Vitendawili

Na Pelagia Daniel

1.       Rafiki yangu ana mguu mmoja. Uyoga
2.       Reli yangu hutandika ardhini. Siafu
3.       Ruka Riba. Maiti
4.       Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajazi kiganja. Nywele kichwani
5.       Shamba langu miti mitano tu. Mkono wa vidole
6.       Shangazi yangu ni mrefu sana lakini hafikii tumbo la kondoo. Njia
7.       Sijui aendako wala atokako. Upepo
8.       Sijui afanyavyo. Nyoka apandavyo mtini
9.       Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa babangu. Ni nani huyo? Mtoto wangu
10.       Subiri kidogo! Miiba

Author: Gadi Solomon