Vitendawili

Na Pelagia Daniel

1.       Wanao wakati wao wa kuringa, nao ni weupe kama barafu. Nyota
2.       Wanapanda mlima kwa makoti mazuri meusi na meupe. Vipepeo
3.       Wanastarehe darini. Panya
4.       Wanatembea lakini hawatembelewi. Macho
5.       Watoto wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka. Maboga
6.       Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu. Fuu
7.       Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu. Jogoo
8.       Watoto wangu wote wamebeba vifurushi. Vitovu
9.       Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao? Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono, walioona ni macho mawili, waliochuma ni vidole vitano vya mikono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni mdomo
10.       Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu. Kuku, katani au mahindi

Author: Gadi Solomon