakuna

Author: Gadi Solomon