Vitendawili

1.       Nilipo, juu kuna miiba na chini vivyo hivyo; lakini sichomwi. Ulimi kinywani
2.       Nilipokuwa mchanga nilikuwa na kijikia lakini sasa sinacho. Chura
3.       Nilitembea na mwezangu naye hupita vichakani. Kivuli
4.       Nimechoma fimbo yangu pakabaki pa kushikia tu. Njia
5.       Nimefyeka mitende yote kiungani isipokuwa minazi miwili tu. Masikio
6.       Nimejenga nyumba babu akaihamia kabla mimi sijahamia. Mjusi
7.       Nimekata mti, akaja samba mwekundu akaukalia. Utomvu
8.       Nimekata mti bara ukaangusha matawi pwani. Nzige
9.       Nimekwenda na rafiki yangu kwa jirani, yeye akafika kabla yangu. Sauti ya nziga
10.       Nimemtahiri binti wangu akatoa damu mchana kutwa. Kivuli

Author: Gadi Solomon