
Na Pelagia Daniel
- Yajapo yapokee, makusudio ya neno ‘yajapo’ (yanapokuja). Yaani unapojiwa na mambo, hasa mabaya au mazito, yapokee. Usibabaike, usilalame wala usipite ukishtakia watu. Pambana nayo wewe mwenyewe kiume. Methali hii inatufunza kuwa na ustahamilivu na moyo wa kuweza kupambana na matatizo, tuwe tayari saa zote kwa litakalotokea.
- Visima vya kale havifukiwi, si vizuri kuvifukia visima vya zamani, huenda siku moja vikafaa. Methali hii hutumiliwa wazee-kwamba wasiachwe au wasitupwe ovyo ovyo bila ya kutazamwa kwa sababu ni wazee. Maarifa waliyonayo ni mengi, kwa hivyo wakati wowote wanaweza kutufaa.
- Vyanda vya miguu havivishwi pete, ‘Vyanda’ maana yake ni vidole. Vidole vya miguu havivishwi pete kwa kuwa vikivishwa havipendezi wala havielekei. Methali hii hutumiwa kumwambia mtu kwamba asimpe mamlaka au madaraka mtu mjinga. Akipewa mamlaka mtu kama huyo, mambo yataharibika.
Maoni Mapya