Vitendawili

na Pelagia Daniel

1.           Chumba changu kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo. Pazia
2.           Chungu changu cha udongo hakipasuki kikianguka. Mjusi/Panya
3.           Chungu kikubwa sana chenye kifuniko kikubwa sana. Dunia na mbingu
4.           Dada yangu akitoka kwao harudi kamwe. Jani likwanyukapo
5.           Dada yangu kaoga nusu. Jiwe mtoni
6.           Drrrrrh1 Ng’ambo. Daraja la buibui
7.           Dume wangu amelilia machungani. Radi

8.           Fahali wa ng’ombe na mbuzi wadogo machungani. Mwezi na nyota angani
9.           Fika umwone umpendaye. Kioo
10.           Fuko kajifukia, mkia kaacha nje. Kata mtungini
11.           Funga mizigo twende Kongo. Mikia ya mbwa
12.           Hachelewi wala hakosei safari zake. Jua

Author: Gadi Solomon